Mungu aliuliwa na NYONGO YA mamba afu akapigiliwa Misumari ya kenchi then akabanikwa juani kwa mbao zilizo kaa kama jumlisha then wakamchoma na spear of destiny
Zile damu zilizotoka zkaja kusafisha dhambizetu..
MUNGU ALIEUMBA ULIMWENGU HAYUPO HIVI AISEE.
mnamtafsiri vibaya na ndo mana
Kiranga anasema hayo aliyoyasema.
Kiranga ingia Google playstore andika quran swahili then download
Afu tafuta (ndani) yaqurani suratul naaba..kwa akili ya kujaji vitu ulionayo utaondoka na kitu.
Sihitaji Quran ya Google Store.
Kama umeniita hapa, ukifikiri nitapinga Wakristo tu, umekosea sana na hunielewi.
Nina "The Meaning of The Holy Quran" ambacho ni Quran nzima, Kiarabu na Kiingereza, na maelezo ya tafsiri yaliyohaririwa na Abdullah Yusuf Ali.
Kwa hivyo kunifikiria sijaijua Quran na nianze ku download Google Store leo, unaniweka chini sana.
Quran nayo ina ujinga ule ule tu.
Katika aya za mwanzoni tu unaambiwa kwamba.
1. Kuna watu wabishi sana kuhusu dini, waumini msibishane nao.
2. Msibishane nao kwa kuwa, Allah mwenyewe amefanya mioyo yao kuwa mizito kumuamini, ameziba macho yao na masikio yao.
3. Watu hawa, kwa kuwa wamezibwa mioyo, macho na masikio wasimjue Allah, hawatamjua Allah.
4. Kisha, Allah atawahukumu vikali sana hawa watu, kwa sababu hawajamjua, wakati hawajamjua kwa sababu yeye mwenyewe kawaziba mioyo, macho na masikio wasimjue.
Hivi mtu na akili zake akisoma hizi habari za Allah anakubali kabisa huyo Allah yupo, na ni Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?