Interested Observer,
Mkuu sina mashaka kabisa kwamba unapopinga matumizi ya kitu chochote ni lazima liwe na sheria fulani unayoitumia, iwe sheria ya dini au iliyofuatana na mazingira fulani in the case of Polygamy nadhani ni haki kusema kwamba tafsiri yako imetokana na uzungu na ndio maana unatumia maneno kama Primitive na civilisation..Sasa nikifuta hivyo itakuwa vigumu kukuelewa kwani mifano yako mingi inatokana na mtazamo wa wazungu au Kikristu..Sina maana they are wrong isipokuwa ni ktk kujenga hoja lazima kuwepo na sheria inayotufunga sote kulingana na mitazamo yetu tofauti..
Mkuu, labda hatuelewani hapa..binafsi sitetei Polygamy kwa sababu nafikiria kuwa ni ni haki ya mwanamme au commandment fulani ktk maisha ya binadamu isipokuwa natetea kwa sababu ni swala la choice ambayo kila mmoja wetu anaweza kuwa na mtazamo tofauti...
Siwezi kuoa wake wawili kwa sababu nje kabisa ya ukweli unajaribu kusema hapa kwani wapo watu wengi hawafungi ndoa kabisa kwa sababu zao wenyewe nje ya kutazama ndoa ya mke mmoja kuwa ni Civilisation ama Primitive..Na utaratibu huu ulikuwepo toka Adam yaani watu walichagua kuoa mke mmoja, wawili au watatu maadam wake wenyewe wameridhia hivyo sio jambo jipya hata kidogo.
Mkuu swala la ndoa halihusiani kabisa na civilisation kwa sababu mara nyingi Civilisation hulenga maendeleo ya jamii ktk swala fulani na asilimia kubwa ya matukio ya civilisation yametokana na Sayansi na technologia na bado kuna mazingira ambayo bado hayawezi kubeba ustaarabu mpya... Naweza tu kukubali kama utasema Polygamy imepitwa na wakati kutokana na mazingira tunayoishi..yet bado huwezi kusema ni primitive... Kwa mfano tulitoka ktk utumiaji Ngamia kama chombo cha Usafiri, tukatumia magari, gari moshi ndege na kadhgalika haya ni mageuzi ambayo yanakubalika na sote lakini huwezi kumwambia kitu mwarabu ya jangwani Saudia na yemen kuwa utumiaji ngamia ni kuwa uncivilised, Huko jangwani hakuna gari linaloweza kusafiri hata kama limetengenezwa vipi..
Hata hivyo nadhani ni bora zaidi nikirudi ktk mada hii kuelezea yale niliyo promise pamoja nna kwamba naweza jaza kurasa mia kwa maelezo..
Mkuu saikologia ni kipaji ambacho namshukuru Mungu kanipa na nimeweza kuona mengi, kusoma na kusikia mengi..Ktk dunia hii tunayoishi hakuna kitu kisichokuwa na sura mbili na zote zinaweza beba mazuri na mabaya lakini mara nyingi tunapokea yale ambayo hujenga na kuimarisha jamii zetu..
Nikitazama swala la kuoa mke mmoja ambalo hata mimi nimo, siwezi kutoa sifa zaidi ya experience yangu mwenyewe, lakini napotazama mabaya yake naona kwamba leo hii kutokana na mfumo huu tumekuwa na broken families kuliko wakati wowote ule..
Ni kweli badala ya mwanaume kuwa na wake wengi kwa mara moja tunaona 1.ziku hizi wanawake wakipitia ndoa zaidi ya moja wakizaa watoto kibao kila mmoja na baba yake..Kwa hiyo wale wanawake wanaodai kuwa wanataka nao uhuru wa kuwa na waume wengi (ngono) nadhani wanaupata sasa hivi lakini does it help them! au kujenga familia zao.. Ukweli ni kwamba hapana!.. wanawake kwa hesabu kubwa sana leo hii ni single mothers kuliko wakati wowote ule na bahati mbaya hawana uwezo wa kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja yaani Ku provide na kulea watoto, hata kama wamepewa nafasi kubwa ktk kujiendeleza lakini bado nguvu ya mwanaume kuwa responsible to provide, protect and head of the family inahitajika ili kuwapa watoto malezi mazuri..
Sasa pamoja na yote haya tumeona kuwa leo hii nchi hizo unazofikiria kuwa wako civilised wanaongoza duniani kwa 1. Single mothers, 2. Wanawake wanaohitaji social assistance (childcare), 3. Watoto wengi wametupwa foster homes, 4.Adoption, 5. Kufunguliwa kwa NGOs nyingi kama World vision zinazolea watoto..na kadhalika..
Nyuma ya yote haya utakuta kwamba kukosekana kwa mwanaume yaani baba ndio chimbuko lake, tofauti na ukitazama nchi ambazo swala la ndoa limetazama zaidi nje ya ngono na badala yake kujenga familia, na asilimia 80 ya ndoa zinazovunjika nchi hizi zinatokana na ngono..na Ukweli utasimama kwamba wanaume wengi hawapendi kuoa mwanamke ambaye tayari kisha kuwa na watoto wanaona ni mzigo.. wanaepuka responsibility ambayo ndio malengo ya ndoa na sio sex!.. Sisi wote tumekuwa tukifanya matusi tulipokuwa vijana na single kuliko wakati wowote ule na kama kweli ndoa ingekuwa inahusiana na sex basi nadhani kila mmoja wetu angebakia single maanake huko hatufungiwi na sheria ya aina yoyote!..
Je, kuna abuse ktk ndoa za wake wengi?.. Yes zipo na zipo sio kwa sababu ya wake wawili au watatu isipokuwa inatokana na tabia ya mwanaume mwenyewe kwani abuse wanazopata wanawake zinatokana na akili mbovu ya wanaume iwe mke mmoja, wawili au watatu... Mwanamme mshenzi ni mshenzi tu..
Je, ukewenza ni adha kubwa kwa wanawake?.. Yes lakini kama hutaki hakuna mtu anayekulazimisha na ustaarabu wa mapenzi ni kwamba mwanaume huomba na mwanamke ndiye mwenye maamuzi ya mwisho!..It's her Choice!
Kwa wasomaji wengine,
Hakuna sehemu yoyote ktk Biblia ama Kuran au kitabu chochote kile kinachosema (as commandment) kuwa ndoa ni ya mke mmoja. Yesu na Muhammad wote walipendekeza (maoni) kuoa mke mmoja na kama ingekuwa ni Amri hata Yesu mwenyewe angetakiwa kutuonyesha mfano kama alivyofanya ktk maswla mengineyo..
Mwisho, kwa wale wanaofikira kuwa Uislaam unawanyima haki wanawake na kuwatumia wao kama tool..kusema kweli watu hawa wamekosa busara ya kutazama undani wa jambo hili kwani ktk swala la ndoa siku zote mwanaume ndiye TOOL, Kama vile gari limetengenezwa kubeba abiria, lakini haiwezekani abiria kubeba gari..(kwa wale mnaofikiria otherwise).. Hii ni logic tu kwani mwanaume ndiye kizazi cha falimia zote..Familia nyingi zenye baba tofauti huwa hazina mapenzi wala mshikamano kwa ndugu kuliko zile zinazobeba jina moja..Ukweli huu hauna cilivisation hata kama Wayahudi wamemtumia Mama ktk kuongeza hesabu yaTaifa (Wayahudi) zima badala ya familia...