Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Ki ukweli kazi ya ualimu ina vimelea vingi vya umasikini na ufukara wa kutukuka japo ni kazi ya heshima, ila inakimbiliwa kwa sababu ajira yake ipo kwa wingi. Elimu ya ufundi ilidharaulika sana na ilionekana inawafaa zaidi darasa la saba, lakini mambo yamebadilika. Mafundi sasa hivi ndio wanatengeneza hela kuliko mwalimu, kijana mdogo tu anamiliki nyumba aliyojenga bila kukopa kutokana na hela za ufundi. Basi tu, kwa kuwa walimu wanahitajika kufundisha wanafunzi, wakusomea ualimu wakasome tu waridhike na mshahara wa mwezi mpaka watakapostaafu, maana ni fungu walilolichagua maishani.
 
Tukubaliane na hali halisi, walimu wanaosubiri ajira mtaani ni wengi mno, na ambao wako mbioni kuhitimu na ni wengi, maelfu kwa maelfu, ukijumlisha na walio mtaani wanaweza kufika makumi ya maelfu.

Tusipochukua hatua hii, ipo siku idadi ya walimu itakuwa sawa na wanafunzi. Hivyo basi tujiulize, nini hupelekea mtu kusomea ualimu huku akijua kabisa tatizo lilipo la over-supply ya walimu? Je ni kukosa taarifa ya hali ya soko la ajira ya ualimu? Je, ni viwango vidogo vya ufaulu vinavyowekwa kama vigezo vya kusomea ualimu? Au ni nini hasa? Maana mishahara ni midogo, na mazingira ya kazi ni magumu pia, so then why mnasomea ualimu?

USHAURI:
1.) Vijana muende mkasome VETA, achaneni na ualimu, huku mtaani kuna demand kubwa ya watu wenye technical skills mbali mbali, huu mtego tuliowekewa na mkoloni kwa mfumo wake wa elimu umetutesa vya kutosha jamani, inatosha!!!! Enough is enough, huu uchawi wa mkoloni ufike mwisho, ni uchawi hatari sijawahi ona, ufike mwishoo!

2.) Serikali ipige kodi nzito mno bidhaa yeyote inayoagizwa toka nje ambayo pia inadhalishwa hapa nchini; tumeanza na fenicha toka China, angalau sasa vijana tunaona jinsi wanavyotusua kwenye biashara za useremala huko Instagram, vijana wamejiajiri na wanauza vitanda, masofa, makabati ya nguo , meza, dressing table n.k, kabla ya hapo waChina walikuwa wanaua kabisa hizi ajira na makabati yao ya pumba za maranda ya mbao. Na bado ongezeni kodi hizo fenicha ili walau vijana watakaoenda VETA wakitoka huko wajiachie na kujimwayamwaya kwenye nchi yao, tusiwanyanyase, pigeni kodi nzito!!!!

3.) Wachomelea mageti, Alluminium na glass nao naona wanakula kiulaini sana huko instagram, majengo mengi siku hizi watu wanaweka magrill ya chuma, glass na alluminium kwenye madirisha, vijana wanajimwayamwaya sana kwenye hii sekta, sasa kikubwa ni kuhakikisha wale wazalishaji wa ndani wa vitu kama alluminum , steel nk. wapewe upendeleo wa aina yake ili yale washindane na zinazotoka nje, vijana wapate ajira huko. Either way, vijana mkasomee huu utalaam wa kuchomelea mageti yale ya kisasa na madirisha ya alluminum, fungueni ma-account Instagram, tangazeni kwa fujo (sponsored ads) mle mema ya nchi yenu nyei, achaneni na ualimu.

3.) Washonaji wa seatcover za magari nao nimeona wanafaidi vinono huko instagram, sasa kikubwa yale maseat cover ya kutoka China yapigwe kodi nzito hadi waagizaji waone kizunguzungu, kiukweli huu utaalam inabidi vijana muende VETA mkasomee hii taaluma, inaitwa ‘CAR UPHOLSTERY’ aisee hii ni tamu, nadhani zile ngozi zinazotupwa vinginguti zitakuja kiwa lulu, maana Upholstery inakuwa tamu kupindukia ukitumia ngozi halisi, achana na yale maleather famba toka China, yaani gari inarekebishwa Dashboard inakuwa tamu hadi unatamani uilambe, seat covers za ngozi zinautamu wake jamani, Instagram watu wanafaidi sana kwenye hiki kitengo, achaneni na ualimu, tumieni akili vijana, magari yenye uchakavu wa interior ni mengi kupita maelezo, go where the demand is!

Nikiamka asubuhi naweka list ya vitengo kama kumi hivi ambapo watu wanalamba asali kiulaini huko instagram, ila kwenye mzinga wangu sitawaambia, bado nalamba lamba mwenyewe kwanza, nikishiba nitawaambia.😂

==================================

4.) Huko Instagram nimebaini pia kuwa kitengo cha BAKERY (CAKES) wananyonya vitamu kiulaini sana! Siku birthdays zimekuwa ni kitu cha kawaida, hadi watu wazima wanafanya birthday, na hii shughuli kiungo chake muhimu ni Keki, halikadhalika graduations za vyuo, maharusi nk; kote huko keki zinahitajika. Vifaa vya kutengeneza keki vinapatikana kwa urahisi na ni bei nafuu sana; mkosomee kozi za bakery jamani, tena ukija kubabatiza order za keki za harusi ndio utaona utamu wa bakeries, keki unatumia laki2 kutengeneza ila unauza laki8. Unatafuta hata bodaboda unaemuamini anakuwa anafanya deliveries sehemu mbalimbali, anapewa pesa on delivery anakuletea. Tena hii unaweza kufanya baking ya keki hata chumbani kwako, unatangaza Instagram kwa sponsored ads wateja wanamiminika tu, keki ziko on high demand jamani, tukajifunze BAKERY!
  • Ongezea na fani za ufundi wa magari/bajaji/pikipiki nao sii haba wanafyonza vijiasali wanatupiga spea za uongo mpaka tunakoma.😀
  • Kuna ufundi mwingine wala huitaji kwenda veta, mfano hawa wanaoweka urembo/tinted/stika/rim kwenye magari
  • Kuna watu wanafyonza asali vibaya mno kwa kuweka urembo kwenye milango/madirisha ya nyumba dirisha 1 utaambiwa 60,000 na material zote zakwako
  • Kuna watu wa garden siku izi kuotesha ukoka na kuulea utaambiwa 300k kwa mwezi.. vijana changamkieni fursa hizi
 
Kwa hio suluhisho ni VETA tu, hao mafundi wakijazatazana watamtengenezea nani?
Mtaani mafundi ni wengi sana tu.

Jambo la msingi vijana wawe competent na wawe na confidency.
Ukiwa na hivyo viwili ajira utapata au utajiajiri. Wekeza kijifunza life skills sio tu vocational skills haisaidii sanaa.
Vijana wajifunze teknolojia za kisasa hasa computer nabna online bussiness .

Wajifunze kujiajili kupitia mitandao, mfano wewe unasema hakuna ajira za kufundisha wakati kuna ajira nyingi tu za kufundisha mitandaoni.

Wekeza ktk lifelong learning, kuwa multi purpose, angalia soko ka dunia linataka nini.
Elimu ya ualimi ina kufindisha how to be critical thinker, presentation skills, personality, communication skill hata teknolojia. Tatizo lipo kwa wasomaji wenyewe wana focus katika nini.

I tell you education is multidisciplinary discipline inaingiaa kila eneo kuanzia ujasiliamali,ufundi, uhasibu,sayansi, saikolojia, fslsafa, teknolojia, jamii , lugha(hizi ni nyanja zote za maisha ya mwanadamu, acheni ujinga)

Msio elewa hii fani mtabaki kuiponda lakini ndio fani inayoongoza kwa ajira nyingi na uwanja mpana hata viongozi wengi wanatokana na fani ya elimu.

Kuna usemi unasema elimu ni ufunguo wa maisha haujabainisha kuwa ualimu si ufunguo wa maisha bsli ni ufunguo wa umasikini.
Poor young boy! Open up your mind.
 
Asee mi naona ni vzur wakaanzisha elimu ya ufundi Hadi kwa shule za sekondari yani mtu anachagua fani moja tu anaisomea na ataifanyia mtihani wa form 4 pale au ata form six akifika atasomea fani ile ile aliyochagua ,,,kwa kufanya ivyo ikitokea mtu amefeli kabs form 4 pale ile fani aliyosomea itamwezesha ata kwenda veta kujiendeleza na kuwa na ujuzi mzur zaid.
 
Ni kweli, Lakini kwa standard za kimataifa walimu bado hawatoshi kabisa. Ni kama madaktari tu, Tanzania ipo chini sana kwenye uwiano wa daktari kwa mgonjwa lakini bado madaktari wanakosa kazi.
 
Hivi mpaka sasa hapa Tanzania bado watu wanahimizwa kusoma ili kuja kuajiriwa? Tumechelewa sana.
Zama zimeshabadilika, usomi wa kuja kuzurura na bahasha ya kusaka ajira mitaani ni zaidi ya kubet.
 
Na wale Assistant clinical officer huwa wanaajiriwa?
Kwa mbinde sana, kuna course ukisoma inakua kama ngazi ya kupandia kielimu tu na sio kwa ajili ya ajira, mfano kwa sasa hiyo clinical medicine ni ya kusoma na kupambana kupata GPA ya at least 4.5 on the way to degree, period.
 
Tujiulize hizo shule zina walimu wakutosha!kuna shule inawalimu wawili tu.unasemaje mahitaji ya walimu hakuna.tatizo ni serikali haina pesa za kuajiri walimu.lakini mahitaji ni makubwa sana.shule azina walimu..

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Hapa duniani hakuna taaluma yenye upungufu ya watendaji, bali kuna upungufu wa pesa za kuwaajiri. Tunaposema supply imekuwa kubwa kuliko demand, tunamaanisha wanaosomea ni wengi kuliko uwezo wa soko la ajira kuwafyonza, tumeelewana?
 
Back
Top Bottom