DALALI MKUU
JF-Expert Member
- May 7, 2022
- 2,011
- 4,705
Kuimba kwaya sio Kazi ni Huduma ya kujitolea.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ikisha fika hatua ya kuuza nyimbo baada ya kuzirekodi au kualikwa kwenye mikutano,basi,hiyo neno la kujitolea lisitumike tena,walipwe posho yao.Kuimba kwaya sio Kazi ni Huduma ya kujitolea.
Hoja yako ni nzuri,IFIKE MAHALA WANAKWAYA NA WATOA HUDUMA KANISANI WALIPWE MISHAHARA KWA MWEZI!
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu Jeusi.
Hii ni mara ya tatu nazungumzia Jambo hili. Mara ya Kwanza nililizungumza mwaka 2012, mara ya pili 2020, Kutokana na Unyeti wa Jambo lenyewe.
Mambo ya Huduma za burebure yalikuwa zamani Enzi za UTUMWA. Kwa sasa kila mtu yu Huru. Yesu alisema mkiujua ukweli utwaweka huru. Kwa nini umtumikie Mungu burebure Kama vile mtumwa wake. Wewe sio mtumwa. Wala wewe sio MATEKA, Wengi hutumia Kauli kuwa mtumikie Mungu atakulipa yeye mwenyewe, wakati wao tunawalipa Sisi kwa Zaka na Sadaka zetu. Mtu akikuambia hivyo mwambie amtumikie yeye huyo Mungu burebure. Mbona wao wanalipwa?
Wachungaji wanalipwa,
Waalimu wanalipwa,
Watangazaji wanalipwa,
Waandishi wanalipwa,
Maaskofu wanalipwa,
Madaktari wanalipwa,
Madereva wanalipwa,,
Hao wote wanamfanyia kazi Mungu kila mmoja Kwa nafasi yake,
Iweje hawa Wanakwaya na wahudumu wa Kanisani wafanye kazi burebure Kama watoto wadogo au kama Watumwa?
Makanisa yaandae utaratibu wa kuwaajiri wanakwaya na wahudumu wa kanisani na kuwalipa Kwa mwezi Kwa Mshahara uliorafiki kulingana na mapato ya Kanisa husika.
Asije akakudanganya Mtu kuwa Dini sio biashara, huo ni uongo wa Mchana. Na anayekuambia hivyo kakudharau.
Dini ni biashara, ni Huduma ya kiroho ambayo watu hulipia Kwa zaka na Sadaka, na baadhi ya Huduma kama ubatizo, sijui ndoa, sijui mazishi n.k. Sasa iweje isiwe biashara.
Kuwa na imani bila akili madhara yake ndio kugeuzwa MSUKULE wa watu Fulani katika taasisi za Kidini.
Kukombolewa kiimani ni pamoja na kumtumikia Mungu na kupata faida ya kile ukifanyacho.
Nimeona Vijana wengi wengi Sana wanalitumikia Kanisa pasipo faida yoyote. Sasa huko ni kumtumikia Mungu au kugeuzwa MATEKA na viongozi wa Dini.
Vijana, msikubali kazi za kujitolea kama vile wajingawajinga. Jitolee kama unauwezo na unakipato cha kulisha familia yako. Lakini huna kazi, huna Ajira lakini unapoteza muda na jasho lako burebure wakati wenzako wanalipwa huo ni ukosefu wa kujitambua na maarifa.
Makanisa yanamiradi mingi, yapo mashule, yapo mahospitali, zipo media na vyanzo vingine vya mapato. Iweje Kanisa likose mishahara ya kuwalipa Wanakwaya?
Hiyo miradi licha ya kuwa niya kanisani lakini haina faida yoyote Kwa waumini. Kama ni Ada au pesa za huduma ni ghali Kwa Aidha waumini na wasiowaumini.
Vitoto vya masikini na wanawake WA masikini ndio wamegeuka wahanga wa Biashara hizi za makanisa.
Kupitia nyimbo zao wateja WA Kanisa (waumini) wanaongezeka lakini kipi Wanachokipata hao Wanakwaya. Zaidi ya kupoteza muda wao bure huku wao na familia zao wakiendelea kufa masikini ilhali wanalitumikia Kanisa.
Au faida ni kuzikwa, embu ifike mahala mambo ya kinyonyaji Kwa mgongo wa kutishia watu kiroho yaishe.
Unakuta mpaka Familia zingine zinavunjika kisa upuuziupuuzi wa Kidini.
Wanawake wengine wasio na akili ati wanakuwa bize na mambo ya Kanisa kuliko kumhudumia Mume na familia lakini hakuna faida yoyote. Huo ni upuuzi ambao Taikon nasema kamwe hautavumiliwa na Wanaume Makuhani.
Watu lazima waelewe kuwa wanapofanya kazi, wanawatumikia watu wa Mungu. Unapoimba kanisani unawaimbia Watu, haumuimbii Mungu.
Mchungaji anahubiri kanisani hamuhubirii Mungu. Anahubiria watu. Hivyo lazima Alipwe. Mungu Hana uhitaji na hayo mambo yetu ya kibinadamu.
Dereva anapoendesha abiria, hamuendeshi Mungu Bali anaendesha watu wa Mungu.
Mungu kaweka hizo kazi ili kila mtu apate kipato kulingana na kazi yake. Sio yeye apate kipato. Mungu kipato anapeleke wapi.
Zaka ni pesa ya watumishi wa Mungu wanaohudumu madhabahuni wakiwemo hao wanakwaya na wote wanaofanya kazi madhabahuni.
Wachungaji na viongozi WA dini wamejimilikisha Zaka na kuwasahau Watumishi wengine WA Kanisa.
Kwa nini muwape Posho ilhali nao watumishi wa Kanisa na sio vibarua.
Watu wajanja na matapeli ndio hutumia neno la Mungu vibaya kuwadhulumu watu.
Kanisa lazima lifanye Reformation kuhakikisha linatenda HAKI.
Sio litumie nguvu kazi za bure Kwa watu kujiimarisha Kwa thamani ya neno "Mbarikiwe"
Sisi waumini ndio hatupaswi kulipwa Kwa sababu hatuzalishi ingawaje Kila siku kanisani tunapewa majukumu ya kutangaza Injili Jambo ambalo sio jukumu letu. Nitangaze Injili mtanilipa?
Lakini wanakwaya Ambao wanawaongezeeni wateja(waumini wapya) hamtaki kuwalipa ilhali wanachangia kwa kiasi kikubwa katika Huduma zenu. Huo ni uhuni.
Mnataka waumini wafanye majukumu yasiyowahusu ili ninyi mfanye nini?
Hivi mtu ni Daktari aache kufanya kazi yake ya kutoa Huduma Kwa wateja wake(wagonjwa) aanze kuhubiri habari za Kanisa lake ambapo halipwi. Seriously!
Waumini kazi Yao ni Kutoa zaka na Sadaka ili ninyi ndio mpange mikakati ya kukuza Huduma zenu ili muongeze wigo wa wateja wenu mpate pesa zaidi.
Sajilini Wanakwaya na watoa Huduma wote kanisani waingizeni kwenye malipo ya mishahara Kwa mwezi. Hao watendakazi ndio wawe na wajibu wa kusambaza neno la Mungu mnayemuamini kujipatia wateja wapya.
Wapo waimbaji WA kwaya mashuhuri lakini maisha Yao halisi yanatia Aibu. Na hakuna anayejali.
Ni Bora labda wangepewa hata ofa kuwa Watoto wao watasomeshwa bure au watalipia Nusu ya gharama za Shule katika shule za taasisi za Dini Kama wanavyofanyiwa Wachungaji.
Lakini wanakwaya wamesahaulika Kama sio kudharauliwa.
Alafu mtu anamfuata Mwanakwaya mbona siku hizi Hauimbi kwaya, akikuambia mambo yamembana, unamwambia mambo ya Dunia yasikufanye ushindwe kumtumikia Mungu.
Walipeji watu Kwa mwezi Kama wengine wanavyolipwa muone Kama kuna atakayesuasua.
Mimi nimemaliza.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Nairobi, Kenya
Nashauri ungemjibu kwa maandiko pia,kama alivyokujibu yeye.Kunukuu vifungu siyo kujua misingi ya dini. Na zaidi unanukuu kitu kinachoonyesha uko very wrong. Kumbe bwana amesema wapate riziki, kitu ambacho kinafanyika. Unajua maana ya riziki? Mbona wanakwaya wanapokuwa na safario hupata huduma eh chakula, usafiri, malazi bure? Hiyo siyo riziki au riziki mpaka iwe fedha?
Hawauzi kanisan hakuna biashara ni kuchangiwa hudumaIkisha fika hatua ya kuuza nyimbo baada ya kuzirekodi au kualikwa kwenye mikutano,basi,hiyo neno la kujitolea lisitumike tena,walipwe posho yao.
Maandiko yake yanasapoti hoja yangu. BTW mbona kanisa ninalosali mimi wanakwaya wakiwa na trip kanisa za kikanisa, kanisa ndiyo linatoa huduma?Hoja yako ni nzuri,
Ni kweli,wahudumu wengine katika kanisa wanapaswa watiwe moyo kwa;
1.Kuwapa chochote kwa kadili ya mapato ya Kanisa&kwa utaratibu litakalojiwekea kanisa.
2.Kanisa ligharamie huduma zake,na si kutegemea watu kujitolea mara zote.
Mf;Nauli za wahudumu kwenda mahali fulani kihuduma,mawasiliano n.k.
3.Watumishi ngazi za juu,watambue michango ya wahudumu wengine katika huduma.
Nashauri ungemjibu kwa maandiko pia,kama alivyokujibu yeye.
Aliyekuambia padre ana mshahara ni nani? Jimbo gani hilo? Ule siyo mshahara bali ni posho. Habari ya kuishi kila Jumapili tumapeleka matoleo kwenye nyumba ya mapadre!😀😀😀
Kwani mishahara wanayolipwa wengine kazi yake si kuwasaidia kuendesha maisha Yao.
Aliyekuambia Padri Hana Mshahara ni Nani?
Anaishije?
Anakula chakula kutoka wapi?
Analala kwenye nyumba ipi?
Anavaa nguo Kwa pesa ipi?
Anasafiri Kwa pesa ipi?
Hakuna ambaye halipwi hapa Duniani, tena hao ndio Mshahara Yao ni mikubwa kuliko watu wengine
Posho na mshahara zote ni payment in form of money sijui mnafail wapi kumuelewa mtoa mada.Aliyekuambia padre ana mshahara ni nani? Jimbo gani hilo? Ule siyo mshahara bali ni posho. Habari ya kuishi kila Jumapili tumapeleka matoleo kwenye nyumba ya mapadre!
Wanauza wapi?Hawauzi kanisan hakuna biashara ni kuchangiwa huduma
Unazidi kuonyesha uchanga wako kwenye neno. Uchungaji, uanakwaya, uhudumu wa kanisani SIYO kazi. Ni huduma za kujitolea zisizo na malipo. Achana na hawa viongozi matepeli wanabadilisha magari kila kukicha.
Hiyo pesa ya kujikimu ni sh ngapi? Na kwann hao wanakwaya hawapewi hiyo ya kujikimu? Itakuwa ww ni miongoni mwa hao matapeli wanaotumia iman kuwalaghai watuPadri hana mshahara ficha ujinga wako. Padri anakula chakula kinachopikwa kwenye parokea kwa kutumia fedha za parokea. Akiwa nje kihuduma ndiyo anapewa posho ya kujikimu na siyo mshahara. Nimesema tena na tena, wanapata posho na siyo mshahara. Unajua sifa za malipo kuitwa mshahara wewe?