IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

Asante kaka kwa maoni yako kama raia ila tuchambue kama wadau wa kijeshi karibu sana
Brother, mbona kila anaetoa maoni tofauti na mtazamo wako unaishia kumuita "raia"?

Can't we discuss facts without calling eachother "names"?


Let's debate the facts!


Umesema IDF ni jeshi bora zaidi, wanaopinga wanatakiwa kupewa facts ili waelewe. Sio kuitwa "raia".

As a matter of fact, wewe pia ni "raia".
 
Mimi najadili kwa upande wa mtazamo wa kijeshi sababu najadili mada ya kijeshi.Lakini nawashukuru sana michango yao kwa mtizamo wa kiraia ila ningependa tujadili kwa mitazamo ya kijeshi mada hii.Karibu tujadili kaka kwa mtazamo wa kijeshi ndugu yangu kama nilivyofanya kuhusu yom kippur event,s kumuhusu kamanda Ariel Sharon siku nne baada ya vita vya yom kippur kuanza nimeelezea hapo juu
 
Mkuu ninasubiri sana hii,nakumbuka kwenye Documentary Wazazi wake walivyoambiwa "Yoni is no more" na mdogo wake Benjamini walivyopokea ile taarifa na ilivyowaumiza.Nilizidi kumchukia zaidi Idd Amin.
 
Mkuu ninasubiri sana hii,nakumbuka kwenye Documentary Wazazi wake walivyoambiwa "Yoni is no more" na mdogo wake Benjamini walivyopokea ile taarifa na ilivyowaumiza.Nilizidi kumchukia zaidi Idd Amin.
Kuna askari mstaafu niliwahi kuona mahojiano yake na kituo kimoja cha televisheni pale Kampala alikua anajinadi kua yeye ndie aliempiga risasi zilizomjeruhi Yoni na kumsababishia umauti.Na alipongezwa na Amin na kupandishwa cheo kwa mujibu wa maelezo yake na mwandishi wa habari ile
 
Unajua kwanini wataalamu wa mambo ya kijeshi tunasema IDF ni jeshi bora kabisa linapokuja suala la kupambana na mpinzani kwenye uwanja wa vita.Ebu tuangalie vita vya yom kippur na jinsi gani vikosi vya IDF viliweza kustahimili mashambulizi ya kushitukiza ya vikosi ya jeshi la Syria.Kwanza tuangalie mazingira ya maeneo ya uwanda wa vilima vya Golan hasa eneo la kaskazini ambalo baadae lilikuja kujulikana kama"BONDE LA MACHOZI".Ni eneo ambalo katika hatua za mwanzo za mashambulizi ya kushitukiza ya vikosi vya Syria wanajeshi wengi wa IDF waliuawa na wengine kuchukuliwa mateka wakiwa majeruhi.Zilikua siku nne mfululizo za mashambulizi kutoka angani na kutoka aridhini,na IDF walijitahidi kuzuia vikosi vya Syria visivuke red lines licha ya mashambulizi makali kutoka kwao kupitia vifaru vya T-55 na T-65,anti-aircraft missiles aina ya (SA2-3-6-7) na (Sagger anti-tank missiles) na ndege za kivita za kirusi za Mig,s 21,s na 23,s na 29,s na SU -22,s na SU-24,s .Ilikua October 6 saa 2pm mwaka 1973 wakati majeshi ya Syria yamesogea zaidi na kuanza kurusha makombora kutokea nyuma kupitia kikosi chake maalumu cha mizinga lengo likiwa askari wa miguu wa jeshi la Syria wapate mwanya na urahisi wa kuingia uwanda wa vilima vya Golan kupitia eneo hili la kaskazini sababu ni tambarare na sawaziko na ni njia sahii ya kupitisha vifaru na askari wa miguu eneo lenye ukubwa wa maili tatu au nne kwa mahesabu ya haraka haraka.Japokua walishitukizwa askari wa IDF waliokua pale kwa mda wa masaa mawili hawakurudi nyuma kitaalamu tunaita RWD ambayo ina maelezo yake ya kina na iliasisiwa na makamanda wa IDF miaka ya 1970,s ila walipata hasara kubwa sana maana zaidi ya vifaru 200 vya M48A3 na M60A1 viliharibika either kwa matatizo ya kiufundi au kushambuliwa na mpinzani wao kwenye uwanja wa mapambano. Walipambana mfululizo kwa siku mbili ila siku ya tatu majeshi ya Syria yalianza kufanikiwa kusogea mbele na sasa hapa ndipo ule ubora wa majeshi ya IDF kubadili mbinu katika uwanja wa mapambano ulianza kuonekana baada ya kuona wakiendelea kuzuia tu watazidiwa.Kwanza wanajeshi wa IDF walirudi nyuma kama wanakimbia uwanja wa mapambano lengo likiwa kuwezesha vikosi vya vifaru aina ya T-55 na T-65 vya vikosi vya Syria viingie kwenye mtego,huwezi kutumia mbinu ya RWD kama hujamtengenezea mtego mpinzani wako kwenye uwanja wa vita,rudisha nyuma askari wote wa miguu afu mwachie uhuru mpinzani asogee akidhani unakimbia mapigano.Vifaru vya T-55 na T-65 vilivyotengenezwa urusi ni bora zaidi kwa kupigana usiku kwa sababu ya uwezo wake wa miundo mbinu ya kuona usiku ila mchana vinawahi kupata joto na kujam na ni rahisi kuvishambulia kutokea angani kwa sababu ya mwendo wake mdogo vinapopata joto na kua vinajam vikitumika mda mrefu kwenye uwanja wa mapambano.Wakati wanajeshi wa IDF wanarudi nyuma kutengeneza mtego walikua na nia mbili,moja kupunguza risk na majeruhi maana wengi waliuawa na wengine kuchukuliwa mateka siku mbili za mwanzo za mapigano na mbili kumtegea mpinzani aingie uwanda wa chini kabisa wa vilima vya Golani ili awe rahisi kuonekana hasa vile vifaru vya T-55 na T-65 ili hii mbinu ya RWD iwe na matokeo chanya.Ubora wa IDF unaonekana hata kwenye stracture ya uongozi sababu kamanda aliyepo uwanja wa mapambano ana uwezo wa kupanga mbinu zake binafsi ili kumdhoofisha mpinzani haraka kwenye uwanja wa mapambano bila kusubiri amri kutoka juu.Tofauti na majeshi mengi duniani ambayo yanasubiria amri kutoka makao makuu ndio yafanye chochote kwenye uwanja wa mapambano...............NITAENDELEA KUWAJUZA JE HII MBINU YA RWD YA IDF ILIFANYA KAZI KATIKA KUZUIA MAGARI YA DERAYA NA ASKARI WA MIGUU NA VIFARU VYA JESHI LA MPINZANI SYRIA VILIVYOKUA VINASONGA MBELE KATIKA SIKU YA TATU YA MAPIGANO KUINGIA KWENYE UWANDA WA BONDE LA MACHOZI?????
 
Unawapima kwa vita vyake na Hamasi. Ili tulione bora alianzishe pale na muirani basi
 
Katika wale Comandos waliokuja kwenye hiyo operation,kuna watano walirudi tena Uganda nadhani 2020 wakiwa watu wazima sana. Walitembelea uwanja wa Entebbe na wakawa wanaelezea kile walichokifanya usiku ule. Walikutana pia na huyo aliyejinasibu kuwa alimjeruhi Yoni,ni jamaa mmoja mtu wa Kaskazini mwa Uganda huko anatokea Lira au Guru.Niliona pia hayo mahojiano yake.
 
Niliona habari yao you tube pia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…