If our President has more than one wife: The question of human rights

Kuhukumu kuwa wanawake ni wajinga hujatenda haki.Si wanawake wote ni wajinga, na si kila anayevumilia manyanyaso ni mjinga.Wengine huvumilia kwa vile hawana ubinafsi - umimi.Wanaona huruma kuacha watoto wao kunyanyaswa na wakati mwingine wanawapenda waume zao regardless.Huu ni upendo wa kweli.

Kwanza ungesoma post yangu yote ungeona niliposema wanawake wa namna hii nikimaanisha sio wote.

Pili, kuvumilia manyanyaso katika ndoa ni ujinga, period. Anyway you slice it, cut it, spin it, bado ni ujinga tu!

Tatu, kwenye mapenzi ya kweli hakuna kunyanyasana. Kuna kupendana. Mtu akupendaye hawezi kukunyanyasa. Kwa nini umnyanyase mtu umpendaye? Mtu umpendaye unamtendea kwa upendo na mapenzi ya dhati. Na sielewi inakuwaje mtu anampenda mtu amnyanyasae.

Nne, hivi kweli wewe ni mwanamke au unatuzuga tu hapa? Kama kweli wewe ni mwanamke basi sijui hata nikwambie nini maana unatetea kubaki kwenye abusive relationship kwa kisingizio cha penzi. Mapenzi gani ya kutesana hayo.

Tano, have a wonderful day!
 
You nailed it right Wameno!

Nakumbuka miaka ya nyuma nili muuliza mama yangu mzazi hivi kwanini hakuamua kuondoka kuachana na manyanyaso ya baba ambayo ilikuwa ni pamoja na vipigo, kumdhalisha mbele za watu, na kumzalia watoto nje ya ndoa? Mama yangu alinipa jibu moja zuri sana kwamba Angeondoka nyumbani sisi (wanae) tusingekuwa tulivyo!

Hiyo sentensi sitakaa niisahau, ni kweli wamama huurumia sana watoto wao na hivyo kuvumilia mateso/manyanyaso toka kwa waume zao!

Somo kubwa kwetu jameni wababa tupende wake zetu na tutunze ahadi zetu jinsi tulivyo waahidi! kwa wenye mitara ni wazi 'PENZI HALIGAWANYIKI' tusidanganyane!
 
Mimi nakataa katakata! Mwanamke kutoondoka kwenye abusive relationship na kutoa kisingizio cha watoto sijui nini ni ujinga mtupu. Yaani hiyo reasoning iko flawed kichizi. Yaani mtu uko radhi watoto wako waone, wakue wakiona jinsi unavyokuwa abused? Unajua ina madhara gani hiyo kwa watoto hasa wale walio katika formative years?

Astaghafururah!! Mnanishangaza kweli nyie. Anyways, kila mtu ana threshold zake za kuvumilia. Mimi threshold yangu iko chini sana. It's one and done. Hakuna cha second chances hapa.
 
Mama na Womenofsubstanc,

Hata hivyo, niwaache na kicheko kidogo - mbona hamzungumzii haki ya mwanaume ktk ndoa.. Iweje sisi tu ndio tuombe uchumba na mwanamke ndiye mwenye last say akisema NO hakuna ndoa!..why can't we have the last say on divorce!.. si tumegawana madaraka... kwi....kwi.....kwi!

Mkandara sheria hizi zinatofautiana toka nchi moja hadi nyingine. Ndio maana nilitahadharisha kuwa naongelea Tanzania.

Sikia, nadhani suala la kuombana uchumba ni la kihistoria katika jamii husika. Najua kuna jamii mbalimbali duniani ambazo mwanamke ndio anataka uchumba. Huku kwetu sijui ilikuwaje wanaume ndio wakawa wakitaka uchumba.

Kwa sababu mwanaume aliomba uchumba, hawezi kuwa na last say kwenye divorce pia. Kumbuka wanawake wengi hawaolewi kwa ajili ya mapenzi, most of them wanaolewa kwa vile ndio option waliyonayo at hand...hivyo hujifunza mapenzi wakiwa ndani ya uhusiano au ndoa. Hujifunza kumpenda huyo mwenza.

Ingekuwa nasi tunafuata nafsi zetu, kutaka kuolewa na wale tunaowapenda tu...basi nadhani wengi wa wanaume wangekosa wake! Hivyo wanawake kuwa na last say kwenye suala la divorce ni kuonyesha tu umuhimu wa huyo mwanamke. Ulimuomba penzi akaamua kukupa, so wakati wa kulimaliza pia ana uamuzi wa mwisho. Ukiwa unaomba inabidi uwe mnyenyekevu na usubiri matokeo.

Haya ni mawazo yangu sidhani kama ni jibu sahihi kwenye suala lako la mwisho.
 
Mama na Womenofsubstanc,
Dada zangu labda mnifahamishe mimi.. Hivi katika ndoa hizo za Kizungu kisheria mwanamke anaweza kuondoka tu bila kudai talaka?...Je, mwanaume hawezi pia kukataa kutoa talaka na hakuna talaka inayoweza kukubaliwa kisheria hadi swala zima limekuwa solved na mahakama as if waliooana wameoana kwa sheria za nchi..

Nachojaribu kusema hapa talaka ni haki ya mwanamke ndani ya ndoa ambayo haikuwezekana..haijalishi kuwa ni dini gani ama sheria ya nchi gani isipokuwa maamuzi..ndipo unaona waislaam wameingia na swala la mahakama ya kadhi kwa sababu sheria zinazotumika ktk kuota hukumu za ndoa hasa za kidini kuna ubadhilifu na mara nyingi mwanamke amekuwa akifukuzwa ndani ya nyumba na watoto wake..
Hakuna compesation ya kweli zaidi ya nani mwenye nguvu kisheria.
Binafsi napingana na mahakama ya kadhi tu pale napotazama kuwa ndoa nyingi nchini hazikufungwa kwa kufuata sheria za dini zaidi ya kisomo na Sheikh..

Hata hivyo, niwaache na kicheko kidogo - mbona hamzungumzii haki ya mwanaume ktk ndoa.. Iweje sisi tu ndio tuombe uchumba na mwanamke ndiye mwenye last say akisema NO hakuna ndoa!..why can't we have the last say on divorce!.. si tumegawana madaraka... kwi....kwi.....kwi!

Kaka..kweli u made me smile maana nashindwa kucheka nikiwaza mambo mengine yanayoendana na joke hiyo.
Kimsingi nadhani ulichosema kina ukweli ndani yake unapozungumzia haki kupitia sheria iwe ya kidini au kiserikali ( kwa lugha nyepesi).Mwisho wa ndoa ni ama talaka yenye kufuata utaratibu au kifo. Kwenye kifo hakuna malumbano. Kwenye talaka hapo kuna kazi.Ingekuwa rahisi namna tunavyofikiri basi ingekuwa kila kukicha ni talaka na ndoa mpya - na sijui madhara yake yangekuwaje!Kama ulivyosema ndoa nyingi huanza vibaya bila kufuata taratibu na inapokuja kuzivunja kuna kazi.Tupende tusipende kuomba/ kudai /kutoa talaka ni mlolongo unaokatisha tamaa.Pale mtu anapoona unashadidia sana talaka basi kutakuwa na jitihada za ku frustrate na hii imetokea mara nyingi.Mwisho wa siku inaonekana kama vile wanawake ni wajinga wanan'gang'ania kukaa ndani ya ndoa za mateso.Ingekuwa kama kwa wenzetu ambapo mifumo ya utoaji haki inafanya kazi sawasawa basi mambo yangekuwa si kama yalivyo sasa.
 
Rwabugiri,
Somo kubwa kwetu jameni wababa tupende wake zetu na tutunze ahadi zetu jinsi tulivyo waahidi! kwa wenye mitara ni wazi 'PENZI HALIGAWANYIKI' tusidanganyane!
Jamani tusitake kujidanganya hapa.. ukweli ni kwamba penzi linagawanyika laa sivyo tusingewapenda mama zetu, dada zetu kaka zetu, marafiki na jirani kwa mapenzi.. Tofauti moja tu ni kwamba hatuwezi kufanya nao mapenzi ya kimwili..Na kibaya zaidi ni kwamba ktk ngono hakuna sheria zaidi ya nyege zetu wenyewe.
Abuse ni abuse tu iwe mzazi wako, ndugu yako na kadhalika yote haya yanatokana na hulka mbaya ya mhusika. Wapo watoto waliokaa na wazazi ambao wamewa abuse kama huyo mama yako na sidhani kama kuna kipimo kizuri cha mapenzi kati yao. Ukimuuliza mzazi atasema nampiga kwa sababu napenda!...what a crap!
Lakini tusijaribu kutumia Mapenzi kwamba hayawezi kugawanyika.. hata ktk ngono watu wanatembea nje ya ndoa zao kila siku wakitumia kisingizio kwamba I don't know what happened -I LOVE U! na kesho bado ataamkia huko..
 
Rwabugiri,

Jamani tusitake kujidanganya hapa.. ukweli ni kwamba penzi linagawanyika laa sivyo tusingewapenda mama zetu, dada zetu kaka zetu, marafiki na jirani kwa mapenzi.. Tofauti moja tu ni kwamba hatuwezi kufanya nao mapenzi ya kimwili..Na kibaya zaidi ni kwamba ktk ngono hakuna sheria zaidi ya nyege zetu wenyewe.
Abuse ni abuse tu iwe mzazi wako, ndugu yako na kadhalika yote haya yanatokana na hulka mbaya ya mhusika. Wapo watoto waliokaa na wazazi ambao wamewa abuse kama huyo mama yako na sidhani kama kuna kipimo kizuri cha mapenzi kati yao.
Lakini tusijaribu kutumia Mapenzi kwamba hayawezi kugawanyika.. hata ktk ngono watu wantembea nje ya ndoa zao kila siku wakitumia kisingizio kwamba I don't know what happened -I LOVE U! na kesho bado ataamkia huko..

Mkandara penzi haligawanyiki. Kama linagawanyika basi utampenda dada yako sawa na unavyompenda mkeo na pia mama yako sawa na unavyompenda shangazi yako au binti yako. KIUKWELI PENZI HALIGAWANYIKI HATA SIKU MOJA. Lazima kuna mmoja unayempenda kuliko wote hapa duniani....iwe ni baba, mama, kaka, dada, daughter or son, mkeo au ex-mchumba, kimada au yeyote yule unayehusiana nae. Lakini ni mmoja tu ndio utampenda kuliko wote.
 
Kwanza ungesoma post yangu yote ungeona niliposema wanawake wa namna hii nikimaanisha sio wote.

Pili, kuvumilia manyanyaso katika ndoa ni ujinga, period. Anyway you slice it, cut it, spin it, bado ni ujinga tu!

Tatu, kwenye mapenzi ya kweli hakuna kunyanyasana. Kuna kupendana. Mtu akupendaye hawezi kukunyanyasa. Kwa nini umnyanyase mtu umpendaye? Mtu umpendaye unamtendea kwa upendo na mapenzi ya dhati. Na sielewi inakuwaje mtu anampenda mtu amnyanyasae.

Nne, hivi kweli wewe ni mwanamke au unatuzuga tu hapa? Kama kweli wewe ni mwanamke basi sijui hata nikwambie nini maana unatetea kubaki kwenye abusive relationship kwa kisingizio cha penzi. Mapenzi gani ya kutesana hayo.

Tano, have a wonderful day!
1.Thanks Im having a wonderful evening so far...
2.Mimi ni mwanamke kweli---- no doubt about that and i enjoy being what I am.
3.Sitetei abusive relationship kama unavyodai-- ila nimeshare what is being said by many women who cannot get out of their abusive marriages!

Alamsiki!
 
Okay, basi hao wanawake wanahitaji high self-esteem transplant!!
 
This is the "what" part of the solution.. can u share the "how"?

I believe many would really like to get out of the nightmare they are in as quickly as possible.
 
...nakumbuka kuna mme wa cousin yetu alikuwa na tabia ya kumdunda cousin wetu,tukampa warning mara kibao bila kusikia,one day cousin wetu katupigia simu kapigwa,tulimfuata huko huko kwake na tulimpa kipigo ambacho hatasahau maishani mwake,tukabeba na cousin wetu...alikuja kumpata mke wake baada ya vikao kama 10 hivi na message akimpiga tuu atapata kibano alichopata mara 100 na jela ataiona,siku hizi kawa baba mzuri sana...dawa ukiona dada yako,cousin etc wanapigwa na wanaume zao dawa ni kuwageuzia kibao na kuwatandika kisawasawa na unahakikisha unavunja mkono au mguu!
 
Knowing you..... naamini jamaa mlimpa kisago cha uhakika....

Ila hata mimi hivyo hivyo.....kama dada au mtoto wangu wa kike anapigwa na mume wake....basi huyo mume itabidi a deal na Ngabu...kitu hatakifurahia kwa kweli....
 
...nakumbuka kuna mme wa cousin yetu alikuwa na tabia ya kumdunda cousin wetu,tukampa warning mara kibao bila kusikia,one day cousin wetu katupigia simu kapigwa,tulimfuata huko huko kwake na tulimpa kipigo ambacho hatasahau maishani mwake,tukabeba na cousin wetu...alikuja kumpata mke wake baada ya vikao kama 10 hivi na message akimpiga tuu atapata kibano alichopata mara 100 na jela ataiona,siku hizi kawa baba mzuri sana...dawa ukiona dada yako,cousin etc wanapigwa na wanaume zao dawa ni kuwageuzia kibao na kuwatandika kisawasawa na unahakikisha unavunja mkono au mguu!

Kumbuka pia kuwa manyanyaso si lazima vipigo.Kuna manyanyaso mengine ya kisaikolojia.. je hao nayo utaenda kumdunda huyo shemeji yenu?
 
Oh yeah...any kind of spousal abuse, be it physical, emotional, or psychological is a no-no. Kwangu mimi ni kibano tu. Unajua wakati mwingine emotional na psychological zinakuwa na madhara zaidi kwa mtu kuliko physical. So yeah kibano mtindo mmoja...all the way
 
This is the "what" part of the solution.. can u share the "how"?

I believe many would really like to get out of the nightmare they are in as quickly as possible.

Ok, how? Well, in many cases that is hard for I think self esteem is something that is inborn. You either have it or you don't. In other words hivyo ni ndivyo ulivyo. Sasa kama ni ndivyo ulivyo unaweza ukabadilika tu muda mfupi halafu baadaye una revert back ulivyo siku zote. Kwa sababu kama huna high self esteem, utakuwa unajiona uko duni na kwamba huwezi kumpata mwingine huyu akikuacha. Kwa hiyo unabaki kuvumilia tu ma BS yake....
 
Oh yeah...any kind of spousal abuse, be it physical, emotional, or psychological is a no-no. Kwangu mimi ni kibano tu. Unajua wakati mwingine emotional na psychological zinakuwa na madhara zaidi kwa mtu kuliko physical. So yeah kibano mtindo mmoja...all the way

Mara nyingi pschological/emotional abuse huja kwa njia nyingi- mtu anaweza kuamua hakuna communication hata wiki nzima, hakuna conjugal rights, na mengine mengi ambayo huyo binti au dadako hawezi kuja kukushtakia...hivi utajuaje kama anateseka kinamna hadi ukamrescue na kumfunza adabu huyo mume? Kipigo its so obvious
Navutika kuendelea kuuliza maswali mengi ila tutakuwa tunatoka nje ya mada kuu.Pengine itakuja thread muafaka.
 
Mimi nakataa katakata! Mwanamke kutoondoka kwenye abusive relationship na kutoa kisingizio cha watoto sijui nini ni ujinga mtupu. Yaani hiyo reasoning iko flawed kichizi. Yaani mtu uko radhi watoto wako waone, wakue wakiona jinsi unavyokuwa abused? Unajua ina madhara gani hiyo kwa watoto hasa wale walio katika formative years?

Astaghafururah!! Mnanishangaza kweli nyie. Anyways, kila mtu ana threshold zake za kuvumilia. Mimi threshold yangu iko chini sana. It's one and done. Hakuna cha second chances hapa.

Yawezekana tumekulia katika mazingira tofauti sana ndugu Nyani, lakini kama alivo sema mama kwa famiia za Kitanzania hasa za kule kwetu Kasulu/nanyamba/Irugwa/nakabale nikiwa namaana familia za wakulima na wafugaji wa kitz, Mama kuondoka akaacha wanawe, baba huo mke wa pili na maisha ya wale watoto husihia kuwa vijakazi wa mama anye olewa pale, na kwa vile PENZI HALIGAWANYIKI, baba huconcentrate kumpenda bibi mpya na watoto wapya kwa kisingizio cha kwamba ni wadogo.. at the end watoto walo achwa na mama yao ama huliwa na funza, akili hudamaa kwa kukosa uangalizi, hata shule hawafanyi vyema kwani huwa wamechoshwa na mikazi migumu wanayo twishwa na mama yao wa kambo matusi na fimbo juu.. at the end zaidi ya asilimia 80 ya watoto hao huwa wanaishia kuwa watoto wa mitaani ama huwa hawafanikiwi kwa sababu hizo.

Kwahiyo ndugu NI KUKOSA CHA KUWARUDISHIA MAMA ZETU WALIO VUMILIA MANYANYASO KWA AJILI YETU WATOTO TUWE KAMA TULIVYO! NA KAMWE SI UJINGA NDUGU, Inshalah Mungu wetu atawalipa!
 
Sasa muwapokee kama walivyo hao wenye high self esteem. Msiwabeze iwe wanaself esteem kutokana na mazingira au hata kama ni inborn.
 
Mara nyingi pschological/emotional abuse huja kwa njia nyingi- mtu anaweza kuamua hakuna communication hata wiki nzima, hakuna conjugal rights, na mengine mengi ambayo huyo binti au dadako hawezi kuja kukushtakia...hivi utajuaje kama anateseka kinamna hadi ukamrescue na kumfunza adabu huyo mume? Kipigo its so obvious
Navutika kuendelea kuuliza maswali mengi ila tutakuwa tunatoka nje ya mada kuu.Pengine itakuja thread muafaka.

Ni lazima utumie akili na busara zako na ujue wapi uchore mstari na wapi huo mstari utakuwa umevukwa. Psychologial an emotional ninayoizungumzia mimi ni ile iliyo wazi. Kama kumwita majina ya kudhalilisha, kumfokea fokea pasipo na sababu, kuwa rude kwake, na mambo mengine kama hayo. Hayo ya conjugal rights wala sio biashara yangu na wala sitaki kuyasikia.
 
Back
Top Bottom