Nyamizi,
Kuwa naweka picha kujionyesha na hazihusiani na niliyoandika si kweli.
Nijionyeshe nini?
Utafikiri hivyo ikiwa hizo picha zinakuudhi.
Ikiwa picha hizo zinakuudhi tatizo litakuwa kwenye moyo wako.
Picha zote ninazoweka hapa ni kudhihirisha ukweli wa kauli yangu ili moyo wako usije ukakuchezea kukuambia kuwa niliyoandika si kweli.
Nimepata kuandika katika blog yangu mohamedsaidsalum.blogspot.com makala: "From Kipata to Cape Town" mwaka wa 2006.
Kipata ndiyo mtaa niliozaliwa.
Nilikuwa Cape Town siku moja na kaka yangu pamoja na wake zetu restaurant tunakula chakula cha usiku.
Huyu kaka yangu yeye ni Prof. wa Genetics akifanya kazi huko miaka hiyo.
Mama yetu amekufa sisi wadogo sana kwa hiyo hakutuona tukikua.
Nilipomtazama kaka yangu na pale tulipokuwa nikamkumbuka mama yetu moyoni lakini sikusema kitu.
Ilinijia simanzi.
Nikawa nawaza rehma zake Allah kwangu mimi na kwa kaka yangu.
Kila nchi alikokuwapo kaka yangu akifanyakazi mimi nimefika kuanzia Uingereza, Uholanzi hadi Afrika Kusini.
Paliponishinda kufika ni Papua New Guinea.
Hii nchi iko mbali sana.
Kuweka picha zote zilizomo katika makala hiyo ni nyingi mno.
In Shaa Allah nitaweka link ustafidi na nafsi yako.
Picha niliyoweka hapa jana nipo Azhar, Cairo ilikiwa ni makala IDF.
Naamini hii ndiyo iliyokushtua.
Niliandika kuhusu Ikhwan Muslimin, Hizbullah na Wayahudi.
Elimu yote kuhusu Uislam na dini nyingine inasomeshwa Azhar na hapo nimefika na Cairo yenyewe nimekwenda mara mbili.
Sehemu nyingine yenye elimu kubwa kuhusu dini ya Kiislam na nyinginezo na historia ni Yemen na nimefika pia.
Ukipenda naweza nikakuwekea picha ikiwa hutotabika na picha.
Naweza pia nikakuwekea picha ya Msikiti Mkuu wa Paris ambamo Imam wa msikiti huu aliwaficha Wayahudi wasiuliwe na Hitler Vita Kuu Vya Pili Vya Dunia (1939-1945).
Hii ni historia maarufu.
Paris pia nimefika mara mbili.
Uzi huu wa IDF umenikumbusha mengi.
Nimefika Berlin ipo kumbukumbu kubwa ya Wayahudi na hapo ulinzi wake mkali sana.
Nimefika.
Ikiwa si dhiki kwako naweza nikakuwekea picha.
Sielezi haya kwa kujidai bali kwa kuthibitisha yale niandikayo kuwa nayajua kwa kutafiti na kufika nchi na maeneo husika.
Sikutegemea kuwa uthibitisho wa hizi picha itakuwa kero kwako.
Nakutaka radhi.
Kipata Street 1970s Regent Park Mosque, London 1991 Kushoto Mume wa Alma Sykes, Yahya Lweno, Lusaka 1993 Le Havre, France...
mohamedsaidsalum.blogspot.com