Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Upo sahihi kabsa kule pesa ndo ngumu ila chakula kipo cha kutosha….+nyama na samaki
 
Dah! Hayo maeneo ya Mang'ula A, Mang'ula B, Mwaya, Mgudeni, Kisawasawa, Kiberege, Signal (Ziginali), Sonjo, Mkula, Kidatu, Nyandeo, Mkamba, Ruaha, Ifakara yote, Mahenge, Malinyi, Mngeta kurudi nyuma, nk. Nimepiga sana mishe huko miaka ya 1990's.
Mkuu umesahau Kikwawila na Sagamaganga
 
Kitonga hamna mlima pale ule ni muinuko tu mlima gani unapanda umenyooka,hio ndororo unacheza na kona 24 na zote ni fupi fupi kupanda na kushuka,ila waliozoea kina kidinilo wanapanda na kushuka kwa 60 wanacheza na stopper sana.
Usie mzoefu lazima wakakuokote chini mita elf 3 Kama Sio 6 bondeni huko
 
Ndororo ya miaka ya 90 ilikuwa ni noma sana hasa nyakati za masika. Tulikuwa tunaupanda huo mlima kwa kutumia gari aina ya Landrover 109, huku tukikaa juu ya machuma na chini ikiwa imejaza mizigo ya kutosha.

Na hapo kulikuwa hakuna lami kwenye huo mlima. Yaani ni full utelezi.
 
Mmetoka mbali aisee angalau wameweka lami kuondoa utelezi
 
mbona sijaona sehemu umeitoa hiyo siri
 
Mpogoro akiwa anatuma salamu ukawasalimie utasikia "mpe shikamo yangu mama ,mpe shikamo baba,mpe shikamo kaka...." Ha ha

Ni watani zangu hao
 
Dah! Hayo maeneo ya Mang'ula A, Mang'ula B, Mwaya, Mgudeni, Kisawasawa, Kiberege, Signal (Ziginali), Sonjo, Mkula, Kidatu, Nyandeo, Mkamba, Ruaha, Ifakara yote, Mahenge, Malinyi, Mngeta kurudi nyuma, nk. Nimepiga sana mishe huko miaka ya 1990's.
Loh! Umepataja nyumbani moyo wote umenisisimka, mkula ndio nyumbani mkuu
 
Epanko ni Rubi yachimbwa.. ila kuna maeneo mengine ambayo nilibahatika kufika ... Lukande, ketaketa,mwaya na hata huko mbele kama una enda selous kunaitwa ibuyu
Shikamooo umekikumbusha miaka ya 2006 Lukande, ketaketa, mwaya, ipundi, mbuga palikuwa na barabara mbaya ajabu kipindi cha masika siku 3 ketaketa morogoro hapo ni crusier mpyaaa
 
Wale jamaa wa Kidinilo walipata wapi uzoefu wa ule Mlima ?
 
Mbona hujasema kwamba kuna Junior Seminari ya St Francis maarufu kama Kasita Seminari ambayo imezalisha vipanga mbalimbali wanaokimbiza kwenye sekta nyingi hapa nchini.

Kwiro secondary
Regunamundi
Kasita
St Agnes
 
[emoji23] Wale wamama wanaokuja kuuza vyakula jioni?! Haujaacha mtoto kule wewe?
😂😂😂 Sina uhakika japo nakumbuka kuna mama mmoja nilikuwa nakula free na kupiga shoo tu, nakumbuka nilimpaga ada ya shule nikasingizia kwa baba nimeibiwa🤣🤣🤣
 
Shikamooo umekikumbusha miaka ya 2006 Lukande, ketaketa, mwaya, ipundi, mbuga palikuwa na barabara mbaya ajabu kipindi cha masika siku 3 ketaketa morogoro hapo ni crusier mpyaaa
Kaka nimetoka ketaketa mwezi wa 12 mwaka 2024. Nakuhakikishia barabara ni mbaya Sana. Ilibidi tupaki gari pale ilonga niende na bodaboda adi ketaketa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…