Ifike mahali Wanakwaya kanisani na wahudumu wa Kanisani Walipwe mishahara Kwa mwezi

Kuimba kwaya sio Kazi ni Huduma ya kujitolea.
Ikisha fika hatua ya kuuza nyimbo baada ya kuzirekodi au kualikwa kwenye mikutano,basi,hiyo neno la kujitolea lisitumike tena,walipwe posho yao.
 
Ni vema na haki kabisa.
Wako wale walimu au huitwa makatekista hawa watu wengi wao huishi maisha magumu sana tofauti na mapadri.
Makatekista wanambiwa kufanya kazi ya Mungu lakini mapadri wao wanaposho hakika hili halijaa sawa.

Sehemu nyingine niliona mpishi wa parokia fulani amefanya kazi kwa miaka mingi bado anatembea bila viatu yani kapigika choka mbaya mfukoni jela jeraha.
 
😆😆nacheka huku naogopa
Kuna watu tutafika mbinguni tumechoka sana😂😂
 
Siku zote wajinga ndio waliwao.. Huu ni ukweli wa

wazi kabisa ..,lakin kusikia kwa kenge mpaka

masikio yatoke damu.
 
Hoja yako ni nzuri,
Ni kweli,wahudumu wengine katika kanisa wanapaswa watiwe moyo kwa;
1.Kuwapa chochote kwa kadili ya mapato ya Kanisa&kwa utaratibu litakalojiwekea kanisa.
2.Kanisa ligharamie huduma zake,na si kutegemea watu kujitolea mara zote.
Mf;Nauli za wahudumu kwenda mahali fulani kihuduma,mawasiliano n.k.
3.Watumishi ngazi za juu,watambue michango ya wahudumu wengine katika huduma.
Nashauri ungemjibu kwa maandiko pia,kama alivyokujibu yeye.
 
Ikisha fika hatua ya kuuza nyimbo baada ya kuzirekodi au kualikwa kwenye mikutano,basi,hiyo neno la kujitolea lisitumike tena,walipwe posho yao.
Hawauzi kanisan hakuna biashara ni kuchangiwa huduma
 
Maandiko yake yanasapoti hoja yangu. BTW mbona kanisa ninalosali mimi wanakwaya wakiwa na trip kanisa za kikanisa, kanisa ndiyo linatoa huduma?
 
Aliyekuambia padre ana mshahara ni nani? Jimbo gani hilo? Ule siyo mshahara bali ni posho. Habari ya kuishi kila Jumapili tumapeleka matoleo kwenye nyumba ya mapadre!
 
Aliyekuambia padre ana mshahara ni nani? Jimbo gani hilo? Ule siyo mshahara bali ni posho. Habari ya kuishi kila Jumapili tumapeleka matoleo kwenye nyumba ya mapadre!
Posho na mshahara zote ni payment in form of money sijui mnafail wapi kumuelewa mtoa mada.
 
Nikweli! Makanisa yangeweka mifumo na namna yakuwalipa watumishi wake ndani ya makanisa ilikusaidia kuwapunguzia changamoto za maisha. Na wafocus kulitumikia kanisa kusudi ya kwamba muda wote wakitakiwa wawe wanapatikana.
 
Hawauzi kanisan hakuna biashara ni kuchangiwa huduma
Wanauza wapi?
Mkusanya fedha za mauzo ni nani?
Kuna kwaya/kanisa wanamiliki hadi coaster na zipo barabarani zinatoa 'huduma' kwa abiria...
Tusitetee unyonyaji mchungaji,tuishi kwa akili
 
Tatizo la muafrika hajielewi na hajui hata kuhesabu mda aliokuwa Dunia kaingiza kipato gani na mda alioupoteza
Kweli ni haki yao walipwe lakini ninavyojua wanavyopenda kukatika na kucheza hata ukiwaambia walipe wao watalipa tu
Mwafrika kwa mziki weee
 
Ya duniani yafanyike tukiwa duniani, na ya mbinguni yafanyike tukiwa mbinguni; kwa sababu bado tuko duniani, tuyaishi ya duniani
 
Mchungaji ana mshahara na posho pia hapa naongelea makanisa nje ya katoliki(ila hata hawa wa katoliki watakua wanalipwa pia maana wapo wenye watoto kisiri siri na wanawasomesha) na pia nje ya walokole. Yale yanayobaki wanalipwa maana wameoa na familia zinawategemea.
Unazidi kuonyesha uchanga wako kwenye neno. Uchungaji, uanakwaya, uhudumu wa kanisani SIYO kazi. Ni huduma za kujitolea zisizo na malipo. Achana na hawa viongozi matepeli wanabadilisha magari kila kukicha.
 
Hiyo pesa ya kujikimu ni sh ngapi? Na kwann hao wanakwaya hawapewi hiyo ya kujikimu? Itakuwa ww ni miongoni mwa hao matapeli wanaotumia iman kuwalaghai watu
 
Mleta mawazo nisamehe ila mawazo yako ni ya kipuuzi unafikiri neema uliyonayo ni kwasababu ya pesa yako???
 
Mkuu unajaza sana servers za jf,sio kila kitu ni cha kuleta huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…