IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

I rest my case,naona nyinyi kumbe mna mambo yenu binafsi na mnajuana kitambo.Kila la kheri kwenye kutunishiana misuli ya nani zaidi.
 
ITR,
Hakika uzi ungenoga sana.

Nilianza na vituko vya Sadat wakati wa Yom Kippur nikieleza mazungumzo ya Heikal na Commander in Chief.

Yeye hakutaka.

Ilikuwa tukitoka pale nimpeleke kwa majeshi mengine ili afananishe majeshi hayo na IDF.

Nilikusudia kumpeleka Yugoslavia alione jeshi la Partisan Army la Field Marshall Josip Tito anapambana na jeshi la Wajerumani lenye Air Force na kila aina ya silaha hadi mbwa aina ya German Shepherd.

Wayugoslavia wana nini?

Wana moyo na ari ya kuikomboa nchi yao hata kama watauliwa wote.
 
Nyamizi,
Ndiyo sababu nilimkataza asiweke picha.
 
I rest my case,naona nyinyi kumbe mna mambo yenu binafsi na mnajuana kitambo.Kila la kheri kwenye kutunishiana misuli ya nani zaidi.
Nyamizi,
Sina chochote binafsi na yeyote hapa JF.

Wala sijuani na yeyote hapa JF.
Wala sijatunisha msuli.

Nguvu yangu ipo katika kalamu yangu.
Wewe ndiyo umeniandikia kuhusu Nelson na nimekujibu.
 
Mkuu hongera sana kwa mada hii Mimi ni miongoni naipenda kufuatilia mada za kijasusi na kijeshi
Isipokuwa nakushauri

kuwa mvumilivu wa kupokea mawazo ya wachangiaji ,naona unataka kuonyesha kwamba una uzoefu kwenye vita na kwamba kila unachoelezea umeshiriki,
Lakini ukweli ni kwamba vitu vingi umechukua kwenye maandiko mbalimbali kama sio vitabu,
Nimekufatilia muda mrefu unalazimisha mawazo unayotaka wewe
Acha watu wafunguke wasomaji watapima wenyewe

Pia ukishaweka mada kwenye hii forum inakuwa Mali ya Jf sio yako Tena so Kila member wa Jf ana uhuru wa kuchangia openly
Ahsante mkuu
 

Naomba tuendelee kuchangia Kwa uhuru kabisa bila chuki kwa lengo la kuelimishana na kuburudishana

Lakini tukumbuke michango yetu halifanyi Idf au mossad kuwa Bora kama sio Bora
Pia michango yetu haiwezi kulidhoofisha Jeshi la Israel au Mosssd ikiwa ni bora
ukweli tutaendelea kushuhudia kwenye battlefield
 
Gift...
Ukishaitaja Israel umetaja dini.
Ukishaitaja Israel umeitaja nchi ambayo ni taifa na dini kwa pamoja.

Unahitaji kwanza mleta mada alijue hili.

Unapoitaja Hizbullah jua umewataja Shia.

Unapoitaja Misri jua umewataja Ikhwan Muslimin (Muslim Brotherhood).

Inawezekana mleta mada haya hakuyajua toka awali.

Sasa anajikuta katika hali ambayo hakutegemea.

Anauliza Uislam unaingiaje katika Waarabu kukabiliana na Wayahudi?

Haya mambo yanahitaji mtu kusoma au kufanya utafiti angalau kidogo kujua nini ni nini.

Vinginevyo utajitaabisha mwenyewe bure na wakati mwingine utawataabisha wengine.

Kuhusu ubora wa IDF mleta uzi yeye alishaamua kuwa IDF inashinda majeshi yote duniani yaliyopo na yaliyopita.

Ndipo kuna mahali hapa nikauliza kama anajua historia ya Partisan Army ya Yugoslavia chini ya Field Marshall Josip Tito Vita VyaPili VyaDunia (1939 - 1945).

Au kama amepata kusoma historia ya Ho Chi Minh Trail wakati wa Wavietnam walipokuwa wanapigana na Wamarekani.

Nimesimama nje ya Chuo Cha Azhar, Cairo mwaka wa 1991 chuo kikubwa sana duniani cha Waislam
 
Israel watu wamekaa kanisani weeh wakachukua mahaba ya kiimani sasa wanaiabudu nchi.Hata uhalifu wanaoufanya hawauoni wanaipaisha tu nchi.Miaka mingi ijayo utakuja ambiwa afrika kusini ni ya watu weupe.Kama palestina ilivyofanywa.Jinga kabisa watu.
 

Kiukweli chanzo kikuu Cha vita ya mashariki ya Kati imebase zaidi kwenye dini ,
Na ikumbuke kwamba taifa la Israel ndo ambalo Lina maeneo matakatifu ya dini kuu zote tatu ukristo uislam na uyahudi


Tukirejea kwenye mada tunajadili ubora wa Idf na Massod baada ya kuundwa kwa upya taifa la Israel 1948,
Tukianza kutaja na operesheni za nyuma tunakuwa hutuetendei haki Uzi huu ingawa hili jukwaa ni huru pia
 
Gift...
Hakuna ubaya kueleza historia za vita vilivyopita yote haya ni katika kueneza elimu.

Halikadhalika kufanya mjadala upendeze zaidi.

Mathalan ukieleza mauaji ya Shatila ipo haja na kugusia pia mauaji ya My Lai Vietnam.

Huwezi kusema mauaji ya My Lai hayakuwa Mashariki ya Kati.
 
 
 
Mzee wetu bwana,huwa kila ukipata ki upenyo lazima uchomekee na picha zako kuonyesha umetembea kila pembe ya hii Dunia hata kama haihusiani na mada.

Unaonaje ukianzisha mada maalumu kwa ajili ya kutuonyesha sehemu zote ulizotembelea na huko ukatuwekea picha zote ili tuweze kukusoma vizuri?
 
Nyamizi,
Kuwa naweka picha kujionyesha na hazihusiani na niliyoandika si kweli.
Nijionyeshe nini?

Utafikiri hivyo ikiwa hizo picha zinakuudhi.
Ikiwa picha hizo zinakuudhi tatizo litakuwa kwenye moyo wako.

Picha zote ninazoweka hapa ni kudhihirisha ukweli wa kauli yangu ili moyo wako usije ukakuchezea kukuambia kuwa niliyoandika si kweli.

Nimepata kuandika katika blog yangu mohamedsaidsalum.blogspot.com makala: "From Kipata to Cape Town" mwaka wa 2006.

Kipata ndiyo mtaa niliozaliwa.

Nilikuwa Cape Town siku moja na kaka yangu pamoja na wake zetu restaurant tunakula chakula cha usiku.

Huyu kaka yangu yeye ni Prof. wa Genetics akifanya kazi huko miaka hiyo.
Mama yetu amekufa sisi wadogo sana kwa hiyo hakutuona tukikua.

Nilipomtazama kaka yangu na pale tulipokuwa nikamkumbuka mama yetu moyoni lakini sikusema kitu.

Ilinijia simanzi.
Nikawa nawaza rehma zake Allah kwangu mimi na kwa kaka yangu.

Kila nchi alikokuwapo kaka yangu akifanyakazi mimi nimefika kuanzia Uingereza, Uholanzi hadi Afrika Kusini.

Paliponishinda kufika ni Papua New Guinea.
Hii nchi iko mbali sana.

Kuweka picha zote zilizomo katika makala hiyo ni nyingi mno.
In Shaa Allah nitaweka link ustafidi na nafsi yako.

Picha niliyoweka hapa jana nipo Azhar, Cairo ilikiwa ni makala IDF.
Naamini hii ndiyo iliyokushtua.

Niliandika kuhusu Ikhwan Muslimin, Hizbullah na Wayahudi.

Elimu yote kuhusu Uislam na dini nyingine inasomeshwa Azhar na hapo nimefika na Cairo yenyewe nimekwenda mara mbili.

Sehemu nyingine yenye elimu kubwa kuhusu dini ya Kiislam na nyinginezo na historia ni Yemen na nimefika pia.

Ukipenda naweza nikakuwekea picha ikiwa hutotabika na picha.

Naweza pia nikakuwekea picha ya Msikiti Mkuu wa Paris ambamo Imam wa msikiti huu aliwaficha Wayahudi wasiuliwe na Hitler Vita Kuu Vya Pili Vya Dunia (1939-1945).

Hii ni historia maarufu.
Paris pia nimefika mara mbili.

Uzi huu wa IDF umenikumbusha mengi.

Nimefika Berlin ipo kumbukumbu kubwa ya Wayahudi na hapo ulinzi wake mkali sana.

Nimefika.
Ikiwa si dhiki kwako naweza nikakuwekea picha.

Sielezi haya kwa kujidai bali kwa kuthibitisha yale niandikayo kuwa nayajua kwa kutafiti na kufika nchi na maeneo husika.

Sikutegemea kuwa uthibitisho wa hizi picha itakuwa kero kwako.
Nakutaka radhi.

 
Mzee said mohamed samahani kusema haya ndugu yangu ila una tatizo linaloitwa "Mjibwanu"kwa kiswahili kisicho rasim cha kitabibu.Unataka kuonekana kama kila kitu unajua na ukiongozwa njia sahii unapata tatizo linaloitwa kwa kiswahili cha kitabibu "Sonona".Nakuelewa mzee wangu na itikadi zako katika kuyasimamia yale unayoyaamini.Ni sawa wa sio kosa na ndio maana ya upana tambuzi katika uwanja wa majadiliano.Karibu tuendelee
 
Samahani kwa kusema haya ndugu yangu ila mzee wangu na jitani yangu kaka Said mohamed ana tatizo linaoitwa kwa kiswahili kisicho rasmi cha kitabibu"Mjibwanu".Namuelewa mzee wangu sio kosa ni sawa kabisa na ndio maana ya upana tambuzi katika uwanja wa majadiliano
 
Israel watu wamekaa kanisani weeh wakachukua mahaba ya kiimani sasa wanaiabudu nchi.Hata uhalifu wanaoufanya hawauoni wanaipaisha tu nchi.Miaka mingi ijayo utakuja ambiwa afrika kusini ni ya watu weupe.Kama palestina ilivyofanywa.Jinga kabisa watu.
Upo sahii kaka ila upo nje ya mada.Karibu tuendelee
 
Mada nimeleta mimi mkuu.Lakini wadau wanatoka nje ya mada kwa kuingiza siasa na itikadi na mahaba ya kinasaba kwenye uchambuzi wa kitaaluma wa maswala ya ujasusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…