Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Miaka ya nyuma usafiri ulikuwa changamoto sana huko. Gari nyingi zilikuwa ni lori aina ya fuso, canter, landrover 109, na pickups.

Hivyo ili mpandishe huko, hizo gari lazima zijaze mzigo wa kutosha! Halafu abiria ndiyo mnakaa juu ya mabomba.

Na usafiri huo huo wa malori, ulikuwa pia ni common kwa safari za Ifakara - Mbingu - Mngeta - Chita mpaka Mlimba. Sijui kwa miaka ya sasa. Huenda basi aina ya Tata zikawa nyingi zaidi.
Huko ni mwendo wa Noah Ifakara - Chita
 
Miaka ya nyuma usafiri ulikuwa changamoto sana huko. Gari nyingi zilikuwa ni lori aina ya fuso, canter, landrover 109, na pickups.

Hivyo ili mpandishe huko, hizo gari lazima zijaze mzigo wa kutosha! Halafu abiria ndiyo mnakaa juu ya mabomba.

Na usafiri huo huo wa malori, ulikuwa pia ni common kwa safari za Ifakara - Mbingu - Mngeta - Chita mpaka Mlimba. Sijui kwa miaka ya sasa. Huenda basi aina ya Tata zikawa nyingi zaidi.
Nimepanda sana fuso maana mabasi yalikuwa hayapandi ule mlima kipindi hicho, sijui ile barabara imeshatengenezwa siku hizi!?
 
Mahenge ni wilaya inayopatikana kusini mwa mkoa wa Morogoro na kabila la Wapogoro ndio wanapatikana huko. Ikiwa eneo la juu (Mlimani) na hali ya hewa ya ubaridi na mvua mvua.

Wilaya hii ina vivutio na siri nyingi mno, kihistoria,kiserikali na hata kidini (Je, umewahi kuisikia Wilaya hii na unapata picha gani juu yake?)

Vivutio; kwa upande wa vivutio kuna;
1. Kabila lenyewe linalopatikana huko (wapogoro) asili yao na lugha yao,tamaduni na style yao ya maisha. (kuoana ndugu mradi wasitike nababu mmoja) Uzuri wa wanawake wao wana miili yenye nguvu mno..

2. Ardhi na landscape yake, jinsi kulivyo na miinuko na misitu na vile ambavyo mji umechongwa.

3. Majengo ya mjerumani (boma) ambalo linatumika kama ofisi kuu za serikali (wilayani) na jengo la mkuu wa wilaya . Lakini pia majengo ya wamisionari (kanisa katoliki la tatu kwa ukubwa la tanzania lilojengwa kwa mawe tupu na mji wake ikijumuisha na shule zilojengwa na wao)

4. Misitu na miti pekee, na alama zilowekwa juu ya milima na misituni na wakoloni, hivyo ni baadhi.

Siri zilizoko;
1. Kuna madini ya aina mbali mbali yanayopatikana na kuchimbwa huko (rubi, spinal, greentomalin, uno, dhahabu na hata almasi)

2. Kutokana ni mji wa kikoloni, Mjerumani na Muingereza walikuwako huko hivyo alama zao juu ya milima na misitu zinamaana fulani, je ni ipi?

3. Kwanini wilaya hii licha ya kuwa na vyote hivi lakini bado imefungwa kimawasiliano ya barabara??? njia ni mbovu lakini pia haitoki inatoka kwa njia za mikato pekee.

4. Toka miaka viongozi wake wamekuwa wakinifaidisha wao, maajabu maendeleo yao pia yamekuwa hayaonekani sio kwa wao tu hata kwa ndugu zao (viongozi walowahi kutoka huko kwa uchache Late Amati liyumba aliwahi kuwa BOT, Late Mama Celina kombani alikuwa mbunge kabla CCM hawakumpa asante ya kumuweka mwanae kuwa mbunge baada ya mama yake Bw. Goodluck Mlinga ambae ameshindwa kuchukua jimbo mara baada ya miaka mitano kuisha .Sasa linashikiliwa na Bw. Almasi.

Je, kwanini hakuna maendeleo?

Je, kwanini viongozi wa huko ni kama wanaogopwa na wapogoro?

Je, kwanini mpaka leo barabara ni ya vumbi na kuna muda inakuwa mbaya na chafu kabisa?? kama unaogopa mlima kitonga basi usiendeshe kwenda Mahenge kuna mlima unaitwa ndororo ni hatari mno..

Kwa nini Viongozi wanaweza kaa msimu mzima wakaenda tembelea jimbo mara moja? especially walopita!!

Mimi nimeeleza vitu baadhi, waeza jazia vingine vile unafahamu kuhusu mji huu pia kuweza kualika kiongozi unae mjua aje ajibu baadhi ya hoja. Pia hata kueleza maswahibu au vituko ulivyowahi kutana navyo kwa mji huu maana na hata uchawi upo na wanatumia live.

cc: Goodlucky Mlinga
cc: Mkuu wilaya Mahenge Ulanga na mkurugenzi wake..
cc: Mbunge wa sasa Bw. Almasi
Umeandika: "Mahenge ni wilaya inayopatikana kusini mwa mkoa wa Morogoro..."

Hapo kuna makosa ya utangulizi na utambulisho. Kwanza, Mahenge si wilaya bali ni makao makuu ya wilaya iitwayo Ulanga. Pili, haiko kusini mwa mkoa wa Morogoro bali iko "Kusini-Magharibi".

Huko kwa wapogolo ni asili ya sisi Wanyakyusa, wanatuita watoto wao hadi leo!
 
Hapo kwenye Alana za wakoloni zinaonyesha sehemu walikoficha Mali zao wakati wanaondoka nchini baada ya kututawala Kuna Vitu kama madini walificha na kuweka Alana zao ili baadae waje wavichukue


UONGO.
 
Back
Top Bottom