Ifahamu ishara ya tandu, jongoo, sisimizi na popo nyumbani kwako!

Ifahamu ishara ya tandu, jongoo, sisimizi na popo nyumbani kwako!

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Usiku Kipindi cha mawingu ambako nyota na mbalamwezi hazionekani ni hatari sana kwa usalama wa maisha. Na pia sa nyingine huwa ni bahati sana katika maisha yako.

Umeshawahi kujiuliza ni kwanini unaota ndoto usiku unakImbizwa lakini huna mbio? Pia ushawahi jiuliza kwanini unaota unakula chakula usiku?

Kuna kitu kinaitwa sleep paralysis, ambayo kwa watu wengi tunaamini ni jinamizi linatukaba.

JONGOO:
Huyu umwonapo nyumbani basi katika ulimwengu wa kiroho huwa anaashiria amani na upendo vitatawala katika maisha yako.

SISIMIZI:
Hawa uwaonapo nyumbani kwako basi jua mikosi inakunyemelea na iko njiani either iwe kwako au kwa wanafamilia wako.

TANDU:
Huyu tandu kwanza ni mdudu wa kipekee, ukimchukua tandu ukatafuta majani ya mlonge longe, majani mabichi ya tumbaku na ndulele ukavichoma kwa pamoja yale majivu yake yachukue na uende nayo kwenye lolote tafuta na mafuta ya kondoo uchanganye na damu kidogo, unanyunyiza pale kwenye kaburi huku ukinena maneno unayotaka yampate mbaya wako. Basi nakuhakikishia miguu ya tandu yote kama iko mia baada ya siku mia tarajia taarifa.
Hivyo tandu umwonapo kwako jua kabisa anaakisi mabaya, na pia umezungukwa na marafiki wabaya na uko hatarini

POPO:
Popo umuonapo nyumbani mara kwa mara basi elewa hio ni ishara ya namna kifo chako kitavyokuwa! Naam utajuaje namna ya kifo chako, chukia samaki hawa perege wadogo wapake samli na unga wa muhogo kisha tupa sehemu ambapo wanajining'niza, alafu sema maneno haya leo ndotoni nataka nataka nione mwisho wa miamba ya dunia. Nenda kalale kisha utaota namna utavyokufa iwe ni kwa presha, ukimwi au ajali n.k

Hivyo umwonapo popo nyumbani kwako jua kifo kinakunyemelea.
N.B Nenda kayafanyie kazi haya maneno yangu utakuja kuamini na kuleta mrejesho

Sasa ni Saa saba za usiku nasikia bundi linalia hapa nje, ngoja nitoke nijue kulikoni!
 
Hiyo ya bundi hata mimi hapa naskia..
Ila ni kwa mbali sana
Basi nimeshalifukuza halikuja kwa shari ila kwa amani na kutuma ujumbe. Kama ni kweli na hapo kwako kuna bundi basi toka nje na mayai mawili yapasue kisha chukua nyonya la kuku na majivu weka chini ya gododo ulale unono. Kesho utaleta mrejesho.
 
Mmmh sitakua nimejiingiza kwenye shirki mkuu
 
Huu ndo upumbavu unaotufanya tubaguliwe sisi watu weusi.

Ndomana hata picha ya Shetan tunaaminishwa ni jitu jeusi.
NONSENSE
Ungejaribu kuulewa kilichopo na kufanya speculation zako ingesaidia zaidi. Kuliko kuja na conclusion moja kwa moja.
 
Duuh ebu fafanua kidogo maana naona kama mambo ya uganga hivi....
Mayai yana ule ute na kiini ambacho yanaakisi chimbuko lako ulipotokea, nyonya la kuku linaakisi mwelekeo wako tangu nyota yako ilipotengezwa katika sayari za mbali na majivu yanaakisi taswira ya mwili wako. Hivo mjumuiko huo hutumika kukuangamiza au kukuponya!
 
Duu sawa mkuu. Ngoja nijaribu kufanyia kazi tuone
Haya mambo haya daah
 
Back
Top Bottom