Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Mahenge nilikaa huko vijijini kwa miaka miwili aisee nikajua kumbe sijawahi ishi kijijini kabisa.
Network ya simu ilikuwa hamna achilia mbali umeme. Tulikuwa tunakusanyika sehemu moja yenye network unakuta watu tumeinua mikono juu tunaongea na simu yaani hakuna Siri
Kwa Sasa wamekuja halotel mawasiliano kila mahali.
Pia umeme umeingia vijiji vingi Kuna maendeleo Fulani ukilinganish na zamani.
Maji yapo ya kutosha tena hakuna kulipa bill tena maji safi sana.
Kuhusu single mamaa wapogoro ni watu jeuri sana huwezi msumbua kwa hiyo wanawake wao wanajiamini na hawaogopi Maisha yaani ni maskini jeuri haswaa.
Wana majivuno na kwao utafikiri London yaani huwaambii kitu na kwao.
Mavuno yakianza watu wanatoka mjini kwenda vijijini sherehe Kama zote sangura kwa kwenda mbele. Wanakula walicholima wenyeji kikiisha hao mjini.
Barabara ndio ilikuwa tabu wakati wa mvua mpaka utoboe ifakara umekoma. Ila Kuna hela kwa mfanyabiashara Kuna fursa za kilimo sababu ya mvua za mara kwa mara.
Kuna watu wamejichimbia huko huwatoi wanapiga biashara balaa.
Wapogoro pia wapo Ikulu na TISS Nyerere aliwaweka hapo sana sijui nini kilifanya awaamini sana.
Japo ni sehemu mkoloni alikaa kwa muda mrefu hakuna chotara kama kaskazini ambapo unaona kabisa rangi ya mzungu.
Wapogoro wengi ni weusi sijui kwa nini mzugu hakutaka changanya rangi.
Dada zao warembo sana black beauty haswaa. Nitarudi one day. Wakashiina.
 
Wanakula nyama zote ni walafi wa nyama, iwe nyoka, kenge, ngedere, kenge, kwao wali ni sawa na chips mjini
Ila si Neema ya Mungu tu ndio maana tunachagua...ikitokea njaa ya kutosha hapa mbwa hawa watapungua tu automatically.
 
Nimekaa Bangui yalipo makazi ya Dc nikasoma Ukwama primary nyuma ya Jengo la Askofu
 
Hapo kwenye Alana za wakoloni zinaonyesha sehemu walikoficha Mali zao wakati wanaondoka nchini baada ya kututawala Kuna Vitu kama madini walificha na kuweka Alana zao ili baadae waje wavichukue
Hv huwa ni kweli hz story? Ni kweli wanakuja kuchua?wakichukua serikali na wananchi wanakua wapi? Hayo maeneo kn picha zake?
 
Mzungu anatambika mkuu??
Sijui kuhusu hao wanaokuja huku ila kikawaida tambiko (ritual) ni uchawi na uchawi upo kwenye mila zote duniani kinachotofautiana ni jinsi hayo matambiko yanavyofanyika.

Kwa wenzetu wazungu, waarabu, wachina, waisrael wana husudu sana elimu hizo na unakuta kabisa kuna familia au kabila fulani linafanya hayo mambo sana tu.

Fuatilia kuhusiana na "wiccans" utaelewa ninachomanisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…