Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Miaka ya nyuma usafiri ulikuwa changamoto sana huko. Gari nyingi zilikuwa ni lori aina ya fuso, canter, landrover 109, na pickups.

Hivyo ili mpandishe huko, hizo gari lazima zijaze mzigo wa kutosha! Halafu abiria ndiyo mnakaa juu ya mabomba.

Na usafiri huo huo wa malori, ulikuwa pia ni common kwa safari za Ifakara - Mbingu - Mngeta - Chita mpaka Mlimba. Sijui kwa miaka ya sasa. Huenda basi aina ya Tata zikawa nyingi zaidi.
Bila kusahau njia ya Malinyi, Mtimbira
 
sasa kuna sehemu ngoja niwape kodi,, inaitwa kwa dit rich, kuna sehemu ukiingia ndani kama uko dar panaitwa club exchange ,kuna hiyo river side, kuna stone pub, na ku moja ipo panaitwa safari road nimesahau jina .. hutajutia kama una taka mambo yale na lile baridi kule si mchezo... wapogoro wana mvuto si masihara..
Hapo kwenye mvuto umetupiga na kitu kizito mkuu
 
Umeandika: "Mahenge ni wilaya inayopatikana kusini mwa mkoa wa Morogoro..."

Hapo kuna makosa ya utangulizi na utambulisho. Kwanza, Mahenge si wilaya bali ni makao makuu ya wilaya iitwayo Ulanga. Pili, haiko kusini mwa mkoa wa Morogoro bali iko "Kusini-Magharibi".

Huko kwa wapogolo ni asili ya sisi Wanyakyusa, wanatuita watoto wao hadi leo!
Kumbe ndio maana wapogoro wana tabia ya kujisikia kama wanyakyusa.
 
Mahenge nilikaa huko vijijini kwa miaka miwili aisee nikajua kumbe sijawahi ishi kijijini kabisa.
Network ya simu ilikuwa hamna achilia mbali umeme. Tulikuwa tunakusanyika sehemu moja yenye network unakuta watu tumeinua mikono juu tunaongea na simu yaani hakuna Siri
Kwa Sasa wamekuja halotel mawasiliano kila mahali.
Pia umeme umeingia vijiji vingi Kuna maendeleo Fulani ukilinganish na zamani.
Maji yapo ya kutosha tena hakuna kulipa bill tena maji safi sana.
Kuhusu single mamaa wapogoro ni watu jeuri sana huwezi msumbua kwa hiyo wanawake wao wanajiamini na hawaogopi Maisha yaani ni maskini jeuri haswaa.
Wana majivuno na kwao utafikiri London yaani huwaambii kitu na kwao.
Mavuno yakianza watu wanatoka mjini kwenda vijijini sherehe Kama zote sangura kwa kwenda mbele. Wanakula walicholima wenyeji kikiisha hao mjini.
Barabara ndio ilikuwa tabu wakati wa mvua mpaka utoboe ifakara umekoma. Ila Kuna hela kwa mfanyabiashara Kuna fursa za kilimo sababu ya mvua za mara kwa mara.
Kuna watu wamejichimbia huko huwatoi wanapiga biashara balaa.
Wapogoro pia wapo Ikulu na TISS Nyerere aliwaweka hapo sana sijui nini kilifanya awaamini sana.
Japo ni sehemu mkoloni alikaa kwa muda mrefu hakuna chotara kama kaskazini ambapo unaona kabisa rangi ya mzungu.
Wapogoro wengi ni weusi sijui kwa nini mzugu hakutaka changanya rangi.
Dada zao warembo sana black beauty haswaa. Nitarudi one day. Wakashiina.
Wakashina mtua, umeupiga mwingi sana kwenye brief explanation yako.
 
Mahenge ni wilaya inayopatikana kusini mwa mkoa wa Morogoro na kabila la Wapogoro ndio wanapatikana huko. Ikiwa eneo la juu (Mlimani) na hali ya hewa ya ubaridi na mvua mvua.

Wilaya hii ina vivutio na siri nyingi mno, kihistoria,kiserikali na hata kidini (Je, umewahi kuisikia Wilaya hii na unapata picha gani juu yake?)

Vivutio; kwa upande wa vivutio kuna;
1. Kabila lenyewe linalopatikana huko (wapogoro) asili yao na lugha yao,tamaduni na style yao ya maisha. (kuoana ndugu mradi wasitike nababu mmoja) Uzuri wa wanawake wao wana miili yenye nguvu mno..

2. Ardhi na landscape yake, jinsi kulivyo na miinuko na misitu na vile ambavyo mji umechongwa.

3. Majengo ya mjerumani (boma) ambalo linatumika kama ofisi kuu za serikali (wilayani) na jengo la mkuu wa wilaya . Lakini pia majengo ya wamisionari (kanisa katoliki la tatu kwa ukubwa la tanzania lilojengwa kwa mawe tupu na mji wake ikijumuisha na shule zilojengwa na wao)

4. Misitu na miti pekee, na alama zilowekwa juu ya milima na misituni na wakoloni, hivyo ni baadhi.

Siri zilizoko;
1. Kuna madini ya aina mbali mbali yanayopatikana na kuchimbwa huko (rubi, spinal, greentomalin, uno, dhahabu na hata almasi)

2. Kutokana ni mji wa kikoloni, Mjerumani na Muingereza walikuwako huko hivyo alama zao juu ya milima na misitu zinamaana fulani, je ni ipi?

3. Kwanini wilaya hii licha ya kuwa na vyote hivi lakini bado imefungwa kimawasiliano ya barabara??? njia ni mbovu lakini pia haitoki inatoka kwa njia za mikato pekee.

4. Toka miaka viongozi wake wamekuwa wakinifaidisha wao, maajabu maendeleo yao pia yamekuwa hayaonekani sio kwa wao tu hata kwa ndugu zao (viongozi walowahi kutoka huko kwa uchache Late Amati liyumba aliwahi kuwa BOT, Late Mama Celina kombani alikuwa mbunge kabla CCM hawakumpa asante ya kumuweka mwanae kuwa mbunge baada ya mama yake Bw. Goodluck Mlinga ambae ameshindwa kuchukua jimbo mara baada ya miaka mitano kuisha .Sasa linashikiliwa na Bw. Almasi.

Je, kwanini hakuna maendeleo?

Je, kwanini viongozi wa huko ni kama wanaogopwa na wapogoro?

Je, kwanini mpaka leo barabara ni ya vumbi na kuna muda inakuwa mbaya na chafu kabisa?? kama unaogopa mlima kitonga basi usiendeshe kwenda Mahenge kuna mlima unaitwa ndororo ni hatari mno..

Kwa nini Viongozi wanaweza kaa msimu mzima wakaenda tembelea jimbo mara moja? especially walopita!!

Mimi nimeeleza vitu baadhi, waeza jazia vingine vile unafahamu kuhusu mji huu pia kuweza kualika kiongozi unae mjua aje ajibu baadhi ya hoja. Pia hata kueleza maswahibu au vituko ulivyowahi kutana navyo kwa mji huu maana na hata uchawi upo na wanatumia live.

cc: Goodlucky Mlinga
cc: Mkuu wilaya Mahenge Ulanga na mkurugenzi wake..
cc: Mbunge wa sasa Bw. Almasi
Kwa kumbukumbu zangu Mahenge sio wilaya ila ni mji katika wilaya ya Ulanga na mkuu wa wilaya ni Ngollo Malenya!
 
Naona lawama zipo Kwa viongozi, umeacha kuzungumzia uvivu wa vijana wa huko wanajua kuzalisha tuu, halafu wanakimbia, asilimia kubwa Kuna singo Maza wengi wenye umri mdogo, wanaofaidika hapo mahenge ni wageni Wakat wenyeji wamelala
Bado lawama haziwezi kuacha kutupiwa Kwa viongozi, serikali Ina wajibu wa kupeleka elimu husika Kwa wananchi na kuwaeleza umuhimu wa kujikita ktk utafutaji na kujikomboa kutoka ktk umasikini wa kiuchumi na kifikira he hayo yanafanyika na kama yanafanyika ni Kwa ukubwa upi

Kuna Jamii nyingine zimejikita ktk kuyafanya hayo unayo yaeleza Kwa sababu ni Jamii ambazo bado zipo ktk ulimwengu Giza wa kiutambuzi ila Endapo wakifikishiwa elimu kwa kina Kwa namna Moja au nyingine lazima watajitoa ktk hicho kivuli Cha ujinga wa matendo Yao
 
Barabara ya kwenda Mahenge itakuwa bora hivi karibuni kuna mradi mkubwa sana wa kuchimba Graphite unakwenda kule Mahenge katika vijiji vya Mdindo, Kisewe na kuna barabara itajengwa kuja kutokea kijiji cha Chikuti pale!
Siasa tu, utekelezaji sifuri.
 
Back
Top Bottom