Mambo ya Huduma za burebure yalikuwa zamani Enzi za UTUMWA. Kwa sasa kila mtu yu Huru. Yesu alisema mkiujua ukweli utwaweka huru. Kwa nini umtumikie Mungu burebure Kama vile mtumwa wake. Wewe sio mtumwa. Wala wewe sio MATEKA, Wengi hutumia Kauli kuwa mtumikie Mungu atakulipa yeye mwenyewe, wakati wao tunawalipa Sisi kwa Zaka na Sadaka zetu. Mtu akikuambia hivyo mwambie amtumikie yeye huyo Mungu burebure. Mbona wao wanalipwa?
Wachungaji wanalipwa,
Waalimu wanalipwa,
Watangazaji wanalipwa,
Waandishi wanalipwa,
Maaskofu wanalipwa,
Madaktari wanalipwa,
Madereva wanalipwa,,
Hao wote wanamfanyia kazi Mungu kila mmoja Kwa nafasi yake,
Iweje hawa Wanakwaya na wahudumu wa Kanisani wafanye kazi burebure Kama watoto wadogo au kama Watumwa?