Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Adui Jordan aligundua kwa maumivu makubwa kuwa Wapalestina hawadhaminiki. Bado Jordan ikagundua Waarabu wengine ni wanafiki wanataka kutoa msaada wa vyakula na dawa alafu wanaopigana wawe Jordan waumie. Anayetaka kuipiga Israel apeleke jeshi mwenyewe na humuoni. Sasa cha kufia nini.
Adui Misri yeye ana hasara akiiwekea vikwazo vya usafiri Israel. Kwani hujui kuweka naval blockade ni act of war. Sasa Misri ina ubavu wa kuingia vitani na Israel?
Au hujui kama Israel iliishambulia Misri tarehe 5 June baada ya Misri kuifungia access ya maji Israel tarehe 22 May.
Misri izuie meli kuingia Israel alafu Israel ipitishe meli makusudi, ili Misri itimize kufungia lazima izishambulie kama isiposhambulia basi katazo lake ni batiri. Sasa unataka Misri ichokoze nyuki? Au unalinganisha Misri na Houthi wavuta shisha, wale Houthi utaitetea Yemen useme ni wahuni kwahiyo Wayemeni wasamehewe kwa makosa ya wachache. Sasa jeshi la Misri lenye serikali rasmi na utulivu lifabye hivyo utaiteteaje Misri.
Na kwa bidhaa nyingine, bado Misri ina hasara kuinunia Israel. Wote wanafaidika si ni majirani.
Umekuwa msemaji wa Jordan?