Hivi uwepo wewe unaweza kuuelezeaje labda?
Ukisikia "uwepo" unaelewa nini?
Kila kitu kwa context na framework yake.
Kwa hiyo, uwepo nao upo na context na framework pia.
Kuna uwepo wa kufikirika, ndio huo unaouongelea wewe wa dhana, kwamba ukiweza kukifikiria kitu kipo, kwa sababu umeweza kukifikiria.
But this is just abstract, not real.
Kwa sababu nishaonyesha hapo juu kwamba kuna vitu tunaweza kufikiria vipo, kitu kitakachomaanisha kwamba vipo, na hapo hapo tulafikiria kwamba havipo, kitu kitakachomaanisha kwamba havipo.
Kwa mfano, tuchukulie motokari.
Motokari unaweza kufikiria ipo.
Na unaweza pia kufukiria haipo, kwa maana ya kwamba unaweza kufikiria kwamba hakuna kitu kinachoweza kuenda kama motokari. Kuna primitive societies kibao.watu hawajaona magari mpaka leo wanaishi mosituni Amazon, Congo rainforest etc.
Sasa kama unasema kila kinachofikirika kipo, watu hawa wanavyofikiri kwamba ulimwengu hauna motokari, TV, video, simu, internet etc ina maana hivi vitu havipo?
Ukifikiri sana itaona kwamba kuwepo kwa dhana si kuwepo kwa uhalisi.
Kwa sababu unaweza kufikiri dhana ya kwamba wewe ulizaliwa kabla ya mama yako.
Lakini kuwepo kwa hii dhana hakaanishi kwamba wewe ulizaliwa kabla ya mama yako.
Kwa sababu ili wewe uzaliwe, ilibidi mama yako akuzae.
Kwa hiyo utaona, ingawa tunaweza kudhani kwamba inawezekana ukazaliwa kabla ya mama yako, dhana hii haina uhalisi.
Ndiyo kama habari ya mungu.
Ni dhana potofu tu.