Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Una uhakika demand ni ndogo kuliko supply????...uliza walimu ujibiwe watu wapo na masomo wasiyosomea kufundisha
Tunaposema demand ni ndogo, tunamaanisha uwezo wa soko kuwafyonza walimu wanaozalishwa vyuoni ni dogo kuliko idadi ya walimu wanaozalishwa, kwenye sekta ya ualimu imefikia critical level.
 
Kwa hio suluhisho ni VETA tu, hao mafundi wakijazatazana watamtengenezea nani?
Mtaani mafundi ni wengi sana tu.
Jambo la msingi vijana wawe competent na wawe na confidency.
Ukiwa na hivyo viwili ajira utapata au utajiajiri. Wekeza kijifunza life skills sio tu vocational skills haisaidii sanaa.
Vijana wajifunze teknolojia za kisasa hasa computer nabna online bussiness .
Wajifunze kujiajili kupitia mitandao, mfano wewe unasema hakuna ajira za kufundisha wakati kuna ajira nyingi tu za kufundisha mitandaoni.
Wekeza ktk lifelong learning, kuwa multi purpose, angalia soko ka dunia linataka nini.
Elimu ya ualimi ina kufindisha how to be critical thinker, presentation skilks, personality, communication skill hata teknolojia. Tatixo lipo kwa wasomaji wenyewe wana focus katika nini.
I tell you education is multidisciplinary discipline inaingiaa kila eneo kuanzia ujasiliamali,ufundi, uhasibu,sayansi, saikolojia, fslsafa, teknolojia, jamii , lugha(hizi ni nyanja zote za maisha ya mwanadamu, acheni ujinga) .
Msio elewa hii fani mtabaki kuiponda lakini ndio fani inayoongoza kwa ajira nyingi na uwanja mpana hata viongozi wengi wanatokana na fani ya elimu.
Kuna usemi unasema elimu ni ufunguo wa maisha haujabainisha kuwa ualimu si ufunguo wa maisha bsli ni ufunguo wa umasikini.
Poor young boy! Open up your mind.
VETA sio ufundi tu, tunazungumzia skills za aina mbali mbali, mfano BAKERY, ni SKILL, ila sio UFUNDI.
 
Asee mi naona ni vzur wakaanzisha elimu ya ufundi Hadi kwa shule za sekondari yani mtu anachagua fani moja tu anaisomea na ataifanyia mtihani wa form 4 pale au ata form six akifika atasomea fani ile ile aliyochagua ,,,kwa kufanya ivyo ikitokea mtu amefeli kabs form 4 pale ile fani aliyosomea itamwezesha ata kwenda veta kujiendeleza na kuwa na ujuzi mzur zaid.
Wazo zuri sana, mtu akifeli awe na back up skills za kusonga mbele.
 
Ni kweli, Lakini kwa standard za kimataifa walimu bado hawatoshi kabisa. Ni kama madaktari tu, Tanzania ipo chini sana kwenye uwiano wa daktari kwa mgonjwa lakini bado madaktari wanakosa kazi.
Hakuna fani yenye uhaba wa watendaji hapa duniani, bali kuna uhaba wa pesa za kuajiri hao watendaji. Hivyo tunaposema supply imezidi demand, ni kwamba supply imezidi uwezo wa kuajiri.
 
Tukubaliane na hali halisi, walimu wanaosubiri ajira mtaani ni wengi mno, na ambao wako mbioni kuhitimu na ni wengi, maelfu kwa maelfu, ukijumlisha na walio mtaani wanaweza kufika makumi ya maelfu.

Tusipochukua hatua hii, ipo siku idadi ya walimu itakuwa sawa na wanafunzi. Hivyo basi tujiulize, nini hupelekea mtu kusomea ualimu huku akijua kabisa tatizo lilipo la over-supply ya walimu? Je ni kukosa taarifa ya hali ya soko la ajira ya ualimu? Je, ni viwango vidogo vya ufaulu vinavyowekwa kama vigezo vya kusomea ualimu? Au ni nini hasa? Maana mishahara ni midogo, na mazingira ya kazi ni magumu pia, so then why mnasomea ualimu?

USHAURI:
1.) Vijana muende mkasome VETA, achaneni na ualimu, huku mtaani kuna demand kubwa ya watu wenye technical skills mbali mbali, huu mtego tuliowekewa na mkoloni kwa mfumo wake wa elimu umetutesa vya kutosha jamani, inatosha!!!! Enough is enough, huu uchawi wa mkoloni ufike mwisho, ni uchawi hatari sijawahi ona, ufike mwishoo!

2.) Serikali ipige kodi nzito mno bidhaa yeyote inayoagizwa toka nje ambayo pia inadhalishwa hapa nchini; tumeanza na fenicha toka China, angalau sasa vijana tunaona jinsi wanavyotusua kwenye biashara za useremala huko Instagram, vijana wamejiajiri na wanauza vitanda, masofa, makabati ya nguo , meza, dressing table n.k, kabla ya hapo waChina walikuwa wanaua kabisa hizi ajira na makabati yao ya pumba za maranda ya mbao. Na bado ongezeni kodi hizo fenicha ili walau vijana watakaoenda VETA wakitoka huko wajiachie na kujimwayamwaya kwenye nchi yao, tusiwanyanyase, pigeni kodi nzito!!!!

3.) Wachomelea mageti, Alluminium na glass nao naona wanakula kiulaini sana huko instagram, majengo mengi siku hizi watu wanaweka magrill ya chuma, glass na alluminium kwenye madirisha, vijana wanajimwayamwaya sana kwenye hii sekta, sasa kikubwa ni kuhakikisha wale wazalishaji wa ndani wa vitu kama alluminum , steel nk. wapewe upendeleo wa aina yake ili yale washindane na zinazotoka nje, vijana wapate ajira huko. Either way, vijana mkasomee huu utalaam wa kuchomelea mageti yale ya kisasa na madirisha ya alluminum, fungueni ma-account Instagram, tangazeni kwa fujo (sponsored ads) mle mema ya nchi yenu nyei, achaneni na ualimu.

3.) Washonaji wa seatcover za magari nao nimeona wanafaidi vinono huko instagram, sasa kikubwa yale maseat cover ya kutoka China yapigwe kodi nzito hadi waagizaji waone kizunguzungu, kiukweli huu utaalam inabidi vijana muende VETA mkasomee hii taaluma, inaitwa ‘CAR UPHOLSTERY’ aisee hii ni tamu, nadhani zile ngozi zinazotupwa vinginguti zitakuja kiwa lulu, maana Upholstery inakuwa tamu kupindukia ukitumia ngozi halisi, achana na yale maleather famba toka China, yaani gari inarekebishwa Dashboard inakuwa tamu hadi unatamani uilambe, seat covers za ngozi zinautamu wake jamani, Instagram watu wanafaidi sana kwenye hiki kitengo, achaneni na ualimu, tumieni akili vijana, magari yenye uchakavu wa interior ni mengi kupita maelezo, go where the demand is!

Nikiamka asubuhi naweka list ya vitengo kama kumi hivi ambapo watu wanalamba asali kiulaini huko instagram, ila kwenye mzinga wangu sitawaambia, bado nalamba lamba mwenyewe kwanza, nikishiba nitawaambia.[emoji23]

==================================

4.) Huko Instagram nimebaini pia kuwa kitengo cha BAKERY (CAKES) wananyonya vitamu kiulaini sana! Siku birthdays zimekuwa ni kitu cha kawaida, hadi watu wazima wanafanya birthday, na hii shughuli kiungo chake muhimu ni Keki, halikadhalika graduations za vyuo, maharusi nk; kote huko keki zinahitajika. Vifaa vya kutengeneza keki vinapatikana kwa urahisi na ni bei nafuu sana; mkosomee kozi za bakery jamani, tena ukija kubabatiza order za keki za harusi ndio utaona utamu wa bakeries, keki unatumia laki2 kutengeneza ila unauza laki8. Unatafuta hata bodaboda unaemuamini anakuwa anafanya deliveries sehemu mbalimbali, anapewa pesa on delivery anakuletea. Tena hii unaweza kufanya baking ya keki hata chumbani kwako, unatangaza Instagram kwa sponsored ads wateja wanamiminika tu, keki ziko on high demand jamani, tukajifunze BAKERY!
Kule tunafata boom
 
VETA sio ufundi tu, tunazungumzia skills za aina mbali mbali, mfano BAKERY, ni SKILL, ila sio UFUNDI.
Kama unatolewa na VETA basi ni ufundi, kazi ya veta ni kusambaza ufund hata upishi ni ufundi, kusuka nywele ni ufundi, kinyozi ni fundi.
Usikariri kuwa fundi kazima abebe nyundo, bisibisi, koleo nk.
Kupika mkate ni ufundi.
Skill maana yake ni ujuzi.
 
Mi naita SKILL, itoshe kusema hivyo, we ita UFUNDI. Kazi iendelee.
 
VETA sio ufundi tu, tunazungumzia skills za aina mbali mbali, mfano BAKERY, ni SKILL, ila sio UFUNDI.
Nimeiggogo jf maana ya fundi.
Ufundi nu ujuzi hasa wa kazi za mikono. Usichanganye ukafikiri skill ni neno la kipekee.
Skill linatumika mahala pengi sana.

Screenshot_20211012-213219.png
 
Napingana na wewe kwa data. Mfano uhitaji wa walimu shule za msi ngi kwa wilaya ya mpwapwa ni wastani wa walimu 2200 ilihali walimu waliopo ni 1300 hv kwa hiyo kuna upungufu wa walimu 900

Shule za awali zinauhitaji wa wastani wa walimu 240 hv lakini Cha kuchekesha wilaya nzima haina mwalimu aliyeajiriwa ili afundishe elimu awali tuu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kwa hiyo wilaya moja tuu ina uhaba wa walimu wa msingi na awali 1140 hv .. je Tanzania nzima????

Tatizo lililopo ni kwamba serikali ya ccm inaona kuwekeza kwenye ajira za walimu ni dhambi ya mauti....

Aiseee kazi iendeleee,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mi naita SKILL, itoshe kusema hivyo, we ita UFUNDI. Kazi iendelee.
Haya ila usije kuropoka mbele ya wasomi utaonekana kilaza.
Inawezekana wewe ni mmoja wa wale wanaolalamikia kutoimudu vizuri lugha ya kingereza, inaonesga hauimudu english vizuri. Ufindi ni kiswahili,skill ni kingereza, huwezi linganisha mneno hayo kimaana.
 
Napingana na wewe kwa data. Mfano uhitaji wa walimu shule za msi ngi kwa wilaya ya mpwapwa ni wastani wa walimu 2200 ilihali walimu waliopo ni 1300 hv kwa hiyo kuna upungufu wa walimu 900

Shule za awali zinauhitaji wa wastani wa walimu 240 hv lakini Cha kuchekesha wilaya nzima haina mwalimu aliyeajiriwa ili afundishe elimu awali tuu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kwa hiyo wilaya moja tuu ina uhaba wa walimu wa msingi na awali 1140 hv .. je Tanzania nzima????

Tatizo lililopo ni kwamba serikali ya ccm inaona kuwekeza kwenye ajira za walimu ni dhambi ya mauti....

Aiseee kazi iendeleee,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Acha ubishi wa kijinga.
 
Nimeiggogo jf maana ya fundi.
Ufundi nu ujuzi hasa wa kazi za mikono. Usichanganye ukafikiri skill ni neno la kipekee.
Skill linatumika mahala pengi sana.

View attachment 1972400
Lugha ni maelewano, naamini naeleweka zaidi kwa hadhira yangu nikitofautisha ufundi na ‘SKILL’, hadhira yangu inachukulia Fundi kama mtu anaerekebisha kilichoharibika au kuunda kitu kipya, hata kama si sahihi, ila huo ndio uelewa wao. Kwa upande mwingine, ‘SKILL’ inachukuliwa kama taaluma yeyote including ‘UFUNDI’. Naomba sana itoshe kusema hivyo.
 
Napingana na wewe kwa data. Mfano uhitaji wa walimu shule za msi ngi kwa wilaya ya mpwapwa ni wastani wa walimu 2200 ilihali walimu waliopo ni 1300 hv kwa hiyo kuna upungufu wa walimu 900

Shule za awali zinauhitaji wa wastani wa walimu 240 hv lakini Cha kuchekesha wilaya nzima haina mwalimu aliyeajiriwa ili afundishe elimu awali tuu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kwa hiyo wilaya moja tuu ina uhaba wa walimu wa msingi na awali 1140 hv .. je Tanzania nzima????

Tatizo lililopo ni kwamba serikali ya ccm inaona kuwekeza kwenye ajira za walimu ni dhambi ya mauti....

Aiseee kazi iendeleee,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Umepaisha mpira ndugu. Tunaposema uhaba wa ajira tunamaanisha uhaba wa pesa za kuajiri taaluma husika, na sio uhaba wa wataalam wa kada husika.
 
Haya ila usije kuropoka mbele ya wasomi utaonekana kilaza.
Inawezekana wewe ni mmoja wa wale wanaolalamikia kutoimudu vizuri lugha ya kingereza, inaonesga hauimudu english vizuri. Ufindi ni kiswahili,skill ni kingereza, huwezi linganisha mneno hayo kimaana.
Post yangu na.54 itakufaa pia.
 
Back
Top Bottom