Usiwe na wasiwasi mkuu, hivi vyote nilivyoviandika sikuvitoa kichwani kwangu ila nimevisoma sehemu na kujiridhisha. Lakini kwa vingi ya nilivyoviandika nilivisoma siku nyingi sana kiasi hiki kipande "cha kuwa miaka 62 ya giza na miaka 62 ya mwanga" nimekisahau nilikisoma wapi .... na nikikipata nitakiweka hapa.(mara nyingi naongea na ushahidi) Lakini kwasasa kwa vile sijakipata basi elewa walivyorekebisha waungwa hapo juu. Ila nakupa nadharia moja kwa hapa duniani kuna baadhi ya inchi kuupata mwanga wa jua ni nadra sana na hii iko ya 3 kutoka jua na ni ndogo sana tena sana kwa Jupiter (kumbuka giza ni kukosa nuru na mchana ni kupata mwanga) Je, inashindikana vipi kwa dude kama jupiter ambalo dunia ni x 1,000+ na iko mbali zaidi ya dunia kutoka kwenye jua ????