Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
Muda mchache uliopita nimesikia mambo ambayo yamenistaajabisha sana. Nilienda salun kwa ajili ya kunyoa, kwavile palikuwa na foleni, nikawa nimekaa kwenye benchi nje, nachezea simu huku nasubiria zamu yangu ifike. Pale pembeni palikuwa na salun ya kike, yaliyokuwa yanazungumzwa humo ndio yaliniacha mdomo wazi.
Walikuwa wanapiga story za waganga na kuelekezana dawa.
Maongezi yao sasa "Shoga wala sio ngumu, ww unajifukiza dawa huku unanuiza tu, tena hakikisha unapata mlipu, huo mlipu ndio kiboko, unamlipua mlengwa wako popote alipo,chochote utakachoomba, lazima akutimizie"
Walitaja na dawa zingine kama 3 au 4 hivi, ambazo sikuzisikia vizuri.
Kiuhalisia, wanaume wengi hatuna Kinga yoyote, kwa Mungu hatupo, kwa waganga hatupo, hizi dawa kama zinafanyakazi kweli siwatatupa ukichaa? Imagine mabinti watatu kila mmoja aamue kukulipua??
Dah, kumbe ndio wamedhamiria kiasi hiki??