Idrisa abadili mawazo. Hatojiuzulu tena

Idrisa abadili mawazo. Hatojiuzulu tena

  • Thread starter Thread starter MegaPyne
  • Start date Start date
Mgogoro mkubwa ni wizi wa umeme uliofanywa na Simba Cement Tanga!!! Kitendo cha Board ya wakurugenzi ya TANESCO kurudisha umeme kiwandani hapo kwa nguvu hakikuweza kuvumiliwa na Dk. Idriss. Hiyo ndio sababu ya kujiuzulu kwake. Suala la kupandisha bei ya kuunganisha na bei ya umeme wenyewe ilikuwa ni moja ya ajenda ya kikao cha menejiment na board na ukweli ni kuwa TANESCO bado ilikuwa ktk majadiliano na serikali. Taarifa zinaeleza kuwa serikali inaendelea kumuomba abadili msimamo wake huku yenyewe ikiwa tayari kusikiliza mapendekezo yake.

Kuhusu swala la kupandisha bei ya umeme, TANESCO waliipa serikali 2 options, Moja kupandisha hiyo bei ili wateja walipe wenyewe au serikali kuendelea kutoa ruzuku. Kwa serikali option ya pili ilikataliwa outright huku wakilazimisha TANESCO wasipandishe bei bila kujali mzigo wa uendeshaji ni mkubwa mno.

Unajua waTZ tumeathiriwa sana na mfumo wa kijamaa, twafikiri kila kitu chaweza kupatikana tu ilimradi serikali imesema. Mbaya zaidi tunasahau kuwa serikali yenyewe huwa inalazimika kutumia usanii ili kuwaridhisha wapiga kura bila kujali athari za usanii huo. Wabongo hatujifunzi na hatutaki kujifunza.

TANESCO ambayo inalipa karibu 40% ya mapato yake kwa IPTL na SONGAS kwa ajili ya Capacity charges tu, bado inatakiwa inunue umeme kutoka huko, ijenge na kukarabati miundo mbinu zake, ilipe wafanyakazi (Nasikia wako karibu 6000) etc etc.

Nyingi ya gharama wanazopata TANESCO leo ni matokeo ya maamuzi mabaya ya serikali. Serikali iache kucheza na akili za wananji, litafutwe TATIZO la kweli ili ufumbuzi wa kweli upatikane. Kwa kuilazimisha TANESCO ilipishe kidogo itafika mahala sio wateja wapya watashindwa kuunganishiwa umeme bali hata wale waliokwisha ungiwa (wateja)watakosa huduma. Hii ni sheria ya Uchumi na utawala si sheria ya Bokassa!!


Idriss kaonesha mfano tu kuwa kwa kiongozi mzalendo, pesa si kila kitu kwake. yasemekana mshahara wake ni zaidi ya 10m pale!! Pengine Karamagi, Balali na watu kama wao ni somo zuri kwao!!

Wakatabahu!!
 
Kada, Si kila asemalo mwanakijiji ni uongo simply bcoz he is a member of Chadema.

Kilichofanyika ni siasa kuchukua mkondo wake baada ya kuharibu.

Sasa bei itapanda, na Tanga cement watashikishwa adabu. Dr alikuwa anataka hayo tu.

MMempa mfupa uliomshinda FISI sasa anaanza KULILA mnamuingilia. Balozi inabidi apishe wengine tu AMECHOOOOKA!
Fikra zake zimefilisika
.

Good point FD, I like that.

Dr. Idriss has proved to be proffessional, right and ethical while the Board has proved to be political, wrong, unprofessional and they are after cheap popularity.

Kilichobakia ni kuwa Bodi ijiuzulu tu, haiko pale kwa manufaa ya TANESCO na ukweli bali siasa za uongo na kuliua shirka la TANESCO!
 
Alichofanya Dr Rashid ni sahihi kabisa, kapewa kazi ya kurejesha hadhi ya shirika kimapato na uendeshaji mambo haya yana gharama zake ( given the current situation ) na anapotekelza hayo whilst some few people playing politics then awaachie shirika lao waliendeshe kama tawi au maskani ya chama.
 

TANESCO ambayo inalipa karibu 40% ya mapato yake kwa IPTL na SONGAS kwa ajili ya Capacity charges tu.Nyingi ya gharama wanazopata TANESCO leo ni matokeo ya maamuzi mabaya ya serikali. Serikali iache kucheza na akili za wananji, litafutwe TATIZO la kweli ili ufumbuzi wa kweli upatikane. Kwa kuilazimisha TANESCO ilipishe kidogo itafika mahala sio wateja wapya watashindwa kuunganishiwa umeme bali hata wale waliokwisha ungiwa (wateja)watakosa huduma. Hii ni sheria ya Uchumi na utawala si sheria ya Bokassa!!


Big up Bokassa!Soma promise ya Mkapa baada ya kuwa amewaingiza watanzania kwenye Mkenge wa IPTL"The Government cannot allow Tanzania's electricity consumers and the economy to be burdened with extraordinarily high electricity tariffs." President Benjamin Mkapa, The Express, 28 May 1998
Dar es Salaam, 12 June 1998
" Kauli hizi za kisiasa ndizo zinazoendelea kuwanyonga walalahoi wa Tanzania. Serikali ya CCM wanapaswa kushughulikia root cause of the problem and not the effects.
 
Hivi Idrisa si alitakiwa awe kwenye retirement au nimepitiwa? Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa alipochaguliwa kuwa Gavana wa BOT alikuwa na miaka 45. Toka that time ni more than 15 years which makes him to be over 60. Au ndiyo kusema Presidential appointments kwenye public sectors hazijali umri?? Naomba kuuliza!!
 
Binafsi nalazimika ku question credibility ya Dr. Idris. Nimekuwa nikimu admire sana kwa uchapa kazi wake kama wengi humu lakini najua uamuzi wa ku resign hakuufanya kwa kukurupuka, alichukua muda wake hadi kuufikia. Its clear hapa ni kwa nini naanza kumuona hana MSIMAMO. Wengine mnasema ameombwa na mkuu wa kaya- if you are strong and you believe in your decisions hata akuombe nani- you stick to it, huu kwangu ni WOGA.Sina hakika na hili la mwisho kwa kuwa figure moja ya mshahara anaoupata iliyotajwa humu inatisha, labda alifikiria familia yake, akaangalia soko la ajira lilivyo sasa akairuhusu njaa yake iingie tena humu, so there might be some economic reasons as well.This is a joke, he has turned himself into a laughing stock na huyu JK kama ametia mkono wake hapa anapaswa kujifunza kuheshimu maamuzi ya watu.
 
nakuhakikishieni muda sio mrefu hii nchi mambo yatakwama kabisa.
ripoti iliyovuja sasa hivi inasema Dr Idris sio kuwa alikuwa akitaka bei ipande kama ilivyoelezwa na magazeti bali ongezeko la bei lilitakiwa kuziba mwanya wa madeni katika uendeshaji hii taa-nesco, sasa dr. akashinikiza hakuna kufukia madeni wote wadaiwa sugu walipe madeni ama la wakatiwe umeme joto hili likapuuzwa na wakubwa lakini amri ikatoka kwa MD kuwa kata! majibu yakaibukia tanga cement, karamagi akapigiwa simu akaamuru umeme urudishwe mara moja Dr.Idris akasema ikiwa kinyume anajiuzulu! akatekeleza hatimaye rais kaingilia kati lakini jibu sio Idris kurudi bali karamagi kuondoka sijui kwanini kikwete anamng'ang'ania karamagi!!!!!!
 
Kanakansungu,
Mshahara unaongea kwa Dr. Rashid? Akiwa Chief BoT, NBC, ACB anajua alilipwa ngapi? Let along huyo jamaa ana biashara nyingi na Vituo vya Mafuta kadhaa hapa jijini! Sio mtu wa njaa- ndo maana akaresign! Ni mtu wa msimamo!
 
Wakuu, sababu ya kujiuzulu kwa Dr Idris kuwa ni wizi wa umeme naodaiwa Kufanywa na Tanga Cement nadhani ni unproportional (kwa maana tunahisi tu, kuwa hiyo ni sababu.) Lakini what we are told by the cement manufacturer (in written explanation) ni kuwa fuse iliungua, na Tanesco wakaunganisha direct, na kwa hiyo umeme uliokuwa unatumika toka hapo haukuhesabiwa kwa siku 3. Tanga cement waliwahimiza Tanesco waweke fuse, lakini hawakufanya hivyo hadi baada ya siku 3.

Baadaye, Tanesco walikadiria kutokana na trend ya past bills, wakachukua estimates za juu kabisa, kuwa Tanga Cement walipe 49 million for the 3 days they used power without meter. Tanga wakagoma, wakiuliza kwa nini isichukuliwe average ya low , ambayo ingekuwa sh 33 million?

Kwa mujibu wa MD wa Tanga, wakiwa kwenye correspondent hizi, kwa miezi 2 hadi 3, ghafla Tanesco wakaamua kukata umeme.

Tanga wanasema wanalipa bills on time, amounting to between 450-500 million kila mwezi. Kwa hiyo, Tanesco waliamua kumkatia mteja anayelipa 500 million kwa kuwa hawakuwa wakielewana juu ya ulipaji wa sh.49 million. Kwa hili, hakuna aliyekuwa tayari kutoa maelezo ndani ya Tanesco...nilipowauliza, wakasema umeme umerudishwa.

Kama kweli Dr Idris alikuwa anaona Tanga Cement ni tatizo, inawezekana kuna sababu nyingine...lakini hii naona kama hai hold water, kuzingatia si tu his integrity, lakini pia hata common economic principles. Tunalionaje hili jamani?
 
Kanakansungu,
Mshahara unaongea kwa Dr. Rashid? Akiwa Chief BoT, NBC, ACB anajua alilipwa ngapi? Let along huyo jamaa ana biashara nyingi na Vituo vya Mafuta kadhaa hapa jijini! Sio mtu wa njaa- ndo maana akaresign! Ni mtu wa msimamo!

Mzalendo, nimesema hapo kuwa sina hakika na suala la njaa lakini huwezi jua labda JK kampandishia dau kumrudisha, do you think it was easy for him to change his mind, inawezekana fedha imemwaga, ni possibility lakini tu, and thats what i mean by saying- NJAA!Hata Karamagi(japokuwa ni millionaire) akisign Buzwagi kwa 10% tunaita njaa watoto wa mjini.
 
Sio fuse iliungua, simba cement walikata seal iliyopelekea kutemper na meter iliyosababisha hiyo hali!

Hii waliifanya kwa kutumia mmoja wa waliowahi kufanya kazi wa Net solution! hiyo ndio inner story.

Magazeti yanaweza kuripoti yatakavyo!
 
WANA JF NAOMBA KUWAKUMBUSHA

TANESCO operational problems : Easier said than done?

2004-06-20 07:36:35
By Nimi Mweta
Experts studying the power sector in Tanzania, contributing to the second open forum on the power sector in September last year, had some pertinent observations on managerial problems at the utility, TANESCO.

They identified a number of problems that were basically related to government policy, and a series of others that were within the control of the utility. It is the latter that a new management set to solve.

According to Prof. Burton Mwamila, F. W. Mtalo and A.H.J. Nzali, problems related to government policies included rural electrification at TANESCO’s expense, an eight per cent interest rate on foreign loans to the sector, and failure to pay electricity bills by several key institutions.

Those within the control of TANESCO include high dependence on foreign finance for development projects, specialised and technical expertise.

Others were the existence of high production costs as a result of inadequate human, financial and material resources, management (in the sense of insufficient capacity), poor system of billing and collection of funds, along with rampant corruption which resulted in operational losses and cash flow difficulties.

Still others were inefficiency and unnecessary red tape or bureaucracy in services delivery, also occasioning revenue losses. The latter was needless to add a major condition for corruption, random charges to clients.

Tied to these difficulties was over employment within TANESCO resulting in unnecessarily high costs of operations, while there was noticeably low productivity due to inadequate training in relevant fields.

It was also observed that uncertainty on the future of TANESCO after being privatised contributed to productivity woes. The researchers were thus of the view that Power Sector Master Plan projections were too optimistic.

An initial study and open forum to discuss it, noted as the first open forum on the power sector, organised by the Tanzania Confederation of Industries (CTI) like the second, came up with recommendations. The follow up study says it gave 14 recommendations the implementation of which could bring about significant improvement of power supply. It would also definitely foster enhanced competitiveness of local industries.

What a rapid view of policy decisions taken in the past two years might indicate, is both a pursuit of those recommendations and further complication of the situation they set to address.

For instance there was a tariff rise on two occasions, first before the new contracted management team took over, and last, at the moment that it was completing two years (of contract). Domestic rates tended to rise, not industrial tariffs.

The second open forum laid considerable accent on problems caused by power supply disruptions and constraints (cost, competition) arising therefrom.

While neither the utility’s management nor the ministry can fail to take note of these concerns, it is difficult to see how they can be addressed, except as part of a wider rationalisation of the power supply as a whole. It merges with TANESCO’s problems, not a distinct issue.

When attention is given to their other concerns, namely not just how to guarantee availability of power supply but also enhancing its quality and reducing the tariff to between four and six US cents, the cap is blown.

All what policy action has been able to achieve is to narrow the gap between domestic use rates and industrial tariffs (first tariff change), and slight reduction of the industrial tariff. But tariffs are still quite high.

The paper raises issues of determining principles governing power tariff setting and establishing how they have been adapted to (suit) various (known) situations. Exploring such a question further would involve the sort of discussion which researchers may prefer to avoid, namely the nature of ownership of the utility and how it influences costing. Prices relate to costs, so only firms with capital, reserve equipment, can cut costs.

By definition therefore, TANESCO will by any definition or scenario become a high cost, and thus high tariff company, and without including any avoidable managerial problems as the first study noted. It has many new projects either coming up recently or whose loans were still being paid, it has a multiplicity of suppliers and expertise for projects, all of which are costly. Reducing tariffs needs connection to cheaper generation.

The paper recommended identifying and comparing power financing between Tanzania and other countries in the region, the tariff setting mechanism adopted here and outside. While one doesn’t seek to upstage the research, little that is unknown can be uncovered here, for instance that Uganda is low tariff as its power supply from the Owen Falls dam has been stable, etc. Adding the IPTL facility to the costs worsens tariffs.

Many of the 14 recommendations had already been met or implemented, like getting alternative sources of power (with Kihansi completed, Songas flow expected), review of TANESCO’s debts (settling outstanding bills), etc. An idea about separating power generation from power supply is contained in recommendations, much in keeping with some current (in the late 1990s) ideas about the issue. Perhaps many might be wiser.

One supposition about the merits of separating generation from supply is that competition is created at both instances, by having several generators (but some experts recommend retaining unitary generation) and suppliers.

For a certain reason there is competition expected, whereas the focal point is negative creation of price setters and takers, as well as monopoly supply (inability to switch from one supply to another).

Thus a crisis emerges out of suppliers being price takers, and these in turn readjusting prices to consumers, at will.

Managerial changes required in the paper have been effected, like putting in place a private management and an interim board before full privatisation of TANESCO.

It however seems that the government is in no real hurry to proceed with actual lease (as no prospect exists of sale of utility), since its leverage would be further reduced with a lease. Yet only full privatisation (virtual sale of assets) could actually change things.

It is, for instance, easy to pour venom on corruption and suggest, inter alia, a reduction of TANESCO’s excess workforce (which often is done by productivity enhancing systems rather than manual depression of size of employees).

Weeding out corrupt employees is in a sense a mistaken recommendation, for rational people know that each person is potentially corrupt. The issue is to put up mechanisms where discretion is minimal.

While reforming or restructuring government departments and parastatals has on certain occasions moved to weed out a number of employees upon whom buzzing stories of bribes existed, this is limited in its scope and effectiveness.

When demand cannot be made without discretion being applied, corruption creeps back. Replacing corrupt people then becomes a matter of generations, replacing layers of corrupt people regularly.

If any achievements have been registered in this direction they may have to do with LUKU as a predictable payment mechanism, or managerial intent (by replacing quitters insensitive to erosion of ethics).

Subsidy of domestic consumers by industry has largely ended, to the groaning of wage earners and alarm at environmental impact likely. A greater reliance on charcoal is likely in many urban homes, reducing electricity consumption.

No doubt exists either that the government will support other power generation projects like Songas (now almost completed), Mchuchuma (a polemic which MPs surfaced), or Rufiji hydropower plant. Greater power flow is likely in the (near) future as Songas is fully exploited, and IPTL thermal facility is converted to gas use or firing. Costs won’t be cut down, for no private investor is pursuing investment to realise a profit later.
• SOURCE: SUNDAY OBSERVER
 
Kwa kweli hata sielewi kwa nini Dr. anaamua kutengua uamuzi wake. Lakini labda niulize huyu jamaa amewahi kushika madaraka makubwa sana kwenye nchi hii... Gavana wa BOT halafu baadaye kuajiriwa kwenye normal Bank kwangu mimi ni demotion... alitakiwa afungue firm yake awe anaisimamia sio kuajiriwa.. Amekuwa MD wa Vodacom hakuweza kufanya cha maana ilikuwa tuu ni juhudi za R.A kuonyesha kuwa na sisi wabongo tunaweza. ila aliprove failure mapema mno.. kwa sasa Meneja mkubwa Tanesco hakuna cha maana kinachofanyika huko.. aliwahi kusema kuwaondoa vishoka sio rahisi (Failure)
Sijui ni kwa nini hatuna PHD holder tanzania ambao wanaweza kusimama na kusema hiki hapana hiki ndio... Ndio maana kuna wau wengine wanasema hakuna haja ya kusoma hadi kwenye level ya Phd kwani sioni wanachokifanya kwenye taif hili... wamekuwa wanasiasa zaidi.
Lini wasomi wetu wata- add value kwa nchi hii??? na sio kwenye mambo yao binafsi
?

Nadhani si sahihi kuanza kuzungumzia mambo ya Ph.D hapa.Ilivyo ni kwamba mtu mwenye hiyo digrii amebobea kwenye fani yake, na hawa watu sehemu zao za kazi ni academic or research institutions.Hawa wote wanaofanya kazi nje ya hizo taasisi ni kwamba wamecross over. Nadhani ingekuwa vema wanapokuwa nje ya academic/research instutitions kama kwenye politics au administration waache kutumia hizo title kwa sababu ni irrelevant.Ndiyo maana hata Condo Rice ni Professor lakini hatumii hiyo title huko white house.Ila akimaliza ngwe ya politics na kurudia uhadhiri kule Stanford University anaweza kuendelea na title ya Professor kama inakubalika.Kuna baadhi ya nchi (mfano Germany), kama wewe ni Prof halafu ukawa nje ya taaluma au utafiti kwa muda fulani ni kwamba hiyo title inafutika automatically. Nadhani Tanzania pia inabidi tubadilike sasa, kwamba wanataaluma wapoacha specialities zao na kuingia kwenye siasa au utawala inabidi pia wasitishe kutumia hizo title (Dr/Prof).
 
FD,

Inawezekana ni kweli walitemper na mita. Sikusoma magazeti, ila nimeona statement ya Tanga Cement mahali. lakini je, unafikiaje kumkatia umeme mteja ambaye hukulipa Sh mil 500 kila mwezi, na hajalimbikiza bill hata mwezi mmoja?

TCC wanaonekana wana confidance kuwa Tanesco wame breach contract inayowataka watoe advance notice ya 48 hrs before they disconnect power, na wanasema wanajadili ili kuchukua hatua za kisheria.

Na inaonekana si kweli kwamba Karamagi aliagiza umeme urudishwe na ukarudishwa kweli mara moja. Kulikuwa na ukaidi fulani uliofanywa umeme uchelewe kurejeshwa, bado haijawa clear.

What do you comment on that, Mzee wa pande zote?
 
This article does not reveal why Idris was ealier decided to quit.
 
Jafar,

i said so because there is a wide belief that Tanga cement power disconnection saga is one of the reasons which led to his resignation. I doubt this, due to the reasons which i have explained in my earlier postings. PLz read the other before that one. It seems to be an argument that may fail to hold water in the face of the MD's resignation reasons.
 
Hii issue kwa ujumla imeniliwaza sana moyo wangu.nilikuwa nadhani waTZ wote wamekuwa watu wa kukubali yaishe, kumbe kuna bado, people can stand on their guns (sitishiwi nyau).I can call this "a storm in a bucket".Itawaamsha na MD wengine wa mashirika ya umma, watekeleze wajibu zao inavyotakiwa.I appreciate the move of Rashid.Bravo Rashid.It is "healthy" move, I'm sure our people will realise sooner or later.Hii sijui kuungua fuse tanesco wakaunganisha direct ni spinning tu!Naamini Rashid ni mtu mwenye akili timamu na hakukurupuka kuwaadhibu.
 
Nilikuwa nimekusudia kukaa nje ya huu mjadala lakini naona pengine kuna umuhimu na mimi nikichangia.
1.Mimi bado uamuzi wa kupandisha tariff na bei ya kuunganisha umeme kama njia ya kuongeza mapato. Hivi hawa wachumi wetu wanadhani ukimuongezea mteja bei ya kuunganisha umeme kwa zaidi ya shilingi laki 3 ataendelea kufanya hivyo? Ninavyojua, wengi tu watabadilisha mawazo na kuamua kurudi kwenye vibatari na kuni. Watangalia televisheni na kupiga pasi kwa jirani au kutumia pasi ya mkaa. Hawa utakuwa umewapoteza katika wateja wako wa muda mrefu. Wengine wataazima umeme kutoka ama kwa jirani au kwa kutumia wafanyakazi waliowahi kufanya kazi Tanesco( na sito shangaa kama hata wengine walio bado wameajiriwa) kuwaunganishia kiujanja unjanja na hivyo kuwakosesha Tanesco mapato. Ushauri wangu kwa hili ni Tanesco wangepunguza au hata kuondoa gharama za uunganishaji umeme kwa sehemu ya jamii na hivyo kupanua wigo la wateja watakaoukuwa wanatumia umeme na hivyo kulipia kila mwezi au vinginevyo. Makampuni mengi ya simu za mkono huko kwa wenzetu wanatoa simu bure au kwa malipo nafuu wakijua watafaidika kwenye matumizi yako. Mfano mwingine ni mashine za kunyolea ambapo faida ni kwenye nyembe na sio mashine yenyewe.
2. Kuongeza tariff kwa kiasi kikubwa kutamfanya mteja ama apunguze matumizi( kupikia maharage kwenye jiko la mchina), kutafuta njia mbadala(solar etc) au kujitoa katika mfumo wa Tanesco. Yote haya yatachangia kupunguka kwa mapato badala ya kuongezeka.
3. Tanesco hawajawahi kuwa makini katika upande wa kupunguza gharama za uendeshaji. Ni lazima waongeze productivity.Wanaweza, kwa makubaliano na wafanyakazi, kupunguza mishahara na marupurupu mengine( mfano marubani wa nadhani continental airline (?) walipokuwa wanaangalia bankruptcy usoni walikubali kupunguzwa mishahara na kufanya kazi kwa ziada),kupunguza wafanyakazi ( mheshimiwa alipoingia aliahidi kuongeza wafanyakazi wa sehemu ya wateja kama nakumbuka sawasawa, kutumia mashine zilizo more efficient, kuangalia fuel mbadala ya generator zake n.k. Kumnyang'anya gari mweneykiti wa bodi ni symbolic, makato yanatakiwa yaende deeper kama wako serious.
4. Suala la hawa mabwana kukata seal bado linanisumbua. Najua Tanesco walikuwa na kawaida ya kudai malipo kwa kukisia badala ya kusoma mita. wakati mwingine haya makisio hayakuwa realistic na mteja hakuwa na recourse ya kujitetea.
5. Tuache siasa kwa kuangalia mantiki badala ya kumshambulia mtu ati kwa sababu ni kaburu au kumtetea kwa sababu ni mzalendo. Bottom line ni manufaa ya taifa na si kingine.Tumevunja mikataba kwa kuzingatia uzalendo au kufanya maaamuzi ( kituo cha mafuta Mwanza, City water n.k.)bila kuangalia athari ya ke na sasa yanatutokea puani!
6. Tuache tabia ya kufikiria kila alie na Ph.D anaweza kuongoza. Apimwe mtu na management skills zake na uwezo wa kuleta mafanikio katika kile anachokiendesha. Hii ni pamoja na kuweza kunegotiate na stakeholders wake.
7. Hivi kwa nini kama mheshimiwa Dr. aliona suala la ofisi na gari kwa mwenyekiti ni hasara hakulipeleka kwenye bodi akijumuisha mapendekezo mengine ya kubana matumizi. Manager mzuri si Don Quixote. Ana strategise mapambano yake yote.
8. Ina bidi tuanze kuheshimu wateja kwa dhati. serikali ilikuwa ikiwa na shida inapandisha kodi kupita kiasi halafu wanashangaa wateja wakiamua kuwahonga watafuta kodi! Mashirika kama NHC na TTCL yaklikuwa nayo yanamtindo huo huo. Sikatai kuwa kuna wakati bei inahitaji kupanda lakini kwa kuzingatia uwezo wa mteja kulipa. Ni nchi chache zenya single digit infalation zina kawaida kama ya kwetu ya kupandisha bei mara dufu hata mara tatu kwa mpigo. Kwa wenzetu hata ongezeko la asilimia 10 linazua mjadala! Inabidi tubadilike jamani.
 
Wakuu, sababu ya kujiuzulu kwa Dr Idris kuwa ni wizi wa umeme naodaiwa Kufanywa na Tanga Cement nadhani ni unproportional (kwa maana tunahisi tu, kuwa hiyo ni sababu.) Lakini what we are told by the cement manufacturer (in written explanation) ni kuwa fuse iliungua, na Tanesco wakaunganisha direct, na kwa hiyo umeme uliokuwa unatumika toka hapo haukuhesabiwa kwa siku 3. Tanga cement waliwahimiza Tanesco waweke fuse, lakini hawakufanya hivyo hadi baada ya siku 3.

Baadaye, Tanesco walikadiria kutokana na trend ya past bills, wakachukua estimates za juu kabisa, kuwa Tanga Cement walipe 49 million for the 3 days they used power without meter. Tanga wakagoma, wakiuliza kwa nini isichukuliwe average ya low , ambayo ingekuwa sh 33 million?

Kwa mujibu wa MD wa Tanga, wakiwa kwenye correspondent hizi, kwa miezi 2 hadi 3, ghafla Tanesco wakaamua kukata umeme.

Tanga wanasema wanalipa bills on time, amounting to between 450-500 million kila mwezi. Kwa hiyo, Tanesco waliamua kumkatia mteja anayelipa 500 million kwa kuwa hawakuwa wakielewana juu ya ulipaji wa sh.49 million. Kwa hili, hakuna aliyekuwa tayari kutoa maelezo ndani ya Tanesco...nilipowauliza, wakasema umeme umerudishwa.

Kama kweli Dr Idris alikuwa anaona Tanga Cement ni tatizo, inawezekana kuna sababu nyingine...lakini hii naona kama hai hold water, kuzingatia si tu his integrity, lakini pia hata common economic principles. Tunalionaje hili jamani?

Ndiyo hiki ninachokizungumzia kila wakati. Mantik hapa iko wapi? Kuna hasara gani kuendelea na majadliano wakati unavuta hizo milioni 500. Matatizo yetu tunaweka uzalendo mbele ambao hautatufikisha kokote. Sasa wakiacha production anaumia nani? Si sisi wenyewe na trust me gharama yote hiyo watamrudishia mteja hapo umeme utakaporudishwa!
 
Back
Top Bottom