Ifike hatua, wanawake muwe na huruma dhidi yetu wanaume

Ifike hatua, wanawake muwe na huruma dhidi yetu wanaume

Eeh tulieni dawa iwaingie, mngechagua wenye uzuri wa kawaida yasingewakuta, mnachagua akina sanchoka , wacha wawanyooshe.
 
Imagine unao watano halafu wote wanakulipua akili yako na moyo wako
Yaani usipopata wazimu basi lazima upate shinikizo la damu ufeee🤣🤣🤣
Ndio maana idadi ya wanaume wanaokufa per day ni wengi sana. Tunalipuliwa kila siku
 
Wachana na hiyo habari buana
Raha ya mume akupende akiwa na akili zake
Ukianza hii shughuli unakua kama unaishi na robot ndani😂😂😂
Asante, endelea kuwapa darasa watuache
 
Muda mchache uliopita nimesikia mambo ambayo yamenistaajabisha sana. Nilienda salun kwa ajili ya kunyoa, kwavile palikuwa na foleni, nikawa nimekaa kwenye benchi nje, nachezea simu huku nasubiria zamu yangu ifike. Pale pembeni palikuwa na salun ya kike, yaliyokuwa yanazungumzwa humo ndio yaliniacha mdomo wazi.

Walikuwa wanapiga story za waganga na kuelekezana dawa.

Maongezi yao sasa "Shoga wala sio ngumu, ww unajifukiza dawa huku unanuiza tu, tena hakikisha unapata mlipu, huo mlipu ndio kiboko, unamlipua mlengwa wako popote alipo,chochote utakachoomba, lazima akutimizie"

Walitaja na dawa zingine kama 3 au 4 hivi, ambazo sikuzisikia vizuri.

Kiuhalisia, wanaume wengi hatuna Kinga yoyote, kwa Mungu hatupo, kwa waganga hatupo, hizi dawa kama zinafanyakazi kweli siwatatupa ukichaa? Imagine mabinti watatu kila mmoja aamue kukulipua??

Dah, kumbe ndio wamedhamiria kiasi hiki??
Najua hio tena ya kibatari hio ni noma sana hata kama unauguza popote ulipo unawasha gari usiku huo huo, hatari sana huo mlipu ni noma sana
 
Punguzeni idadi ya wanawake mtalipuliwa mfeeee
🤣🤣🤣🤣🤣
Wabaki na wake zao mazaa...watulie. Wangetulia haya yote wangeyapata wapi? Wengne wakaoa na kuoa..jua likazama wakarudi mikono mitupu kwa wake zao. Bahati wake wana hekima na huruma wakawasamehe. Pesa wanazozipata zinawazuzua wanatamani kuonja...too bad wanaangukia kwa mlipu..wanalipuliwa. wanadhani ni sifa kumbe..wanafukuza upepo.

Mwisho wa siku mtoto akimpa hela mama yake wanalalamika wanadharauliwa kumbe enzi za ujana na nguvu waliwekeza kwa kina mlipu...solution wabaki na wake zao..kila mtu yu na tamaa..na uzinzi unaondoa ufahamu na akili. Watakuwa watumwa wa ngono mpaka lini. Ngono kila siku ina mambo mapya. Hutamaliza starehe zote dunia hii.

Fanya starehe uchoke..ukishaingia kwenye ndoa tulia. Hawaelewi wanaona wanapangiwa maisha wanataka uhuru. Wataacha kulipuliwa....sad...
 
Eeh tulieni dawa iwaingie, mngechagua wenye uzuri wa kawaida yasingewakuta, mnachagua akina sanchoka , wacha wawanyooshe.
Wote wanaroga tu, sio Waziri sio wabaya, sio wa wastani, wote sawa
 
Najua hio tena ya kibatari hio ni noma sana hata kama unauguza popote ulipo unawasha gari usiku huo huo, hatari sana huo mlipu ni noma sana
Dah nimeumia sana. Tunarogwa sana
 
Wabaki na wake zao mazaa...watulie. Wangetulia haya yote wangeyapata wapi? Wengne wakaoa na kuoa..jua likazama wakarudi mikono mitupu kwa wake zao. Bahati wake wana hekima na huruma wakawasamehe. Pesa wanazozipata zinawazuzua wanatamani kuonja...too bad wanaangukia kwa mlipu..wanalipuliwa. wanadhani ni sifa kumbe..wanafukuza upepo.

Mwisho wa siku mtoto akimpa hela mama yake wanalalamika wanadharauliwa kumbe enzi za ujana na nguvu waliwekeza kwa kina mlipu...solution wabaki na wake zao..kila mtu yu na tamaa..na uzinzi unaondoa ufahamu na akili. Watakuwa watumwa wa ngono mpaka lini. Ngono kila siku ina mambo mapya. Hutamaliza starehe zote dunia hii.

Fanya starehe uchoke..ukishaingia kwenye ndoa tulia. Hawaelewi wanaona wanapangiwa maisha wanataka uhuru. Wataacha kulipuliwa....sad...
Hayo yote hatufanyi kwa matakwa yetu, tunakuwa tumelipuliwa. Mtuombee sana
 
Back
Top Bottom