Katika hali ngumu kabisa ile asubuhi vikosi vya IDF,s katika majengeo yao ya mitego ya(RWD) na wakiwa wachache kimahesabu na wana vipigia mizinga na mota 147 na vifaru 290 wanakutana na divisheni thabiti mbili au tatu za jeshi la Syria SSMF zikiwa na vifaru vya T-55 na T-62 zaidi ya 300 na vipigia mzinga na mota zaidi ya 100 wakiwa tayari kufa au kupona kurejesha eneo lao la vilima vya Golan katika oparesheni waliyokua mwanzoni wanaiita Al-Owda kabla majenerali wa kimsiri kuikataa na kuibadilisha na kua operation Badhr kila kitu kilipangwa Cairo.Basi tuendelee na kilichotokea uwanja wa mapambano.Wanajeshi wa IDF wote waliokua kwenye vifaru walichukua cover,s za aina ya pembe tatu(Angle to angle coverage) na mtambao wa chini.Wakati wanajeshi wa Syria SSMF cover zao zilikua head to head na mtambao wa chini pia.Kuna vikosi pale uwanja wa mapambano vilikua na kazi ya kuharibu vifaru vya adui kwa kutumia RPG,s na anti-tanks missels kwa pande zote mbili.Sasa ule mtego wa IDF wa (RWD) ukaanza kufanya kazi sababu karibia wanajeshi wote wa vikosi vya Syria upande ule walikua wameingia ndani kabisa ya uwanda wa vilima pamoja na vifaru sindikizi vyao na walikua wanaonekana kwa urahisi kuweza kuwashambulia na kuwateka au kuwarudisha nyuma.Sasa suala la ubunifu wa IDF likaonekana hapa maana bunduki za askari wa miguu walizokua wanatumia zilikua ni Berreta M1951 na BT/AT52 na UZ 9mm SMG ambazo zilikua tofauti kabisa na wapinzani wao kiubora na hapa ndipo tunapoona ubora wa jeshi la IDF.Kwa upande wa jeshi la Syria SSMF wanajeshi wake walikua wanatumia AK 47 na Hakim rifle,s