Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baada ya jaribio la kwanza kabisa la kumpindua mwaka 1972, Watanzania tuliokuwa tukiishi Uganda tulialikwa kukutana naye Idi Amin Dada katika ukumbi wa Kampala Conference Center. Kwa woga tulienda na aliongea nasi kwa muda wa saa nzima na baada ya mkutano alisimama mlangoni kumsalimia kwa mkono kila moja wetu aliyehudhuria. Wakati huo mambo hayajaharibika sana ingawa Mwalimu alikuwa amekataa katakata kumtambua.Asante mkuu.
Rafiki yangu ni Mganda, ananiambia kwenye mtihani ilikuwa ukikosea hivyo vyeo umefeli swali. Inabidi uvikariri vyeo vyote vya presedaa.Alivyojiita...
His Excellency President for Life Field Marshal Al Hadj Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Sea and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular...
Operation yake ya kuwafukuza Wahindi na kuwagawia washikaji wake biashara, majumba na mali zao ilijulikana kama Operation Mafuta Mingi, OMM!
Alivyojiita...
His Excellency President for Life Field Marshal Al Hadj Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Sea and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular...
Operation yake ya kuwafukuza Wahindi na kuwagawia washikaji wake biashara, majumba na mali zao ilijulikana kama Operation Mafuta Mingi, OMM!
Propaganda ni kitu cha ajabu sana mtu unapandikizwa chuki wakati hata ugomvi haukuhusu! Tulipandikizwa chuki na kumchukia sana huyu bwana. Nakumbuka wakati tukiwa jeshini kuna wimbo tulikuwa tunaimba "Idd Amini akifa, mimi siwezi kulia, tutamtupa Kagera awe chakula cha mamba".Hizo ni propaganda tupu tukiaminishwa tu ili kuhalalisha kuivamia uganda. Sisi ndo tuli ikosea uganga kwa kuweka kambi za waganda kwa ajili ya kumpindua. Kina museveni walipewa kila msaada.
Amin alikua dictator lkn ilibidi iwe hivo kwani hali ya usalama haukua nzuri kwani alikabiliwa na upinzani wa ndani ma nje
Idi Amin Dada alizaliwa 1923 na alifariki mwezi wa nane 2003 alikua raisi wa tatu wa Uganda, alitawala 1971 mpaka 1979. Kyalow
Angekuepo angukua kashajiita W.C.MbonaHis Excellency
President for Life Field Marshal
Alhaj Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO,
MC, CBE
vyeo hadi kwenye viatu
Angekuepo Leo hii angekua kashajiita hadi W.C.B Mbona
Asante sana, this is very interesting part of the story. Nitaendelea nipeni muda. Kuna Maisha ya binafsi ya Amini.
His Excellency
President for Life Field Marshal
Alhaj Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO,
MC, CBE
vyeo hadi kwenye viatu
No,Anakaaga kaburini"
Angejichanganya aone...! [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]Waandishi kama ninyi tutawasoma sana. Niliwahi kusikia ushuhuda mmoja wa Askofu wa Madhehebu ya Kipentekoste ambaye alikamatwa na Idi Amin kipindi kile cha kuuawa kwa Askofu Mkuu Janaani Luwum. Askofu huyo alipelekwa "Nile Mansion Hotel" ambayo kipindi fulani ilikuwa Command Post ya mheshimiwa. Alisema namnukuu: "Unanijua mimi? Amin aliniuliza! Nikamjibu. Ndiyo nakujua! Wewe ni Field Marshall Iddi Amin Dada; Commander in Chief wa Uganda Army; Life President wa Republic of Uganda; Conqueror of the British Empire; Chairman wa OAU na Wewe ni Jogoo ya Afrika! Iddi Amin aliniachia huru akasema ['Huyu ananifahamu vizuri sana achia yeye!'] ndipo nikatolewa Nile Mansion. Kabla sijaondoka nilimwomba nimwombee Life President wangu! Nilipigwa picha na vyombo vya habari nikimwombea Amin." Mwisho wa nukuu (Askofu Daniel Kasmiri - Plateau, Eldoret, Kenya August 1984 - Victorius Living Ministries Church Leaders Conference}.