Idris Sultan afikishwa katika Mahakama ya Kisutu. Ashtakiwa kwa kumiliki laini ya simu isiyo na jina lake. Aachiwa kwa dhamana

Idris Sultan afikishwa katika Mahakama ya Kisutu. Ashtakiwa kwa kumiliki laini ya simu isiyo na jina lake. Aachiwa kwa dhamana

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
kumbusho_dawson_20200527_2.jpg

Mchekeshaji huyu alikuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay kwa takriban siku 8 akifanyiwa mahojiano.

Haijajulikana ni mashtaka gani atasomewa lakini kwa wa mujibu wa Polisi, walikuwa wakimuhoji kwa tuhuma za kujaribu kuharibu ushahidi na makosa mengine ya Kimtandao.

Endelea kufuatilia....
1590569850475.png

UPDATES
Mchekeshaji Idris amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na mwenzake Innocent Maiga na kusomewa mashtaka yao

Katika shtaka la kwaza, Idris pekee anatuhumiwa kutumia laini yenye namba 0753 617621 ambayo haijasajiliwa kwa jina lake bali kwa jina la Innocent Maiga

Katika shtaka la pili, Innocent pekee anatuhumiwa kushindwa kuripoti ubadili wa umiliki wa laini hiyo baada ya Idris kuanza kuitumia



UPDATE
Idris amepata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutumiza masharti yakuwa na wadhamini wawili na bond ya TZS 15,000,000/-

Kesi itatajwa tena Juni 09, 2020

photo_2020-05-27_13-28-48.jpg
 
Sultani Alifanya Dhihaka.
Kwanza tambueni Raisi JP Magufuli, ni Raisi halari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Hivyo anastahili kuheshimiwa na kila raia wa nchi hii, bila kujali ulimpigia kura au la.

Idrisa kama Msanii anayetazamwa na watu wengi Aliidhihaki Picha ya Raisi na Watanzania wengi waliiona video clip yake.

Je, kama msanii ile video ililenga kufanya nini ktk jamii yetu.

Idrisa anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa wengine.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha wamnyooshe ili akitoka akumbuke enzi za zamani dingi akijamba ulikua huruhisiwi kucheka...

lazima uwe na adabu bhana biashara za kutafuta kiki za k'jinga zilishapitwa na wakati.

si bora angevua taulo kama Calisa kuliko kumchezea simba sharubu ?
 
Yaan ukiingalia Ile clip ya IS lazima uchekee tenaa [emoji38][emoji38] ,, btw naamini Mhe Rais Hana muda na hii ki2, ana Mambo mengi ya kufanya kulitumikia taifa letu, so hao police/mahakama kuendelea kudeal nae ni kumuongezea umaarufu zaidi

Kidumu chama tawala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom