Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Mahenge ni wilaya inayopatikana kusini mwa mkoa wa Morogoro na kabila la Wapogoro ndio wanapatikana huko. Ikiwa eneo la juu (Mlimani) na hali ya hewa ya ubaridi na mvua mvua.

Wilaya hii ina vivutio na siri nyingi mno, kihistoria,kiserikali na hata kidini (Je, umewahi kuisikia Wilaya hii na unapata picha gani juu yake?)

Vivutio; kwa upande wa vivutio kuna;
1. Kabila lenyewe linalopatikana huko (wapogoro) asili yao na lugha yao,tamaduni na style yao ya maisha. (kuoana ndugu mradi wasitike nababu mmoja) Uzuri wa wanawake wao wana miili yenye nguvu mno..

2. Ardhi na landscape yake, jinsi kulivyo na miinuko na misitu na vile ambavyo mji umechongwa.

3. Majengo ya mjerumani (boma) ambalo linatumika kama ofisi kuu za serikali (wilayani) na jengo la mkuu wa wilaya . Lakini pia majengo ya wamisionari (kanisa katoliki la tatu kwa ukubwa la tanzania lilojengwa kwa mawe tupu na mji wake ikijumuisha na shule zilojengwa na wao)

4. Misitu na miti pekee, na alama zilowekwa juu ya milima na misituni na wakoloni, hivyo ni baadhi.

Siri zilizoko;
1. Kuna madini ya aina mbali mbali yanayopatikana na kuchimbwa huko (rubi, spinal, greentomalin, uno, dhahabu na hata almasi)

2. Kutokana ni mji wa kikoloni, Mjerumani na Muingereza walikuwako huko hivyo alama zao juu ya milima na misitu zinamaana fulani, je ni ipi?

3. Kwanini wilaya hii licha ya kuwa na vyote hivi lakini bado imefungwa kimawasiliano ya barabara??? njia ni mbovu lakini pia haitoki inatoka kwa njia za mikato pekee.

4. Toka miaka viongozi wake wamekuwa wakinifaidisha wao, maajabu maendeleo yao pia yamekuwa hayaonekani sio kwa wao tu hata kwa ndugu zao (viongozi walowahi kutoka huko kwa uchache Late Amati liyumba aliwahi kuwa BOT, Late Mama Celina kombani alikuwa mbunge kabla CCM hawakumpa asante ya kumuweka mwanae kuwa mbunge baada ya mama yake Bw. Goodluck Mlinga ambae ameshindwa kuchukua jimbo mara baada ya miaka mitano kuisha .Sasa linashikiliwa na Bw. Almasi.

Je, kwanini hakuna maendeleo?

Je, kwanini viongozi wa huko ni kama wanaogopwa na wapogoro?

Je, kwanini mpaka leo barabara ni ya vumbi na kuna muda inakuwa mbaya na chafu kabisa?? kama unaogopa mlima kitonga basi usiendeshe kwenda Mahenge kuna mlima unaitwa ndororo ni hatari mno..

Kwa nini Viongozi wanaweza kaa msimu mzima wakaenda tembelea jimbo mara moja? especially walopita!!

Mimi nimeeleza vitu baadhi, waeza jazia vingine vile unafahamu kuhusu mji huu pia kuweza kualika kiongozi unae mjua aje ajibu baadhi ya hoja. Pia hata kueleza maswahibu au vituko ulivyowahi kutana navyo kwa mji huu maana na hata uchawi upo na wanatumia live.

cc: Goodlucky Mlinga
cc: Mkuu wilaya Mahenge Ulanga na mkurugenzi wake..
cc: Mbunge wa sasa Bw. Almasi
Ninachojua kuhusu haya maeneo Tajwa na Watu wake ni Washirikina, Wafitini, wana Roho Mbaya halafu ni Wanadiki wa Kutukuka.
 
Mengi waliweka Ulinzi wa majini wakayaroga majini yasiweze kuondoka maeneo hayo Ili kuficha mali hadi wao au vizazi vyao ndivyo vije kutoa.
Wao huja kama wawekezaji, wakulima, wafadhili,nk.
Hizo Imani tu Kwa mswahili mzungu na majini wapi na wapi
 
Huu uzi unanikumbusha utenzi darasa la tatu miaka ya 90's

Kwetu ukitoka mwenge
Huendelea mahenge
Ila mwakani upange
Kuja kututembelea

Mwenye beti zote za huu utenzi azishushe hapa nikumbuke enzi zangu za Elimu ya shule ya msingi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mahenge nilikaa huko vijijini kwa miaka miwili aisee nikajua kumbe sijawahi ishi kijijini kabisa.
Network ya simu ilikuwa hamna achilia mbali umeme. Tulikuwa tunakusanyika sehemu moja yenye network unakuta watu tumeinua mikono juu tunaongea na simu yaani hakuna Siri
Kwa Sasa wamekuja halotel mawasiliano kila mahali.
Pia umeme umeingia vijiji vingi Kuna maendeleo Fulani ukilinganish na zamani.
Maji yapo ya kutosha tena hakuna kulipa bill tena maji safi sana.
Kuhusu single mamaa wapogoro ni watu jeuri sana huwezi msumbua kwa hiyo wanawake wao wanajiamini na hawaogopi Maisha yaani ni maskini jeuri haswaa.
Wana majivuno na kwao utafikiri London yaani huwaambii kitu na kwao.
Mavuno yakianza watu wanatoka mjini kwenda vijijini sherehe Kama zote sangura kwa kwenda mbele. Wanakula walicholima wenyeji kikiisha hao mjini.
Barabara ndio ilikuwa tabu wakati wa mvua mpaka utoboe ifakara umekoma. Ila Kuna hela kwa mfanyabiashara Kuna fursa za kilimo sababu ya mvua za mara kwa mara.
Kuna watu wamejichimbia huko huwatoi wanapiga biashara balaa.
Wapogoro pia wapo Ikulu na TISS Nyerere aliwaweka hapo sana sijui nini kilifanya awaamini sana.
Japo ni sehemu mkoloni alikaa kwa muda mrefu hakuna chotara kama kaskazini ambapo unaona kabisa rangi ya mzungu.
Wapogoro wengi ni weusi sijui kwa nini mzugu hakutaka changanya rangi.
Dada zao warembo sana black beauty haswaa. Nitarudi one day. Wakashiina.
Unafahamu kwamba Obotte alifichwa kule Sali? Pogoro ni wasiri wakati huohuo ni wanafiki.
 
Unafahamu kwamba Obotte alifichwa kule Sali? Pogoro ni wasiri wakati huohuo ni wanafiki.
Wanafki kwenye nini ?

Kwanini miaka ya baada ya Uhuru Nyerere alipenda sana kuwatumia wapogoro pale usalama wa taifa ?
 
Upo mang'ula A au B
Dah! Hayo maeneo ya Mang'ula A, Mang'ula B, Mwaya, Mgudeni, Kisawasawa, Kiberege, Signal (Ziginali), Sonjo, Mkula, Kidatu, Nyandeo, Mkamba, Ruaha, Ifakara yote, Mahenge, Malinyi, Mngeta kurudi nyuma, nk. Nimepiga sana mishe huko miaka ya 1990's.
 
Uko ndo yanaenda magari yanaitwa KILAMSA?
Nlipanda siku moja na abiria wa uko tukashuka chalinze pale kuna lodge inaitwa MBUTA nkamla kimasihara tukasafiri kesho yake 😅
 
Back
Top Bottom