If God knows the future (omniscient), can you change your destiny?

If God knows the future (omniscient), can you change your destiny?

Unapozungumza habari ya Mungu,mzungumze kama Mungu.Unapozungumza habari ya binadamu,kumbuka kutofautisha namna yake tofauti na Mungu.Mungu anajua kila kitu,he is timeless,he see things timelessly,he is not bound by age,because age is one of his creations.lakini wewe na mimi tuko within a certain time limit,tuna age.Yeye huona mwanzo wetu hadi mwisho,ndio maana keshaujua na kuunakili,kwa vile hawezi kuubadili,he cant change our future,because it is already written,by us,He is not the writer,we are.He is just waiting for everybody to finnish writing his/her future,out of our free will,actually he is waiting for us to complete our age,of which he already know how it ends.

Kuna baadhi ya watu humu wanapaswa kuisoma kwa kuirudiarudia hii post hapo juu hadi wapate ujumbe.kuna mambo yameshapewa good explanations lakini still mtu anabisha tuu.What i see ni kwamba muktadha wa mabishano yetu hapa si kuelimishana,bali ni kutetea tunachoamini no matter what weighing facts others are giving to challenge us.
 
Halafu hadi hapo hujaona kuwa na wewe umeshindwa ku prove kuwa hayupo ...!!

Hakuna chochote ambacho hakipo ambacho yeyote anaweza ku prove jwamba hakipo.

Kwa sababu hakipo ili kiwe proved kwamba hakipo.

Nikisema kuna mchaga mwenye vichwa vitatau yuko.juu ya mlima Kilimanjaro na huyu ndiye ana conyrol dunia nzima, obviously that is hogwash. Lakini by the nature of proofs, you cannot prove kwamba hayupo. Nitakuchenga tu na kujuambia haonekani kwa macho, and this and that. Therefore you cannot prove kwamba hayupo.

Same thing with god. No one can.prove he doesn't exist, regardless of whether he exist or not.

Proof ni kwa vile vilivyopo.

Na wewe unayesema yupo ndiye mwenye burden of proof.

Ambayo so far hujatoa.
 
Hakuna chochote ambacho hakipo ambacho yeyote anaweza ku prove jwamba hakipo.

Kwa sababu hakipo ili kiwe proved kwamba hakipo.

Nikisema kuna mchaga mwenye vichwa vitatau yuko.juu ya mlima Kilimanjaro na huyu ndiye ana conyrol dunia nzima, obviously that is hogwash. Lakini by the nature of proofs, you cannot prove kwamba hayupo. Nitakuchenga tu na kujuambia haonekani kwa macho, and this and that. Therefore you cannot prove kwamba hayupo.

Same thing with god. No one can.prove he doesn't exist, regardless of whether he exist or not.

Proof ni kwa vile vilivyopo.

Na wewe unayesema yupo ndiye mwenye burden of proof.

Ambayo so far hujatoa.

Kuna wakati watu wanaweza kuamua kuzamisha vichwa vyao kwenye lindi la ujinga

Sijui unashindwaje kuona kwa urahisi kabisa kuwa unaposema "hakuna" unatakiwa utoe ushahidi kwa ku back up madai yako na kama huna utakuwa unaamini tu kuwa hayupo

Ni nini kimekufanya ukasema hayupo?

1;Je ni kitendo cha wewe kushindwa kuelewa yale unayoambiwa yanayomhusu?
2;Je ni kukosa ushahidi wa uwepo wake?

Kama kuna kati ya kimoja hapo kinachokufanya useme hayupo basi;
1;Utakuwa ni mvivu wa kufikiri
2;Utakuwa umeamua tu kuamini hayupo!
 
Kuna wakati watu wanaweza kuamua kuzamisha vichwa vyao kwenye lindi la ujinga

Sijui unashindwaje kuona kwa urahisi kabisa kuwa unaposema "hakuna" unatakiwa utoe ushahidi kwa ku back up madai yako na kama huna utakuwa unaamini tu kuwa hayupo

Ni nini kimekufanya ukasema hayupo?

1;Je ni kitendo cha wewe kushindwa kuelewa yale unayoambiwa yanayomhusu?
2;Je ni kukosa ushahidi wa uwepo wake?

Kama kuna kati ya kimoja hapo kinachokufanya useme hayupo basi;
1;Utakuwa ni mvivu wa kufikiri
2;Utakuwa umeamua tu kuamini hayupo!

Prove kwamba mungu yupo.
 
Kwamba so far huwezi ku prove kwamba mungu yupo.

Flip flopper you can't prove a thing than blahing blahing. Eti tunatambua ukweli na hadith........., my foot.
quote_icon.png
By Kiranga

Kwa.sababu tunahambua ukweli na hadithi zisizo na ukweli.

Kwa sababu wewe ndiye uliyejibuzana nami hapa kama mtetezi wa uwepo wa mungu.

You can't even support your malarkey
 
UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO
Biblia ni kitabu cha ajabu kuliko vyote. Maelezo yake kuhusu chanzo cha uovu; taarifa yake isiyo na kasoro kuhusu mahusiano ya Mungu na taifa la Israel;

ujumbe wake unaopenya kupitia kwa manabii wao; 'habari njema' yake iliyohubiriwa na Yesu Kristo na mitume wake; na juu ya yote uchambuzi wake sahihi uhusuo mapungufu ya silka ya mwanadamu ukilinganishwa na utakatifu, kweli na rehema ya Mungu, iliyodhihirishwa zaidi hasa katika Mwanawe - haya yote ni mambo ya kipekee yasiopatikana katika kitabu kingine chochote
duniani. Haya yalimfanya Henry Rogers, miaka 100 iliyopita kusema: "Biblia sio namna ya kitabu ambacho mwanadamu angekuwa ameandika kama angeweza, au angeweza kuandika angeweza". Kwa maneno mengine, Mungu anahitajika katika kuelezea uwepo wake.


Katika kazi hii fupi tutaangalia mojawapo ya mambo yake ya ajabu:
unabii wake. Kihalisi, unabii sio kuelezea tu mambo ya mbeleni. Nabii alikuwa ni mtu 'aliyesema kwa niaba' ya mwingine, msemaji; na unabii ulikuwa ni ujembe alioutoa nabii kwa niaba ya Mungu. Lakini kwa kuwa unabii wa Biblia unao pia 'utabiri' mwingi wa mambo yajayo, kwa lengo hili tu tutazingatia maana hiyo hapa.


NANI MWENYE MAMLAKA YA UNABII?
Lakini kwanza inabidi tukubaliane juu ya swali moja la muhimu: Biblia inadai kwamba mamlaka ya unabii inatoka kwa Mungu tu na ni uthibitisho wa uweza wake?


Kwa hili lipo jibu muafaka katika unabii wa Isaya. Katika kifungu cha 41 Mungu anazitaka sanamu na wanaoziabudu wa nyakati zile kuthibitisha kama wanazo nguvu za kiungu. Hivi ndivyo anavyoziambia:

"Haya leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema Mfalme wa Yakobo. Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuonyeshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yatakayotokea baadaye." (Ms. 21 - 22)


Msingi wa changamoto hii ni dhahiri: Wanaoabudu kipagani wanadai kuwa sanamu zao ni Miungu. Sawa; wathibitishe basi! Na uthibitisho unaotakiwa na Mungu mwenyewe ni kwamba sanamu zitabiri mambo yajayo na pia kutangaza 'yaliyopita', yaani kueleza jinsi uumbaji ulivyokuwa hapo mwanzo. Katika msitari unaofuata dhana hii iko wazi sana.
"Tujulisheni yatakayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu...." (Ms. 23)

Hapa Mungu mwenyewe anatujulisha kwamba kuweza kutabiri mambo yajayo ingekuwa uthibitisho wa uweza wa kiungu. Kwa zaidi ya mara moja katika sehemu hii ya unabii wa Isaya, Mungu anatangaza ya kwamba Ni yeye pekee aliye na uwezo huo; kwa kuwa Ni yeye pekee aliye Mungu, hakuna mwingine.

"Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine, mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi......" (46:9)

Mungu wa Israeli hapa anatangaza kwamba hakuna kitu kinachostahili kuabudiwa ila yeye; na anaendelea kusemea ishara za nguvu zake kwa maneo haya.

"...nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote." (46:10)


Lifikirie, nani awezaye kusema, "Mapenzi yangu yatasimama..." zaidi ya Mungu? Ni nani katika dunia nzima awezaye kusema kitu kama hicho? Kusemea hili inahitaji mwenye uwezo wa kujua mambo yajayo kabla hayajatokea, lakini awezaye kuhakikisha yanaenda alivyopanga. Kwa maneno mengine, kutoa unabii utakaotimia kwa vyovyote, unamhitaji Mungu. Hakuna namna nyingine ya kuelezea.


Agano jipya linadai hivyo hivyo. Wakati Yesu alipokuwa anakaribia kuwaacha wanafunzi wake, aliwaahidia msaada wa Roho Mtakatifu katika jukumu lao la kuihubiri injili duniani. Mojawapo ya matokeo ya karama hiyo ingekuwa, "na mambo yajayo atawapasha habari yake." (Yoh. 16:13); kwa maneno mengine wafuasi wangepewa ufahamu wa mambo yajayo. Kwa vyovyote inamaanisha wasingepewa karama hiyo ya kipekee wasingeweza kuyajua. Uweza wao kutambua yajayo ndio ungekuwa ushahidi wa nguvu ya kiungu waliyotunukiwa.

Tena, katika kitabu cha mwisho cha Biblia, kifungu 1, msitari 1, inaelezwa kwamba Mungu alimpa Yesu Kristo Ufunuo, "awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi..." (Uf. 1:1). Ufahamu wa mambo yajayo ulitoka kwa Mungu, kupitia kwa Kristo; bila ufunuo huo watumishi wake wasingelijua lolote linalouhusu.

Hitimisho ni wazi: Biblia inasema kiuhakika ya kwamba uweza wa kutabiri yajayo ni wa Mungu pekee.

BIBLIA INATABIRI YAJAYO?
Tunaweza tu kuchunguza historia na uzoefu wetu kutambua kwamba wanadamu kwa jinsi walivyo, hawawezi kujua hata kidogo ya mbeleni. Kwa nini?

Hatuwezi hata kujua litakalotupata usiku wa leo, au kesho tukienda kazini, achilia mbali mwaka kesho; au litakaloipata dunia katika miaka 100, hata tusiposemea miaka 2000! Watu wangekuwa na utambuzi kidogo tu wa mambo yajayo, maamuzi mengi yangebadilika kiasi gani! Ajali nyingi kiasi gani zingeepukwa! Maafa mengi kiasi gani yasingeliachiwa yatokee. Vita vingi kiasi
gani visingeanzishwa! Uzoefu katika maisha yetu wenyewe, na wa historia ya mwanadamu unatuonyesha kuwa mwanadamu hana ufahamu wowote wa hakika wa litakalotokea.

Lakini chukulia kwamba mambo yajayo yameelezewa, sio mara moja, bali mara nyingi. Na kwa nyakati zote katika kitabu hicho hicho, Biblia na sio katika kingine chochote duniani! Halipaswi hilo kutufanya tukae chini na kuzingatia? Ndio maana tunasema kwamba unabii wa Biblia ni wa maana sana, na unapaswa kuchunguzwa kwa makini, kwa kuwa mambo mengi mno
yanautegemea. Ni kiashiria ya kwamba upo katika dunia uweza mkuu na nguvu impitayo mwanadamu.


"NDIO, LAKINI..."
Wale wasioamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu, hawapendi kabisa unabii wake. Unapokubali imetabiri kisahihi mambo kabla ya kutokea utakuwa umeanza kukubali uwepo wa Mungu... Kwa hiyo wanajaribu kuielezea mbali. "Unabii," wanasema, "haukuwa hasa utabiri wa mambo. Uliandikwa baada ya matukio 'unayoyabashiri.'Sasa hii hoja inaweza kuwa na nguvu kama unaweza kuthibitisha kuwa yale yaliyoandikwa katika Biblia, na hasa yale ya Agano la Kale kwamba yaliandikwa baada ya matukio yanayodaiwa kutokea. Lazima tuseme hapa wazi kwamba hawana uthibitisho wa moja kwa moja juu ya hili; hitimisho lao ni matokeo tu ya kutafsiri mambo kujiridhisha wapendavyo. Ukweli ni kwamba, utafiti wote uliofanywa katika miaka 100 iliyopita unaonyesha kwamba yaliyoandikwa katika Biblia ni halisi; ni ya nyakati zinazodaiwa kuandikwa.

Lakini kuna njia ya mkato katika jambo hili inayoweza kutusaidia katika lengo letu. Hakuna anayeweza kubisha kudai kwamba maandiko ya Agano la Kale hayakuwepo miaka 200 kabla ya kuzaliwa Kristo, kwa kuwa yalitafsiriwa katika Kiyunani wakati huo, na huwezi kutafsiri kitu kisichokuwepo!


Ubishi mwingine ni kusema, "Ndio, unabii huu wa Biblia ni utabiri wa kijanja wa kisiasa wa watu waliokuwa wakichunguza matukio enzi zao na kuona mwelekeo wa matokeo yake."

Utabiri wa kijanja kisiasa! Uliotolewa karne nyingi kabla ya Kristo na unaoendelea kuwa kweli miaka 2000 hadi leo! Hao manabii walikuwa wachawi wa namna gani kuweza kufanikisha hilo bao? Kusema hivyo ni kuonyesha tu yasivyowezekana maelezo yake. Lakini jibu la hakika kwa ubishi huu kama ilivyo kwa ubishi mwingine wowote, ni kusoma sehemu ya unabii wenyewe. Kwa hiyo tunaanza na:-


UNABII KUHUSU BABELI
Katika enzi ya manabii wa Israeli (Kama 850-560 K.K) kuliinukia dola mbili kuu katika maeneo yanayoizunguka mito ya Frati na Tigrisi, katika Iraki ya sasa.

Ya kwanza ilikuwa dola ya Ashuru iliyokuwa na makao makuu Ninawi. Kwa karne mbili, Waashuru walivamia ardhi ya mataifa waliowazunguka: kusini wakawatawala Wakaldayo na makao makuu yake Babeli; Magharibi wakaikalia Shamu, na kuendelea chini katika pwani ya Bahari ya Kati, kupitia Israeli mpaka Misri. Sera yao ilikuwa ya kigaidi. Lengo lao lilikuwa kuwatisha
wakazi wa maeneo hayo watii na kulipa kodi kwa mwaka. Kufanikisha hili waliiswaga miji kiuporaji na kuichoma moto, wakavibamiza vijiji, na kuua wakazi na kuchukua maelfu ya mateka Ashuru.

Katika nusu ya pili ya karne ya saba (K.K), nguvu ya Ashuru ilipungua na Babeli ikaanza kupanda. Katika mwaka 612 (K.K), Ninawi uliangushwa. Nebukadreza, mfalme wa Wakaldayo, haraka akaanzisha dola mpya. Mataifa madogo madogo Mashariki ya Kati yalipokuwa yanashangilia uhuru wao kutoka Ashuru, mara yakajikuta wakivamiwa na majeshi ya Babeli. Na hasa
Nebukadreza akaivamia Israeli akaiteka Yerusalemu, akalichoma hekalu lake na kuchukua maelfu ya mateka Babeli. Akaendelea kusini zaidi na kuivamia Misri. Dola ya Babeli ilikuwa ni awamu ya pili ya utawala huu wa kijeshi. Ulikuwa katika
eneo la Frati.Na hasa Nebukadreza, mfalme wake mkuu kabisa aliujenga mji mkuu wa Babeli kuwa fahari ya dunia katika Mashariki ya Karibu. Alijenga Mahekalu makubwa na majumba ya kifalme, na kuzungushia jiji hilo ukuta mkubwa sana
kuulinda. Babeli ukawa utukufu na fahari kuu kwa Nebukadreza mwenyewe na Wakaldayo wake.
Ni vigumu kwetu sisi kwa sasa kutambua athari za utawala kama huo wa kimabavu na uharibifu wa mali kwa wakazi wa mataifa madogo. Kwao dola za Ashuru na Babeli zitakuwa zilionekana tishio na zisizoshindwa.


MAANGUKO KAMILI
La ajabu, miaka 100 kabla Babeli haijafikia kilele cha ukuu wake, nabii Isaya alishatabiria kuangushwa kwake kwa maneno thabiti sana. Katika kifungu kilichopewa kichwa cha habari 'Mzigo wa Babeli' ni hivi alivyosema."...Siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu...Tazama, nitawaamsha Wamedi juu yao...Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa... Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko. Lakini huko watalala
hayawani wakali wa nyikani "(Isaya 13:6,17,19-21)Hatima ya Babeli inaeleweka: wavamizi watakuwa Wamedi (taifa mashariki ya
Babeli); jiji litakuwa maganjo, lisilokaliwa na mtu wala mnyama pori. Tukumbuke utabiri huu ulitolewa miaka 100 kabla ya Babeli kukua kufikia nguvu na utukufu wake.

Nabii mwingine, Yeremia, akiandika miaka 100 baadaye, wakati Nebukadreza alipokuwa akikaribia kuivamia Yerusalemu, aliongeza mtazamo juu ya anguko la Babeli.

"BWANA asema hivi, Angalia, nitaamsha juu ya Babeli upepo uharibuo... Babeli umeanguka na kuangamia ghafla... Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi... Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwa-mwitu, ajabu, na mazomeo pasipo mtu kukaa huko... kuta pana za Babeli zitabomelewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa... Ee BWANA, umenena habari za mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele..."
Na mwishowe nabii anaamriwa kufunga jiwe kwenye gombo la unabii ule na kulitupia ndani ya mto Frati, aseme, "Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena..."(Yer:51:1,8,28,37,58,62-64) uwiano kati ya unabii wa Isaya, ulioandikwa miaka 100 kabla ya mamlaka ya Babeli kushamiri, na ule wa Yeremia, ulioandikwa wakati dola na jiji vilipokuwa
katika kilele cha utukufu wake ni mtimilifu. Kwa watu wa siku zile itakuwa ilionekana kama ilivyo kwetu leo tuambiwe miji mikubwa kama London, New York au Sydney itaangamizwa ibakie magofu milele. Katika enzi hii ya silaha za nyuklia, jambo hilo linawezekana; lakini manabii wa Israeli walitamka hayo zaidi ya miaka 2500 iliyopita wakati hakuna ambaye angeweza kuota kwamba uharibifu kamili namna hiyo ungewezekana.


Historia inaonyesha jinsi ambavyo unabii huo wa maanguko ya Babeli ulivyotimizwa hatua kwa hatua. Wavunjaji wa Kwanza walikuwa Wamedi na Wajemi katika karne ya sita (K.K). Kuanzia wakati huo umwamba wa Babeli ulianza kufifia. Baadaye walikuja Wayunani chini ya Aleksanda Mkuu, wakifuatiwa na Warumi; baada yao makabila kadhaa yapendayo vita kama Wapathi, Waarabu na Watarta.
Kwa karne nyingi mahali halisi pa jiji la Kale la Babeli palikuwa mahame, yaliyoepukwa - wasafiri wasemavyo - na wahamaji wanaotangatanga. Ni hivi karibuni tu wataalamu wa kihistoria wachimbuao chini ( Archaeologists), walipochunguza eneo hilo katika nusu ya kwanza ya karne ya 19, na kugundua mabaki ya kuta kubwa, mahekalu ya nguvu na malango, na masanamu
makubwa yaliyoonyesha ulimwengu ulioshikwa na butwaa jinsi ukuu wa Babeli ulivyokuwa enzi zake. Kwa hiyo historia inatuonyesha jinsi Babeli 'Utukufu wa falme,'

ulivyoangushwa na kuachwa, kama manabii wa Israeli walivyotabiri ingekuwa. Sasa tunageukia mfano wa pili unaotofautiana, unaotuonyesha pia uhakika wa unabii wa Biblia katika:-


HATIMA YA MISRI
Misri iliwahi pia kuwa dola yenye nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati. Ukubwa wake ulikuwa kama 1600 (K.K) wakati majeshi ya Mafarao wavamizi walipojisogeza kusini ndani ya Sudani, Magharibi kuambaa pwani ya Afrika ya kaskazini, kaskazini kupita ardhi ya Kaanani (baadaye Israeli), na ndani ya Syria. Uvumbuzi kaatika baadhi ya Mahekalu ya kale, minara na makaburi
umedhihirisha utukufu wa Mafarao ulivyokuwa katika kilele cha kuu wao.

Lakini ilipofikia miaka ya 1400 K.K nguvu ya Misri ilianza kurudi nyuma kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukua kwa Ashuru, na baadaye Babeli. Hata hivyo katika kipindi Waisraeli walipokuwa wakiikalia Kanaani, 1400-600 K.K, Wamisri waliingilia kati kwa nyakati mbalimbali siasa za Mashariki ya Kati, kwa mafanikio fulani. Waisraeli, walipokuwa wakiogopa
uvamizi kutoka Ashuru na Babeli mara kwa mara walishawishika kutafuta msaada Misri badala ya kumtumainia Mungu wao.
Sasa manabii wa Israeli walikuwa na kitu maalum sana kusema juu ya hatima ya Misri. Nabii Ezekiel, ambaye matamko yake yalitolewa katika siku za Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kuanzia kama 600 K.K, alitangaza kwamba kutokana na hukumu ya Mungu, Misri ingekuwa upweke kwa miaka 40. Baada ya hapo kungekuwa na uamsho, lakini usiofikia ukuu wa nguvu zake za awali.

"Maana Bwana MUNGU aseme hivi; Mwisho wa miaka arobaini nitawakusanya Wamisri, na kuwatoa katika hizo kabila za watu, ambazo walitawanyika kati yao; nani nitawarudisha hata nchi ya Pathrosi, hata nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme duni (ufalme wa chini).
Utakuwa duni kuliko falme zote; wala hatajiinua tena juu ya mataifa; nami nitawapunguza ili wasitawale tena juu ya mataifa... Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu (Memphis), wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri. Ezk. 29:13-15; 30:13Hapa napo maana ya unabii huu inaeleweka: Misri ingekabiliwa na matatizo ya uvamizi na watu kuchukuliwa mateka. Ingawa hakuna kumbukumbu halisi zilizobakia za matukio hayo, lazima yatakuwa ni matokeo ya uvamizi wa Wababeli kwa Misri, kama Ezekiel mwenyewe alivyotabiri (tazama Ezek: 30:17-
20). Lakini huo usingekuwa mwisho wa Misri. Maana baada ya miaka 40, mateka wangerudi tena katika nchi yao wenyewe. Misri, kama ufalme usingeangamizwa: ungedumu lakini nguvu yake ingeshushwa sana - "Ufalme mdogo," usioweza kutumainia nguvu zake kukabili mataifa yanayopakana nayo tena.


Ufalme mdogo
Na ndivyo ilivyotokea. Tangu kama mwaka 600 K.K, Misri aliangukia chini ya watawala wa kivamizi, kwanza wa Wababeli katika karne ya 6 K.K; kisha Waajemi kati ya karne ya 6 na 4; alafu Wayunani katika karne ya 4; wakifuatiwa na Warumi karne ya kwanza K.K mpaka karne ya 5 B.K. Walifuatiwa na Waarabu na Waturuki kutoka karne ya 7 B.K na kuendelea. Hata Waingereza wameitawala Misri kwa kipindi katika karne ya 19. Kwa miaka 2500, Misri imebakia kama alivyotabiri Ezekiel kuwa ingekuwa, "Ufalme wa chini," wakati wote ikikaliwa na wengine. Lakini Misri na Wamisri hawakutokomea. Bado wapo,
na wameponea uhuru kiasi miaka ya karibuni, washukuru misaada mikubwa ya fedha wanayopata kutoka Marekani na Saudi Arabia.

Tuweke pembeni kidogo mawazoni swala la Misri wakati tukiangalia mfano wa tatu wa utabiri wa Biblia wa matukio ya mbele, kwa kutazama.
UNABII KUHUSU ISRAELI
Huu ndio uliojaa kuliko wote, kimaelezo ya utabiri wake, na pia katika wingi wa thibitisho zihusuzo ukweli wake kimatukio kihistoria. Tutazingatia tu mambo halisi mepesi yahusuyo hatima ya ajabu ya Waisraeli.Agano la Kale limeandika kwa ajili yetu jinsi Mungu alivyofanya ahadi madhubuti kwa Ibrahim (Kama 1800 K.K), iliyokuwa imemaanisha kati ya mengi kwamba, uzao wake ungekuwa taifa (Israeli), ambalo lingeimiliki nchi ya Kanaani, iliyoitwa baadaye Palestina. Kama 1400 K.K. Waisraeli walitolewa Misri wakati wa 'Kutoka' chini ya Mussa, na miaka 40 baadaye walianza kurithishwa nchi waliyoahidiwa. Lakini kabla ya hapo, kabla hawajaingia hiyo nchi, walionywa sana na Mungu kupitia kwa Mussa mkosi ambao ungewapata kama wakimwacha Mungu wao na kuabudu sanamu, na kuiga mambo ya Wapagani wa Kikanaani.Katika mlango wa 28 wa Kumbukumbu la Torati, kuna unabii wa ajabu sana - na ulikuwa onyo kali - juu ya balaa ambalo lingewafika Waisraeli kama hawakuwa watiifu. Msomaji anashauriwa kujisomea kifungu chote mwenyewe. Hapa tuna nafasi ndogo tu ya kuonyesha yaliyo msingi kimtazamo.
"Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote... BWANA atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako... Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA... BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia...wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote.." Kumb. 28:15,36-37,64-65.

Hapa napo unabii ulikuwa unaeleweka: Waisraeli wangetawanywa katika mataifa, kuishi huko katika mazingira ya taabu, wakibezwa na kudharauliwa. Ni ajabu iliyoje kuona maisha yao yalivyothibitisha uhakika wa maneno hayo!
Mtawanyo wa Wayahudi dunia nzima ulianza katika enzi za Waashuru katika karne ya 8, K.K. Jambo hili liliendelea wakati wa Wababeli kwenye karne ya sita. Baada ya sehemu yao kurudi kutoka Babeli siku za Wafalme wa Kiajemi, jumuia
ya Waisraeli iliishi katika ardhi yao kama 500 K.K mpaka siku za Kristo, chini ya tawala za kiajemi, Kiyunani na waliowafuata, na mwishowe Warumi. Katika mwaka 70 B.K, miaka 40 baada ya Kristo kusulubiwa msalabani, palitokea patashika mbaya kuliko zote. Jiji la Yerusalemu lilishambuliwa na kuporwa na majeshi ya Kirumi kwa sababu ya uasi; hekalu likateketezwa kwa moto na Wayahudi kutawanywa mateka dunia yote (ya Kirumi) - tazama kielelezo kwenye jalada. Wamekuwa huko tangu wakati huo, kama ilivyotokea; ncha moja wa dunia hata ncha nyingine!Na wamekosa, kama ilivyoandikwa mpaka hivi karibuni kutulivu', wakipata mateso na mara nyingine maangamizi. Wapogrom wa Urusi katika karne ya 19 na mpango wa Hitler wa uhilikishaji katika karne ya 20 ni mifano michache tu ya karibuni. Wayahudi wamekuwa kila mahali wakikabiliwa na
chuki na kukataliwa, kiasi kwamba uwepo wao kama jamii ya watu, ni mojawapo wa maajabu ya kihistoria. Tunaona vile vile ya kwamba Unabii huu juu ya hatima ya Waisraeli umeendelea kuwa kweli kwa zaidi ya miaka 2500 sasa. Nani angeweza kuliona hilo, tukizingatia mtawanyo ulivyokuwa na mateso, kwamba Wayahudi wangeendele kwa karne nyingi kuwa jamii kamili ya watu
inayoendelea kutambulika hadi sasa!Lakini ni zaidi ya hayo...


Lakini jambo la ajabu zaidi juu ya unabii kuhusu Israeli halijasemewa, kwani manabii walitabiri pia wazi wazi badiliko lisilotegemewa la mafanikio kwa Waisraeli. Fikiria, kwa mfano, utabiri wa nabii Yeremia, uliotolewa karibu miaka 600 K.K.
"Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa... nani nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki (30:3)"Basi sasa, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi...Tazama,
nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza, katika hasira yangu... nami nitawaleta tena hata mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao..." (32:36-38)
"Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza. Nami nitawasafisha na uovu wao wote..."
(33:7)
Na hapa pia hakuna utata juu ya lile alilokuwa akisema nabii: Kitendo kile cha kutawanywa na mateso kwa Waisraeli kitageuzwa. Wayahudi watarudi tenakatika nchi ile ile ambayo kutoka kwao walifukuzwa zaidi ya miaka 1990 iliyopita, na kuishi hapo kwa amani zaidi. Madondoo hayo mafupi kutoka kwa Yeremia, yanaweza kuzidishwa mara nyingi kwa matamko kama hayo kutoka Isaya na Ezekieli.\

Hatuhitaji hasa kuzama sana ili kuonyesha jinsi utabiri huo wa kurudishwa upya Israeli ulivyotimizwa kikamilifu. Ushirika wa kisayuni ulikuwa na nguvu kati ya Wayahudi waliotawanywa katika nchi nyingi mwishoni mwa karne ya 19. Uanzishwaji wa Palestina kuwa makao ya kitaifa ya Wayahudi mwaka 1917 ulisababisha idadi yao kukua haraka katika nchi hiyo. Hili lilipozua chuki kali kwa Waarabu, Wayahudi walipambana na jaribio lao la kuwakandamiza mwaka 1948, na kuanzisha taifa lao la Kiyahudi. Nalo lilipanuliwa mwaka 1967 katika jaribio la pili kwenye vita vya siku sita, ambapo Israeli ilijichukulia upya sehemu
kubwa ya ardhi yake ya kale, na Yerusalemu kuwa makao makuu ya taifa lao chini ya utawala wao wenyewe, kwa mara ya kwanza katika miaka 2500. Kwa kifupi, kuibuka kwa taifa huru la Wayahudi Mashariki ya Kati imekuwa ni kitu kisichotegemewa kabisa. Chini ya miaka 100 iliyopita hakuna mchunguzi wa kisiasa aliyedhani inawezekana.

Hatujihusishi hapa na 'siasa' za jambo hilo. Tunachoangalia hasa ni unabii wa Biblia. Kuna mengi mengine Biblia inayosema juu ya Wayahudi. Manabii wanasema, kwa mfano, kwamba kutakuwa na matatizo makubwa Mashariki ya Kati, na kwamba Israeli itafikishwa kwenye toba mbele ya Mungu wake. Hapo ndipo unabii wa mwisho wa kurudishwa upya na amani utakapotimia. Hapa
tungependa kusisitiza tu kwamba manabii walitabiria kurudi kwa Waisraeli kwenye ardhi yao wenyewe, na sisi katika karne hii tumeona kwa macho yetu utabiri huu ukianza kutimizwa.


UNABII AINA TATU - HATIMA TATU
Baada ya kufika hapa, ni kitu cha manufaa kufanya muhtasari wa yale Babeli: Ile dola kuu kabisa Mashariki ya Kati, ilikuwa ipoteze mamlaka yake, na jiji lake kuu maridadi sana liwe mahame, likiepukwa na watu na wanyama pori. Na ndivyo ilivyotokea.Misri: Nayo dola kuu nyingine, ingelibakia kuwa ufalme unaotambulika. Wamisri wangeendelea kukaa katika nchi yao wenyewe. Lakini mara zote wangetawaliwa na mamlaka zingine, wakibakia 'ufalme wa chini.' Na ndivyo ilivyokuwa.

Hatima ya Israeli haikuwa ya kufananishwa na yoyote kati ya hizi. Wakiwa wametawanywa mbali na nchi yao kwenye nchi nyingine, na kupata matesomakali na manyanyaso, wangerudi tena katika nchi ile ile walipotawanywa, na kujianzisha tena hapo.
Tuzingatie kwa makini yafuatayo:-

1. Unabii kuhusu mataifa haya ulitolewa kama miaka 2500 iliyopita.
2. Ukweli wake umekuwa matukio halisi ya kihistoria mpaka leo.
3. Mifano hiyo hapo juu ilihusu mamlaka tatu tofauti, zenye hatima tatu
tofauti kabisa. Moja ilikuwa kutoweka; ya pili kubakia, lakini kukaliwa na mataifa mengine; ya tatu kuangamizwa, na watu wake kufukuzwa na kutawanywa dunia nzima, na bado hatimaye kurudishwa katika nchi ya awali.

4. Hii sio 'mitazamo ya mbeleni ya kisiasa,' ya wachunguzi wajanja wa
kisiasa, bali ni utabiri usiokosea wa mambo.

Nani angeweza kujua?

Utabiri wa mambo wa muda mrefu hivyo unawezekanaje? Kuna jibu moja tu linaloridhisha; Lazima awepo aliyeyajua kabla; lakini ni nani?

Kwa hakika hakuna mtu wa miaka 2500 iliyopita au tangu hapo, angeweza kujua. Tukiupima utabiri wa namna hii kibinadamu tu hauelezeki.

Lakini hata hivyo, manabii wa Agano la Kale hawakudai wanatabiri kwa uwezo wao. Walisema walikuwa wakisema maneno yaliyotoka kwa Mungu. " Hivi ndivyo asemavyo BWANA," ndivyo walivyokuwa wakianza kusema wakati wote.
Kama Mungu alikuwa nyuma ya yale waliyosema, tunapata jibu la nani aliyejua.' Hakuna maelezo mengine yanayoleta maana. Unabii tuliouchunguza hapa ulihitaji uwepo wa Mungu kama chanzo chake. Inaleta maana.Mifano hii mtatu tuliyoinukulu ilichaguliwa kuonyesha aina tofauti za unabii wa Biblia. Lakini mifano iko mingi. Tungeweza, kwa mfano, kuchunguza
ule unaomhusu Yesu Kristo: alipaswa kuwa na mzao wa Ibrahim, na wa Daudi; alikuwa azaliwe Bethlehem; alikuwa akataliwe na watu wake; na bado afe kifo cha upatanisho kwa ajili yao; na maelezo mengi mengineyo - yote yakiwa yametamkwa mamia ya miaka kabla hajazaliwa, na bado yakawa hivyo hivyo katika kuzaliwa, kwa Yesu, utumishi, kifo na kufufuka kwake.

Lakini tutahitimisha uchunguzi wetu mfupi kwa mifano miwili zaidi itakayoleta mpango wa kiunabii mpaka kufikia wakati tulionao.


BIBLIA NA MATAIFA
Unabii wa Daniel unao mpango wa kuvutia unaohusu kukua na kuanguka kwa dola, na hali ya mataifa ya kile kilichokuwa kikiitwa 'Dunia iliyostaarabika,' yaani mataifa ya Ulaya, Mashariki ya Kati, Misri na pwani ya kaskazini mwa Afrika, yote yanayoizunguka Bahari ya Kati (Mediterranean sea).

Unabii huu ulitolewa wakati Daniel alipokuwa mateka katika boma Babeli karne ya 6 K.K. Ukweli wake umejidhihirisha katika historia tangu siku hizo hadi sasa.

Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akiwa amejaa kujikinai na ufahari, aliona katika ndoto sanamu moja kubwa sana ya mtu, yenye sehemu tano (tazama uk.
16,17):
1. Kichwa cha sanamu kilikuwa cha dhahabu.
2. Kifua chake na mikono kilikuwa cha fedha.
3. Tumbo lake na mapaja lilikuwa la shaba.
4. Miguu yake miwili ilikuwa ya Chuma.
5. Lakini nyayo na vidole zilikuwa mchanganyiko wa chuma na udongo wa mfinyanzi.

Kisha jiwe likatokeza 'lililokatwa kutoka mlimani bila kazi ya mikono.' Likaangukia nyayo za sanamu ile, likaiangusha yote chini, na kuzisaga sehemu zake kuwa unga, kiasi kwamba upepo ukaupeperushia mbali. Baada ya hapa lile jiwe likakua kuwa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.

Nebukadreza alisumbuliwa sana na hatima ya sanamu ile, kwa sababu hakuna kati ya watu wake wajuzi aliyeweza kumwambia ilikuwa na maana gani.

lakini Daniel, nabii wa Israel alimwambia "kuna Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho "Dal. 2:28

Kwa hiyo Daniel alielezea maana ya sanamu ile. Kichwa cha dhahabu kiliwakilisha utawala wa Nebukadreza mwenyewe. Ulikuwa ufuatiwe na mwingine, wa hali ya chini zaidi (kifua na mikono ya fedha); na baada ya huo wa tatu (wa shaba); alafu wa nne (miguu ya chuma) ambao ungekuwa na nguvu na kishindo, lakini nyayo na vidole viliwakilisha falme zilizogawanyika, nusu
nguvu na nusu dhaifu". (Ms. 37 - 42) Kitu kimoja ni wazi: Sanamu hii iliwakilisha makabidhiano ya falme zenye
nguvu, na sio vigumu kuzitambua. Wa kwanza tunafahamu; ulikuwa ni dola ya Babeli. Katika kifungu cha 8 (Mstari wa 20 - 21) tunaambiwa afuataye angekuwa Mwajemi na Myunani. Dola ya nne, ' kuu na inayotisha', haikutajwa wazi wazi katika unabii wa Daniel. Historia inathibitisha tabiri hizi kwa wingi. Kama 530 K.K. mamlaka ya Babeli iliangushwa na Wamedi na Waajemi, ambao mwishoni walianzisha dola ya kiajemi. Ilidumu miaka 200, na baadaye kuangushwa kama 330 K.K. na Aleksanda Mkuu (Alexander the Great) aliyesimamisha dola ya Kiyunani.Ni dola gani kubwa iliyofuata falme za mrithi wa Aleksanda? Hakuna mashaka juu ya jibu: ilikuwa dola ya Rumi. Warumi walivamia maeneo ya iliyokuwa dola ya Kiyunani kuanzia karne ya 2 K.K. na kuendelea. Kwa miaka 500 iliyofuata, Rumi ilikuwa mamlaka kuu kuliko zote duniani. Dola yake ilitanda kama sehemu yote ya dola zile tatu, na kuenea mbali ndani ya Ulaya, Mashariki ya Kati na nchi zote zinazozunguka Mediterranean. Walifanikisha uvamizi wao kwa ukatili mwingi kama ilivyodokezwa na maneno "nguvu kama chuma."


Katika karne zake mbili za mwisho za kuwepo kwake, iligawanyika sehemu mbili: ya magharibi makao yake makuu yakiwa Rumi, na ya mashariki makao yake makuu yakiwa Constantinople - miguu miwili ya ile sanamu.


Mungu anayefunua siriLakini ni nini kilichotokea baada ya dola ya Warumi kuvunjika katika karne ya 5 B. K. Haikufuatiwa na dola nyingine yoyote kuu, na kwa kweli haijakuwapo dola ya tano ya kulinganishwa kimamlaka, pamoja na kuwepo jitihada kubwa za watu wenye tamaa kuunda nyingine. Maeneo ya dola ya Kirumi yalimeguka kutokana na uvamizi wa makabila jeuri ya Kihan, Kigoti, Kivisigoti na Kivandali, yaliyoanzisha tawala zao wenyewe tofauti. Mataifa ya sasa ya Ulaya yametokana na falme hizo. Katika kipindi chote cha historia ya miaka 1500 mpaka sasa, mataifa hayo yamebakia katika mgawanyiko, kama ilivyoashiriwa na nyayo za ile sanamu - nusu chuma na nusu udongo: " nusu una nguvu, na nusu yake umevunjika ... hawatashikamana. "(Dan. 2:42-43)

Angewezaje Daniel kujua kuwa mamlaka ile kuu ya Nebukadreza
ingefuatiwa na zingine tatu, ya nne ikiwa na nguvu zisizo za kawaida, ambayo kamwe isingelifuatiwa na ya tano? Angejuaje kuwa baada ya ile ya nne kuanguka, wau wake wangesambaratika kuwa nchi zilizomeguka, zisizo na umoja kati yake? Kwa vyovyote, kwa yeye mwenyewe asingeweza kujua kitu, wala yeyote mwingine. Lakini Daniel hatuachi bila maelezo:

"Yupo Mungu mbinguni afunuaye siri.. Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye, na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti." (Ms. 28,45) Unawezaje kuuelezea uwepo wa unabii wa Daniel 2, karne kadhaa K.K, na bado kuwa na mtizamo sahihi wa madola na mataifa mpaka hivi leo, baada ya zaidi ya miaka 2000? Kama kweli kuna 'Mungu mbinguni,' unaweza kuelewa. Kama Hayupo, hakuna maelezo yanayoridhisha.Tutatoa maoni katika sehemu ya hitimisho, juu ya jiwe linaloigonga ile sanamu miguuni na kuiangusha yote chini. Kwa ajili ya mfano wetu wa mwisho wa kinabii tuone kwanza.


NYAKATI TULIZO NAZO
Ingawa unabii tuliouzingatia mpaka sasa umeendelea kutimia hadi hivi
leo, ulihusu zaidi matukio ya siku nyingi za nyuma (ukiacha urudishwaji upya wa Waisraeli hivi karibuni katika ardhi yao ya kale). Je, kuna kinachosemwa na unabii wa Biblia juu ya nyakati tulizo nazo kuweza kutuongoza katika siku hizi?
Kipo hasa! Tena ni ajabu kinavyotofautiana sana na matazamio na fikra za kibinadamu. Karne ya 19 ilikuwa kipindi cha matumaini. Maendeleo makubwa yalikuwa yakipigwa. Ujuzi wa Kisayansi ulivyoongezeka ulileta maendeleo haraka kiufundi na uzalishaji mkubwa viwandani. Hili lilikuwa lilete neema (ingawa sio kwa walio maskini sana). Elimu ilipanuliwa kuwafikia wengi,
na matumaini ya maana yalipatikana. Watu walioelimika zaidi, ilidaiwa, wangejishughulisha na sanaa kama fasihi, muziki na uchoraji. Maadili ya jamii kwa ujumla yengeboreka. Wanasiasa waliahidi kuleta mpango mpya wa kijamii wa haki na usawa kwa wote. Vile ambavyo watu wangetajirika, ndivyo ambavyo wasingeoneana kijicho. "Tokomeza umaskini, na ndivyo utakavyotokomeza uovu, lilikuwa ndilo bango. Wakati uwezo wa juu wa akili ya mwanadamu ukitumiwa, ilikuwa amani ijengeke kati ya mataifa. Viongozi wa kanisa nao wakatazamia kwa dhati kueneza Injili dunia nzima. Kujiendeleza mwanadamu na kuboresha maisha, kwa mtu binafsi na kwa jamii, vilichukuliwa juu juu tu. Hali ya baadaye ikaonekana nzuri.


Amani na maendeleo?
Kinyume cha matazamio hayo, matukio ya karne ya 20 yamekuwa mfadhaiko. Ndoto za maendeleo na amani zimefifia. Vita viwili vibaya sana vya dunia, vikiwa vimechinja mamilioni na kuleta uharibifu usiosemekana wa mali na mateso, vimefuatiwa na uundaji wa silaha kali za maangamizi ambazo hazijawahi kutengenezwa. Mawazo ya utatuzi ya aina mbalimbali ya 'wenye busara' wa karne ya 19 yamekuwa bure. Kupanuliwa elimu hakujafuatiwa na maadili zaidi, badala yake na kukua kwa dhuluma, choyo, vurugu na uvunjaji sheria. Dini ya Kikristo, mbali na kuwabadili mataifa, imekuwa katika kurudi nyuma duniani pote. Demokrasia katika siasa haijajidhihirisha kuwa muarobaini wa maovu katika jamii kama ilivyotarajiwa. Mwishowe pigo baya zaidi - sayansi imethibitika kuwa silaha ya kutisha ya makali kuwili. Mbali na kuwa enzi ya amani, karne ya 20, ya ustaarabu, imekuwa wakati wa migogoro na mapambano. Ndio maana mtizamo wa wengi umekuwa ule wa kukata tamaa. Inaonekana kama hakuna anayeweza kufanya kitu.


Sasa unabii wa Biblia unasemeaje hali hizi?
Biblia ina utabiri wa kueleweka kabisa juu ya siku za mwisho, 'nyakati za
mwisho,' wakati harakati za mwanadamu katika nchi zitakapofikia hatua mbaya. Sio picha ya maendeleo endelevu na amani, bali ya matatizo duniani na hofu. Mfano wa wazi sana na unaotugusa upo katika yale Yesu aliyowaambia wanafunzi wake walipomuuliza nini ingekuwa ishara ya kurudi kwake duniani na ya 'mwisho wa dunia.' Anawaambia kwanza juu ya hatima ya Wayahudi.

" Wataanguka (Wayahudi) kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa (wasio Wayahudi), hata majira ya Mataifa yatakapotimia." (Luka 21:24)


Sasa haya ni maelezo mafupi juu ya yale tuliyoyaangalia yahusuyo unabii kwa Israeli. Wayahudi wangeng'olewa kuwa mateka kati ya mataifa yote; Yerusalemu ingekaliwa na mamlaka za kimataifa. Gundua kwamba Yesu anasemea mwisho wa hili 'hata majira ya Mataifa yatakapotimia.' Tumeona mwanzo wa jambo hili katika wakati wetu. Yerusalemu haikaliwi tena na watu wa nje - unakaliwa na Israeli yenyewe.


Mashaka na hofu duniani Kwa hiyo yale anayoendelea kusema lazima yahusiane na siku hizo - siku za Israeli kurudishwa katika nchi yao wenyewe. Hivi ndivyo anavyotabiri.

"Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya Mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu; kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika." (Ms. 25 - 26) Hii sio picha ya amani na maendeleo. Ni dunia ya hekaheka na kuchanganyikiwa, hofu ikiikumba mioyo ya watu wanapofikiria mambo yanayotokea katika 'makao ya watu duniani' kama neno alilotumia Yesu linavyomaanisha.

Mtume Paulo, akiwa anaandika kama miaka 35 baada ya unabii huo wa Yesu, anasema hivi juu ya hali ya siku za mwisho.
"...siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, na wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiopenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake;.."

Hii ni sura ya ajabu ya ustaarabu; mtu anatupilia mbali vizuizi vyote na kuzifuata tamaa zake mwenyewe bila kujali matokeo yake. Hakuna asiyeona uwiano wa ali hiyo na mambo yalivyo katika dunia yetu ya sasa.

Kwa hiyo hali ni hiyo; wakati wajuzi wa mambo miaka 100 tu iliyopita walitazamia kwa dhati sana, kipindi cha maendeleo na amani kwa mataifa ya dunia, Biblia, katika maneno ya Yesu na Paulo ilitabiria dunia ya fujo, hofu na kuchanganyikiwa, nyakati za migogoro, kujifanyia mtu atakacho, na chuki.

Wanafalsafa wetu wa kibinadamu walikosea; Yesu na Paulo walikuwa sawa!
Lakini waliongea na kuandika zaidi ya miaka 1900 iliyopita. Waliwezaje kujua?
Sababu pekee ni kwamba hawakusema maneno yao wenyewe, bali maneno ya Mungu Mwenyewe. Ni Mungu aliyejua, akampa uwezo Mwanawe na mtume wake kutufunulia hali ya siku za mwisho.

HITIMISHO
Kuna majumuisho kadhaa muhimu tunayoweza kuyafikia kutokana na kuchunguza kwetu unabii wa Biblia.

Kama Biblia imejithibitisha kuwa sahihi kiasi hiki katika utabiri wake wa matukio katika historia ya mwanadamu - hatima ya Babeli, Misri na Israeli, na pia katika kukua na kuanguka dola, na hali ya dunia kwa wakati huu - itakosa kuwa sawa katika utabiri wake wa matukio yaliyobaki?


Chukulia yale maono katika sanamu katika Daniel, kwa mfano.
Hatujatolea maoni bado juu ya ile hatua ya mwisho: Jiwe, " lililokatwa kutoka mlimani bila kazi ya mikono," liliipiga ile sanamu chini ya miguu, likaivunjavunja, na lenyewe "likawa mlima mkubwa, na kuijaza dunia yote "(Dan. 2:35).


Sasa maana ya jumla ya hili iko wazi: kitu kigeni, kisichokuwa sehemu ya dola za sanamu na falme, kinaziharibu na kuchukua nafasi zake duniani. Kwa kuwa 'bila mikono,' maana yake ni 'bila mikono ya mwanadamu', lile jiwe lazima litakuwa linasimama badala ya nguvu isiyokuwa ya kawaida ya kibinadamu. Lakini Daniel anatuambia mwenyewe maana yake:


" Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele... utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. " (Ms. 44)Serikali za sasa na mamlaka za dunia zitaondolewa, katika tukio moja la aina yake, Mungu atakapoingilia kati na kusimamisha Serikali yake Mwenyewe. Kuondoa utata ieleweke kwamba, sio umati wa watu unaoangamizwa: ni nguvu na mamlaka za falme za kibinadamu, zitakazong'olewa na ufalme mpya wa Mungu.

Unabii mwingi mwingine unatueleza jinsi ufalme huo utakavyokuwa; maongozi yake timamu, mafundisho yake yenye kweli, na amani utakayoleta hatimaye duniani kwa watu wote kutokana na kumtambua kwao 'Mungu wa mbinguni!' Soma kwa mfano Isaya 2:1-4 kupata picha kamili na ya kusisimua juu ya mataifa katika enzi hiyo ijayo.


Lakini ni kwa namna gani mageuzi hayo makubwa yanaweza kufanikishwa duniani? Agano jipya linatupa jibu. Na hasa ni Yesu mwenyewe anayetuambia katika unabii ule wa nyakati za taabu ya hofu kwa mataifa yote. Maneno yake yaliyofuata ni haya "Hapo ndipo watakapomwona mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi" (Luka 21:27)Anasema atarudi tena mwenyewe. Kurudi kwa Kristo duniani ni wazo mojawapo kuu katika mafundisho ya Yesu na mitume katika Agano Jipya na linakubaliana kabisa na manabii. Soma zaburi 72 kupata kinachosemwa juu ya utawala wake.

Sasa, kwa hakika, hili ndilo linalopaswa kutushughulisha sana: Kama unabii wa Biblia kuhusu mataifa na dola umekuwa kweli kama ilivyo kwa zaidi ya miaka 2000, hayo mengine yaliyotabiriwa yatakosa kutimia? Sio kukosa busara kusema: "sawa nakubali manabii walikuwa sahihi katika utabiri wao katika mambo haya ya kihistoria, lakini siamini wanayosema juu ya yajayo kutuhusu sisi." Kwa nini? Wametoa uthibitisho kwamba hawakuwa wakitoa mawazo yao wenyewe, bali makusudio hasa ya Mungu. Yote yale wanayosema yanapaswa kutufanya tujali sana.

Kitu cha muhimu Lakini bila shaka kuna zaidi. Unabii huu wa ajabu unapatikana katika Biblia, na sio mahali pengine popote duniani. Hakuna maandiko mengine, hakuna vitabu, hakuna matamko mengine yoyote ya mwanadamu yanayoweza hata kwa mbali kulinganishwa na Biblia. Lakini Biblia inatuambia kwamba Yesu alikuwa mwana wa Mungu; mambo aliyosema yamehifadhiwa kwa ajili yetu katika Injili za Agano Jipya. Pamoja na mafundisho ya mitume wake Petro, Yohana na Paulo, wanatufunulia ukweli ambao hatuwezi vinginevyo kuujua. Wanatuonya juu ya ukweli kuhusu kifo; wanaeleza kwa nini Injili ni 'habari njema,' 'uweza wa Mungu uuletao wokovu' (Warumi 1:16). Wanatutia moyo na ahadi ya uzima wa milele katika mpango mpya atakaouanzisha Kristo atakapokuja. Ndio maana inatupasa kuisoma Bilia. Inaweza kutupa utofauti wa muhimu kati ya utupu wa kifo, na tumaini la nguvu la maisha yasiyo na mwisho.Usomaji wa makini wa Biblia utatuhakikishia kuwa Mungu yupo, anatawala, na kwamba anatuita tuwe wafuasi wa mwanawe. Biblia ipo kwa ajili yetu. Tunafanya vizuri kujali inachosema.

CC Free ideas
 
Last edited by a moderator:
You know why you abandoned your ID'S Pundit, Bluray Brooklyn etc sasa unatumia IGNORE LIST

Ishmael, look who's talking now, jamaa ameniambia niki-reply post zake ni kama nimemjibu.. who is contradicting himself now?
you simply don't need "proof" to believe that God is there or not, Mungu ni Roho, faith is needed and not scientific proofs. Unaamini, vema. Huamini, kaa hivyo hivyo, maana anayetaka ukweli angeshaujua tangia zamani.
sasa anakataa uwepo wa Mungu, lakini naona kwenye signature yake ameweka Mithali 23:9 "Usiseme masikioni mwa mtu mjinga, kwa maana atayadharau maneno yako yenye busara". Cha kushangaza Mithali ipo katika Biblia, na Biblia neno la Mungu! MUNGU HUYO HUYO asiyeamini uwepo wake.
so according to his signature, sijui kati ya sisi na yeye pamoja na huyo beki tatu wake ni nani wenye BUSARA na nani ni WAJINGA.
 
Ishmael, look who's talking now, jamaa ameniambia niki-reply post zake ni kama nimemjibu.. who is contradicting himself now?
you simply don't need "proof" to believe that God is there or not, Mungu ni Roho, faith is needed and not scientific proofs. Unaamini, vema. Huamini, kaa hivyo hivyo, maana anayetaka ukweli angeshaujua tangia zamani.
sasa anakataa uwepo wa Mungu, lakini naona kwenye signature yake ameweka Mithali 23:9 "Usiseme masikioni mwa mtu mjinga, kwa maana atayadharau maneno yako yenye busara". Cha kushangaza Mithali ipo katika Biblia, na Biblia neno la Mungu! MUNGU HUYO HUYO asiyeamini uwepo wake.
so according to his signature, sijui kati ya sisi na yeye pamoja na huyo beki tatu wake ni nani wenye BUSARA na nani ni WAJINGA.

The kid is frustrated with life. Guess what and who is the fool according to her signature:

Here is how it works:

Biblia inasema:
Mithali 23:9 "Usiseme masikioni mwa mtu mjinga, kwa maana atayadharau maneno yako yenye busara".

Biblia inamjibu:
Zaburi 14:1 Mpum-bavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

Halafu yeye bado ni kipofu.

HAKUNA BUSARA KWENYE SAYANSI NA HAWEZI KULETA USHAIDI WA BUSARA KWENYE SAYANSI.
 
ha ha ha hivi hii mijadala bado IPO? Kiranga.. Ishmael na Eiyer hapa mtakesha Kama hamjaamua hii discussion IPO ktk ujuzi au imani?


Kama ni IMANI ni sawa na kubeba maji kwenye pakacha kwasababu kuamini kila MTU aweza amini chochote na asiamini chochote kwakuwa tu ni mambo yasiyoonekana...

Kama ni UJUZI hapo unaweza pata mshindi maana ujuzi Una kipimo na uthibitisho...

sasa je mpo kiimani au ujuzi?
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha hivi hii mijadala bado IPO? Kiranga.. Ishmael na Eiyer hapa mtakesha Kama hamjaamua hii discussion IPO ktk ujuzi au imani?


Kama ni IMANI ni sawa na kubeba maji kwenye pakacha kwasababu kuamini kila MTU aweza amini chochote na asiamini chochote kwakuwa tu ni mambo yasiyoonekana...

Kama ni UJUZI hapo unaweza pata mshindi maana ujuzi Una kipimo na uthibitisho...

sasa je mpo kiimani au ujuzi?

Mwambie yule God Hater alete uthibitisho wa kuwa hakuna Mungu. Ili yaishe na sie tuwe Makafir wa ki non theist.
 
Ndio dunia Mkuu, unaonewa kwa kusema ukweli. Inshaalah, Mungu anawalipa kwa mabaya yote wanayo fanya.

Ha ha ha nikikumbuka jinsi walivyokufungia kazi huwa nacheka Sana...

Nimefurahi kukuona hapa mdau japo siku hizi sipati muda kabisa wakua hapa jf ni Mara chache mno...

Karibu Sana mkuu
 
Ha ha ha nikikumbuka jinsi walivyokufungia kazi huwa nacheka Sana...

Nimefurahi kukuona hapa mdau japo siku hizi sipati muda kabisa wakua hapa jf ni Mara chache mno...

Karibu Sana mkuu
Unajua, hii ni forum ya ajabu sana. Hapa unaruhusiwa kUmtuna Mungu na Yesu tena mitusi mikubwa mikubwa. Lakini ukisema ukweli kuhsu Muhammad na Allah, walah huto chukua muda utapelekwa Mapumbuziko yasio na hiyari. Lakini uzuri wake ni kuwa, UKWELI UNABAKIA PALE PALE. Watake wasi take hao Muhammadans au hawa God Haters the incarnation of Lucifer ukweli wamesha upata. Wlicho bakiza ni ligi.
 
Unajua, hii ni forum ya ajabu sana. Hapa unaruhusiwa kUmtuna Mungu na Yesu tena mitusi mikubwa mikubwa. Lakini ukisema ukweli kuhsu Muhammad na Allah, walah huto chukua muda utapelekwa Mapumbuziko yasio na hiyari. Lakini uzuri wake ni kuwa, UKWELI UNABAKIA PALE PALE. Watake wasi take hao Muhammadans au hawa God Haters the incarnation of Lucifer ukweli wamesha upata. Wlicho bakiza ni ligi.

Ha ha ha

Poa mkuu kila la heri
 
Unajua, hii ni forum ya ajabu sana. Hapa unaruhusiwa kUmtuna Mungu na Yesu tena mitusi mikubwa mikubwa. Lakini ukisema ukweli kuhsu Muhammad na Allah, walah huto chukua muda utapelekwa Mapumbuziko yasio na hiyari. Lakini uzuri wake ni kuwa, UKWELI UNABAKIA PALE PALE. Watake wasi take hao Muhammadans au hawa God Haters the incarnation of Lucifer ukweli wamesha upata. Wlicho bakiza ni ligi.

Ha ha ha..kweli.ila uliadimika aisee.ha ha ha...ila ulikuwa mkweli ile mbaya...sipati picha...uliwaumiza kichwa watu mpaka basi...nikikumbuka najiskia kucheka.
 
If God knows the future. there's nothing to resist us from doing our thing and change our courses, unless God set forth our destinies, The fact that we can not alter what God has decided for us is obvious. But worry not we are not even certain of it...
 
Back
Top Bottom