Ifahamu mikoa 10 yenye maghorofa mengi Tanzania

Nani kakuambia Mbeya Ni kubwa kuliko Arusha?
 
Magorofa ya mikoa kama Dar, Tanga, Arusha Dodoma, Singida mengi pia sio ya watu binafsi yaani NHC walijenga sana huko hizo gorofa, fikiria sehemu kama mafinga wakazi wanavopambana kujenga wao wenyewe nyumba za kuishi, Mikoa kama Mwanza kwa miaka 20 ijayo itakua haishikiki maana wanapambana sana kujenga mji wao na wana project nyingi binafsi
 
Ukijumlisha katavi na Rukwa wote hawafikii hata ghorofa za kigoma hapo naona kuna tatizo wakati katavi na rukwa kibiashara naona zinakimbia sana
Acha masihala mkuu,wewe unaweza Jenga majengo sehemu ambayo haina biashara kwa hoja yako unamaanisha Kigoma?

Mkoa wa Kigoma una Kasulu na Kigoma Mjini usisahau Hilo Ni Miji mikubwa hiyo ,Rukwa na Katavi Ni hapo Mjini tuu Yaani Sumbawanga na Mpanda.
 
Yaani ukijumlisha majengo ya ghorofa ya Mikoa yote Tanzania bado haifikii kwa Dar..

Aisee Dar ndio Tanzania asikwambie mtu.
Kuna wakati nilikwenda kuangalia nchi mikoa ya kusini.

Sasa nilifika sehemu moja Rufiji inaitwa Muhoro. Nikakutana na msela mmoja akanitembeza sana.

Nikamualika akija Dar anitafute.

Yule mchizi akaja Dar. Nukamuelekeza akaja mpaka Upanga ananiambia ni mara yake ya kwanza kupanda nyumba ya ghorofa.

Mtu mzima kabisa hajawahi kupanda ghorofa.

Nikasema kwamba hapa Dar tuna maisha tofauti sana na mikoani huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…