Ifike hatua, wanawake muwe na huruma dhidi yetu wanaume

Ifike hatua, wanawake muwe na huruma dhidi yetu wanaume

Mlipuliwe tuu maana hamsikii, mtu una mke kutwa kucha kuneng'eneka na michepuko. TULIENI KHAAAA 😔
Mlituona wapi?
Michepuko yenyewe si ndio ninyi pia?šŸ˜†
 
Wale wasumbufu sumbufu...michepuko kila kona..kudanganya danganya wadada kumi kidogo...hao lazima walipuke...
 
Eeh tulieni dawa iwaingie, mngechagua wenye uzuri wa kawaida yasingewakuta, mnachagua akina sanchoka , wacha wawanyooshe.
Kama una uzuri wa kawaida ni DM tufanye jambo.
 
Huu ni ukweli unaoumiza ,ila ni kukomaa tu. Japo kama Mwanaume unaweza ukawa ushakufa at age ndogo lkn ukasubiria miaka mingi kuja kuzikwa.
Lakin majanga meng mnayachuma wenyewe jamani. Hivi mngetulia mngeyapata wapi haya majanga?? Hata kama ni mechi za nje chezeni mara moja moja ikiwabidi...lakin mmegeuza sheria. Mmepafanya ibada huko nje. Na mbaya zaidi mnajisifu wazi wazi. Kazi mnayo..
 
Dawa ni kuwakataa tu,tafuta mke asiyekuwa na mambo mengi form four au six hata la saba owa muhimu msikilizane ndani ya nyumba.

Mke anayekusikiliza hawezi kukuendea kwa waganga kutafuta namna ya kula vyako zaidi atakuwa anakushauri cha kufanya maisha yenu na watoto yasogee hata akidokoa ni kwa ajili ya watoto siyo vinginevyo.
 
Muda mchache uliopita nimesikia mambo ambayo yamenistaajabisha sana. Nilienda salun kwa ajili ya kunyoa, kwavile palikuwa na foleni, nikawa nimekaa kwenye benchi nje, nachezea simu huku nasubiria zamu yangu ifike. Pale pembeni palikuwa na salun ya kike, yaliyokuwa yanazungumzwa humo ndio yaliniacha mdomo wazi.

Walikuwa wanapiga story za waganga na kuelekezana dawa.

Maongezi yao sasa "Shoga wala sio ngumu, ww unajifukiza dawa huku unanuiza tu, tena hakikisha unapata mlipu, huo mlipu ndio kiboko, unamlipua mlengwa wako popote alipo,chochote utakachoomba, lazima akutimizie"

Walitaja na dawa zingine kama 3 au 4 hivi, ambazo sikuzisikia vizuri.

Kiuhalisia, wanaume wengi hatuna Kinga yoyote, kwa Mungu hatupo, kwa waganga hatupo, hizi dawa kama zinafanyakazi kweli siwatatupa ukichaa? Imagine mabinti watatu kila mmoja aamue kukulipua??

Dah, kumbe ndio wamedhamiria kiasi hiki??
Hio huruma unayo waomba kaka sahau tu, tuendelee tu kuishi nao ki akili. Wanawake wana huruma kwa watoto wao tu. OVER!
 
Dawa ni kuwakataa tu,tafuta mke asiyekuwa na mambo mengi form four au six owa muhimu msikilizane ndani ya nyumba.

Mke anayekusikiliza hawezi kukuendea kwa waganga kutafuta namna ya kula vyako zaidi atakuwa anakushauri cha kufanya maisha yenu na watoto yasogee hata akidokoa ni kwa ajili ya watoto siyo vinginevyo.
Mke hafanyi haya, shida ni hawa tunaokutana nao barabarani,michepuko
 
Lakin majanga meng mnayachuma wenyewe jamani. Hivi mngetulia mngeyapata wapi haya majanga?? Hata kama ni mechi za nje chezeni mara moja moja ikiwabidi...lakin mmegeuza sheria. Mmepafanya ibada huko nje. Na mbaya zaidi mnajisifu wazi wazi. Kazi mnayo..
Tunatulia, ila dawa zenu ndio hazitutulizi. Zinazidi kutupeperusha, mnatulipua šŸ˜…šŸ˜…
 
Ni vile tu wanaume tunaponzwa na tamaa, kuepusha yote hayo tafta pisi yako moja kali itunze piga show ya maana hizi mambo za kurogwa ni outcomes ya uzinzi
 
Back
Top Bottom