Idris Sultan akamatwa na Polisi, anahojiwa na Kitengo cha Makosa ya Mtandaoni

Idris Sultan akamatwa na Polisi, anahojiwa na Kitengo cha Makosa ya Mtandaoni

Ndivyo inavyosemekana... chanzo hi hiyo picha...

Ila ngoja tuone polisi na mahakama watasema nini haswa tatizo...


Cc: mahondaw
 
View attachment 1455154
Moderator naombeni sana msiunge huu uzi.

Yule msaani amepelekwa selo kwa sababu ya ile clip yake akionekana kuicheka hii picha? au kuna kingine?

Kama ni kuicheka hii picha,kosa lake ni lipi? amedhalilisha waliopo kwenye picha?kivipi? waliochekwa wameshtaki?wamepata damage gani?

Ukiacha yote hayo,labda pengine kwa sababu kwenye picha kuna rais,lakini ni kweli hicho kicheko kinakuwa big deal mpaka dola kuacha mambo ya msingi na kudeal na jambo kama hili?

Mambo haya tulizoea kuyasikia nchi za madikteta kama Robert Mgabe lakini leo hii tunayahuhudia hapa kwetu Tanzania
Ningekuwa nimevaa balakonya ningesema kitu

Jr[emoji769]
 
Hivi umeyaelewa maswali aliyouliza mtoa maada?

Hiyo nayo mada. Watz tuache utani. Hata mie picha imenifurahisha. Sasa wewe mtu kaitwa polisi unateseka na kuanzisha UMBEYA. Nia yako kutaja neno Dikteta. JPM kahusikaje Hapo. Wanasema wapiga majungu Pua zinawasha na mdomo akiwa na Siri. Sasa wewe hata Siri yenyewe huna Unawashwa na Nini.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nani alikwambia kua alimcheka magufuli wakati kwenye picha wako watu watatu?.Na isitoshe unaweza vip kutafsiri kicheko cha mtu nakusema kafanya dhihaka wakati ata ukifurahi pia unaweza kucheka.inawezekana wewe ndo umetafsiri hicho kicheko vibaya kwa mtazamo wako lakini maana ya mchekaji isiwe hiyo uliyowaza wewe.
Uwezo wa kuelewa fikra ya uwasilishaji wa mawazo kusudio ya mtu mwengine ni matokeo ya baada ya mazingira.
Fahamu yafuatayo:

1. Aliimega ikabaki picha ya Magu peke yake wala hakuiweka picha yote kama unachokiandika wewe.

Ukizungumzia kicheko ni kuwa:
Kicheko kinabeba furaha au dharau (dhihaka). Kicheko cha furaha kinakuwa cha uchangamfu, chenye kuashiria jambo jema. Lakini vyote matokeo yake yanakuja baada ya mazingira. Mazingira yanayozalisha furaha yanafahamika! Mazingira yanayozalisha au yaliyojaa simanzi yanafahamika.

Mazingira yaliyo kwenye picha ya Magufuli si ya furaha, ni mazingira yaliyojaa simanzi. Kwamba huyu mtu kwenye kuvaa ni bado! Alichokivaa kinaonekana, na ndiyo mazingira hayo! Kwa hapo utacheka kwa furaha ipi wakati mazingira yameshaweka mlango wazi hali halisi ni ipi! Hata kihisiya inakupa kwamba hapa Magu kwenye mavazi ni bado! Ashakum si matusi! Tafsiri laini ni kwamba amevaa kishamba! Ameboronga kwenye mavazi.

Kiutu, kiubinadmu ukimcheka mtu kwa muonekano wake wa kishamba kwa mtu aliyeboronga kwenye mavazi si nidhamu nzuri, bali ni utovu wa nidhamu. Ukicheka kwenye mazingira ya namna hiyo ni kwamba umecheka kwa dhihaka! Umemkejeli kwa hali anayoonekana nayo! Kisheria sijui, kiutu ni utovu wa nidhamu.
 
Hiyo nayo mada. Watz tuache utani. Hata mie picha imenifurahisha. Sasa wewe mtu kaitwa polisi unateseka na kuanzisha UMBEYA. Nia yako kutaja neno Dikteta. JPM kahusikaje Hapo. Wanasema wapiga majungu Pua zinawasha na mdomo akiwa na Siri. Sasa wewe hata Siri yenyewe huna Unawashwa na Nini.


Sent using Jamii Forums mobile app

Umeandika nini?
 
Kuna yule dada alikua ana host kipindi cha Fema talk show au Haki Elimu(nimesahau) anaitwa Rebeka Mujuni kama sikosei ni mfano halisi wa hik ulichoshauri,dda kajiongeza na sasa hiv ana organization yake anafanya vyema sana
Wonderful!
Sasa huyu ninayomwengelea mimi, akiamua kufanya hivyo, yeye ndiyo atakuwa KUBWA LAO, hiyo shaka mimi sina kabisa, kwa sababu mpaka muda huu, amerusha kipindi chake nadhani haipungui miaka kumi. Sasa tuseme akiamua kuandika Proposal halafu akaambatanisha na hizo picha kama ushahidi, kwa kuanzia mimi naamini kabisa hata Serikali wenyewe tu lazima wampe support ya hali ya juu mno, both financially and morally. Sasa kitu kikishapata support ya Serikali, kupata financial support kutoka kwenye organisations za ndani na za nje ya Nchi ni kitu cha kugusa tu. Hapo bado watu binafsi wenye ukwasi na wengine ambao ni walala hoi kama sisi akina Makanyaga. Yaani huyu mama mimi naona kama amekalia jiwe la almasi akidhani ni tofali la udongo, huku akiomba watu wamsaidie.
Kitu kingine ambacho hakileti picha nzuri sana katika program yake, ni kwamba inamuonyesha kama yeye haguswi, na hivyo anafanya tu kwa sababu anajua wapo watakooguswa, na ni wengine nje ya yeye. Akianzisha organisation itaonyesha pia kuwa na yeye pia anaguswa na hali walizonazo wateja wake.

Tafadhali mimi naomba mama huyu aanze kufikiria namna ya kubadilisha mfumo wa program yake. Ni program ya maana mno watu hatuwezi kuvumilia kuendelea kuiona iko hivyo hivyo miaka nenda rudi, inafanya kwa mtindo wa zimamoto wakati ingeweza kufanya kwa namna ambayo ingetoa mchango mkubwa sana na wa hali ya juu mno na wenye kuleta impact kubwa sana kwa Taifa.

Hata hivyo mpaka muda huu, bado naendelea kumpongeza sana kwa idea yake hiyo
 
Haha kudhihaki ni kosa? Basi funga nchi nzima, ni kitu kila binadamu anafanya, tofauti moja ni online nyingine ni offline. I'm done dealing with you stupid people, block list yangu karibia ijae.
Yah Ni kosa Kama ulikuwa hujui, na Sheria ipo kumbuka kutokujua Sheria hakukufanyi kuvunja uvunje sheria
 
Haha kudhihaki ni kosa? Basi funga nchi nzima, ni kitu kila binadamu anafanya, tofauti moja ni online nyingine ni offline. I'm done dealing with you stupid people, block list yangu karibia ijae.
Watafungwa wavunja Sheria tu watanzania wote sio wavunja Sheria pili option ya ignore list ipo jf una haki ya kuitumia
 
Back
Top Bottom