Ifike mahali Watanzania tuache kukubali hadaa na uzushi unaotolewa na akina Evarist Chahali na Kigogo

Ifike mahali Watanzania tuache kukubali hadaa na uzushi unaotolewa na akina Evarist Chahali na Kigogo

Na wewe umekubali hadaa kuwa Jiwe alifariki tarehe 17??

Kwa uchu wa madaraka uliopo Africa kiongozi hawezi kufariki ikatangazwa siku hiyo hiyo

Kama ulivyosikia kulikuwepo na timu pinzani miongoni mwa wanakijani ambao kila mtu alikuwa na pendekezo lake nani akwae urais ni uthibitisho tosha wewe ndio uliziona ni hadaa ila ndio ulikuwa ukweli wa mambo.

Pole sana sukumagang.
Kwanza hii stori imekuwaje imeletwa leo, 3yrs later?

Any form of intention?
 
Mkuu ulitaka Generali wa Jeshi la JMT..Aende kinyume na Rais wa JMT ili kitokee nini?

Ulitaka atamka Tarehe tofauti na iliyokubalika na Serkali ili watanzania Wakose imani na Serkali? Halafu kitokee kitu gani?

Kuna Vitu huwa viko Ndani ya Kiapo mpaka unakufa na kama ni Dhambi bhasi utakufanya nayo Ilu kulinda Maslahi ya Serkali iliyopo madarakani
Kama wangetaka kuficha basi hayo aliyosema jana asingesema kabisa.
 
Tumemsikia Mkuu wa Majeshi Mstaafu Generali Mabeyo akisimulia hivi karibuni jinsi Magufuli alivyouguzwa hadi kufariki.

Katika maelezo yake, Generali anadhihirisha kuwa Magufuli alifariki tarehe na muda uliotajwa na Mhe. Samia alipokuwa akitangaza kifo hicho.

Lakini akina Evaristi Chahali na Kigogo wakajifanya wana taarifa za ndani na nyeti na kutangaza kuwa kifo hicho kilitokea kabla.

Mbaya zaidi Chahali akadai kuwa Zitto Kabwe alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Mhe. Samia kuapishwa kuwa Rais akidai kuwa kuna baadhi ya viongozi walitaka asiapishwe.

Lakini Generali anaonesha kuwa hakukuwa na changamoto ya namna hiyo. Hata kama ingekuwepo wasingemtafuta Zitto atoe ushauri.
General hawez kwenda kinyuma na kauli ya mkuu. Nakushangaa wewe ambae ulitarajia kauli tofauti
 
Kwenye hili la kigogo kuhusu kifo cha jpm alikuwa sahihi 100% kwanza pm alitudanganya akisema jpm yupo salama salimin anapiga kazi na anatusalimia.

Pia kwa akiri yangu mimi sina hakika kama rais aliyeko madarakani afariki na kifo kutangazwa palepale yaani ndani ya dk 40 au lisaa sio kweli. kama sisi wananchi ilikuwa ngumu kuamini vipi wao kiongozi mwenzao wa juu kabisa amekata moto hiyo ya kutangaza kifo chake on time kitoke wapi? kigogo alikuwa sawa sawi kabisa
 
Mkuu mimi sijui kipi ni cha kweli ila hata kama hayo madai ya akina kigogo ni ya kweli wewe wadhani angesema.
Bado unaamini tamko la waziri mkuu kuwa rais mzima anachapa kazi.
Kuna mambo mengine yanabaki kuwa siri tu siku zote.
Hivyo ukweli na uongo wanaujua wahusika
Kwani alikuwa hawezi kuzungumza? mbona alikuwa akizungumza mpaka siku ya mwisho? ka anazungumza alishindwa nini kuongea na simu na waziri mkuu na kumpa maelekezo? kumbuka afya ya Rais ni swala la ulinzi na usalama na hakuna viongozi waloruhusiwa kumuona isipokuwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Mimi na wewe tunachozungumza ndicho tulichoambiwa hivyo narudi pale pale ukweli na uongo wanaujua wao.
 
Kwanza hii stori imekuwaje imeletwa leo, 3yrs later?

Any form of intention?
Wanaweka rekodi sawa.

Unakumbuka kile kipisi cha gazeti kilichotoka tu mitandaoni the same day Jiwe kafariki?

Kile kipande kilichoonyesha Jiwe alikuwa na tatizo katika umeme wa moyo tangu miaka ya 80-90's akiwa mwanafunzi UDSM na ikawekwa account ya bank kumchangia pesa za kufanyiwa upasuaji nchini Uingereza?

Kile kigazeti na hii story hazina tofauti.

Waingereza husema" the end justifies the means".
 
Mtoa hoja usiwe mtu wa kuchagua habari unayoitaka wewe,President Magufuli wakati fighting for his life,PM alikuja public kusema kuwa yupo na afya njema na anaendelea kuchapa kazi,pia think out of box,President yupo critical ill,vice wake yupo Tanga for 5 days!,kimkoa ambacho mimi mwenyewe ninakimaliza kukitembelea kwa 2 days,PM yupo huko why hii itokee,cdf ni maoni yake take with a pich of salt
Maoni tena?
 
Mkuu ulitaka Generali wa Jeshi la JMT..Aende kinyume na Rais wa JMT ili kitokee nini?

Ulitaka atamka Tarehe tofauti na iliyokubalika na Serkali ili watanzania Wakose imani na Serkali? Halafu kitokee kitu gani?

Kuna Vitu huwa viko Ndani ya Kiapo mpaka unakufa na kama ni Dhambi bhasi utakufanya nayo Ilu kulinda Maslahi ya Serkali iliyopo madarakani
Ameyasahau ya Job Ndugai yaliyomtokea?
 
Tumemsikia Mkuu wa Majeshi Mstaafu Generali Mabeyo akisimulia hivi karibuni jinsi Magufuli alivyouguzwa hadi kufariki.

Katika maelezo yake, Generali anadhihirisha kuwa Magufuli alifariki tarehe na muda uliotajwa na Mhe. Samia alipokuwa akitangaza kifo hicho.
CDF sio mamlaka halali ya kuondoa utata wa nini haswa kilichotokea!. Mabandiko yangu haya mawili Japo sio lazima kuhoji kila kitu kwa kuuliza maswali lakini mtu mwenye akili zake timamu ni lazima ajiulize. Ukimya wetu, msitufanye mazuzu kuna...

Bado yako very valid!.
P
 
Mbaya zaidi Chahali akadai kuwa Zitto Kabwe alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Mhe. Samia kuapishwa kuwa Rais akidai kuwa kuna baadhi ya viongozi walitaka asiapishwe.

Lakini Generali anaonesha kuwa hakukuwa na changamoto ya namna hiyo. Hata kama ingekuwepo wasingemtafuta Zitto atoe ushauri.
Zitto ni nani
Ana mamlaka gani ndani ya serikali
Yeye mwenyewe anasemaje
 
Back
Top Bottom