Ifahamu Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Majukumu yake

Ifahamu Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Majukumu yake

Hawa jamaa hakuna haja yakuwapongeza maana hua ni mbwembwe tuu mwanzoni baadae hakuna kitu, kwanza wana poor customer service kama huamini fuatilia huu uzi uwone comment walizojibu na matatizo walio tatua.. ukija kwenye ajira portal kulee ndio kabisa hawajui walifanyalo na bado wanashindwa kujua dunia iko 2022 wao wana operate manual na mifumo yao ya 1990...
 
Ni kweli tujue msimu mpya wa kulipa Kodi za nyumba unaingia tusije kulipa baada ya siku mbili placement inatoka na umo umepelekwa mkoa mwingine,tusaidieni kwa hili jobless
hili swala linaniumiza kichwa sana
 
Samahani wakuu nashidwa kuswitch account kwenda ya Ajira so maswali yenu yote nitayajibu badae nikifanikiwa nawasilana na uongozi wa jf kwanza(jokes)[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hahaha!
 
Hapa tutapata changamoto ya kutojibiwa kama ilivyo changamoto ya ucheleweshaji wa Placement

Namimi nimeanza kuhofia isijekuwa ni move ya kisiasa, kuna siku utawasikia Utumishi wakisema, “TUNAMSHUKURU MUHESHIMIWA RAIS KWA ZIARA ZAKE ZA KILA SIKU, AMA HAKIKA ZINATUFUNDISHA MENGI, NASISI ILI KUTANUA WIGO WA KUWAFIKIA JOBLESS TUMEFUNGUA AKAUNTI KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII, IKIWEMO JAMII FORUMS”.

Naamini huyu aliyepewa dhamana ya kuendesha hii akaunti ataitendea haki sio tu kama mfanyakazi bali kama binadamu na mtanzania anayejua madhila mnayopitia watafuta ajira.
 
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 29(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 (iliyorejewa 2019) kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma na kuanzishwa rasmi tarehe 1 Machi, 2010.

Majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni;
  • Kutafuta wataalamu wenye ujuzi maalum na kuandaa mfumo wa kuhifadhi taarifa (kanzidata) za wataalamu hao ili kurahisisha utaratibu wa kuwaajiri pindi wanapohitajika;
  • Kuandaa orodha ya wahitimu wa Vyuo Vikuu na wataalamu wenye weledi kwa madhumuni ya kurahisisha rejea na ujazaji wa nafasi wazi za ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma;
  • Kuhusisha wataalamu maalum kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji;
  • Kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na ajira; na
  • Kufanya kazi nyingine yoyote inayoendana na majukumu yake kadri itakavyoelekezwa na Waziri.
Jamaa wako vizuri mdogo wangu alipata kazi TMDA bila zengwe hawa ni haki bin hak
 
Nyie wasumbufu.
Unafungua account unatumiwa ujumbe kuwa tumetuma link kwenye email yako ya ku activate. Ukienda kwenye email hukuti email. Ile email huwezi kuitumia tena kufungua account mpya, na kuomba wakutumie tena email hakuna option.
Mchezo huu unaweza kwa siku ukafungua email 5 na zote zikagoma.
Mjitahidi katika jambo hili
 
Ukiitwa kwenye interview na utumishi hakikisha unabeba document zote ikiwemo vyeti vya ubatizo na kipaimara Yani ukikosa kiambatanisho kimoja tu unatemwa na hapo kumbuka umetoka mkoa mmoja kwenda mwingine kufatilia mchongo [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom