Ifahamu Kampuni ya Simu za Mkononi ya 'itel Mobile'

Ifahamu Kampuni ya Simu za Mkononi ya 'itel Mobile'

Pia ni SIMU ambayo ikiingia katika ndoo ya maji na ukiitoa ikiwa nzima Shukuru aliyetengeneza Ic zake siku hiyo hakuwa na kilevi kichwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari okiwira, simu yoyote ukiitumbukiza kwenye maji lazima ilete hitilafu ya kiutendaji ama kuharibika kabisa, isipokuwa tu simu ambayo ina kizuia maji ama 'water proof'. Hivyo tunakushauri kuwa makini ili simu yako isiingiwe maji. Asante.
 
honestly hii ni kampuni mbovu kuliko zote nilizowahi kutumia hapa tz.... ITEL haikuwa hata na hadhi ya kutengeneza simu za batani nyinyi mlifaa muwe mnatengeneza midoli ya watoto.
Hello Planett, tafadhali tujuze ni simu gani ya itel unatumia na inakuletea shida? Tuna huduma mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kutatua changamoto yako kwani tuna vituo vya huduma baada ya mauzo yaani 'after sales service', pia tuna huduma ya kubadilishiwa simu bure, kama simu yako imeleta hitilafu unaweza kubadilishiwa bure.
 
Pole Scars kama umewahi kukumbana na changamoto ya namna hiyo kwenye moja ya simu zetu. Tafadhali tujuze ni simu gani uliyokuletea hilo tatizo?
Series ya A karibia simu zote ni msiba

Hizo touch zina sensor ambayo haipo very sensitive halafu ngumu kama kioo cha landrover

It's Scars
 
Mimi ni muuzaji Smartphones itel mnazingua....ila
2160
2180
5081
5625
2150
2190
2090
2060
na viswaswadu vyote mmejitahidi....

Nawezaje kuwa sales guy wenu maana huyu dogo mlompa dhamana huku anazingua
Hongera kwa kuwa muuzaji wa simu zetu, Use brain Heriel, tafadhali upo mkoa gani? Pia tunaomba jina 'inbox' la huyo sales officer. Asante.
 
hilo ni zali tu nadhani hata wao wanatakua wanashagaa imekuaje haikusumbui

A series ndio msiba kabisa bora hiyo S
Hello Scars, tafadhali tujuze simu gani inakuletea hitilafu ili tukusaidie kwani tuna huduma nyingi za kuwasaidia wateja wetu hasa wale wanaoweza kukumbana na changamoto ya mifumo ya simu, tuna warantii miezi 13, tuna huduma ya baada ya mauzo yaani after sales service, tuna huduma ya kuwabadilishia simu bure kama itakuletea hitilafu yoyote. Ukituambia ni simu gani inakuletea hitilafu na ni hitilafu gani itakuwa rahisi kwetu kukusaidia wewe. Tupo kwaajili yako.
 
simu nzuri ila shida moja. Mi natumia itel kitochi inasumbua ukishaongea na simu kwenye kukata hadi nibonyeze mara mbili au tatu bila hivyo simu inaendelea kuwa hewani na hiki kitochi ni cha pili cha kwanza kilikuwa hivo hivo
Pole Naki 12 kwa hilo tatizo, Upo mkoa gani tafadhali ili tukuelekeze ofisi zetu kwaajili ya kupatiwa utatuzi wa hilo.
 
Mi hata nipewe buree itel siwezi kutumia labda niigawe tu angalau kidogo za batani ila smartphone ni big Noooooooo simu gani zinaganda ganda hovyo, kubonyeza wakat wa kuandika sms unatumia nguvu nyingi mpka kidole gumba kinakuwa na sugu na kuuma
Kiukwel itel siwezi tumia hata kwa dawa ya muarobaini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
duuuh huenda lakin mm binafs nshawah tumia hizi simu ni mbovu mno asee, labda tu nkuuliz kuwa ulishawah tumia simu tofauti na itel, mfano samsung au iphone?
Mbona mi Smartphone Yangu itel tena naitumia fresh kuna uwezekano wakawa na mapungufu lakini sio kwa kiwango hicho unachotaka kutuaminisha wana JF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini simu za itel kurepair inakuwa ngumu sana upande wa softwares?

Nimeletewa simu kama mbili Ku reset password hazi detect kwenye USB halafu ni ngumu kutambua kwamba chip zake ni MTK, SPD au intel

Sent from my TECNO WX3 using Tapatalk
 
Kwanini simu za itel kurepair inakuwa ngumu sana upande wa softwares?

Nimeletewa simu kama mbili Ku reset password hazi detect kwenye USB halafu ni ngumu kutambua kwamba chip zake ni MTK, SPD au intel

Sent from my TECNO WX3 using Tapatalk
Kumbe hizi simu ovyo,nisingepitia uzi huu kesho nilikuwa nakwenda kununua itel p 33..nilizamisha simu ya mtu ndani ya shimo la maji aisee!ilikuwa tecno f 2!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itel subcompany ya Tecno ,
Mpo vizuri ila hamfanyi haraka kwenye kuingiza mzigo sokono
 
Back
Top Bottom