Ifunda tech secondary school ya chomwa moto

Ifunda tech secondary school ya chomwa moto

I loved this school hapo zamani ila sasa nimepoteza upendo huo

ilikuwa ni shule nzuri ya mchanganyiko wa jinsia na wanafunzi kutoka mikoa yote waliofaulu vyema masomo ya sayansi na hesabu

ilikuwa na karakana,maktaba na maabara bora kwa kila idara zilizosheheni vifaa vyote muhimu

ilikuwa na walimu magwiji kutoka ndani na nje kama urusi na uholanzi

ilikuwa na majengo mazuri yaliyosambaa kuanzia kwa shabu,mkwawa,mirambo,chabruma,seuta, mpaka kwa singa

walimu walikuwa katika makazi bora yanayofanana na nyumba za serikali za oysterbay

mazingira ya uoto wa kijani na miti mingi ya hali ya hewa safi

Ukumbi wa mazengo na viwanja vya michezo....aah

wahitimu makini walioendelea DIT(DTC) na Arusha Tech

INASIKITISHA ifunda kuwa na migogoro ya kuchoma ofisi na wanafunzi kuvaa barghashia darasani
 
Kwa ninavyofahamu kila shule huwa ina sefa kwa ajili ya vyeti vya wanafunzi. Itashangaza sana ukiniambia vyeti pia vimeungua. Ina maana huwa vinawekwa kwenye kabati?

fire proof safe for every school? Kaka unaongelea U.S. au wap!
 
ukifuatilia sana utakuta ni wanafunzi wamebanwa na mwalimu wa nidhamu au wanadai ratiba ya kupikiwa wali
 
itakuwa ni hitilafu ya umeme tu. nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati nasoma pale nyumba ya mwalimu iliungua mpaka jivu kwa hitilafu ya umeme tena iliyosababishwa na uzembe wa mhusika. alafu ile ni shule ya ufundi mara zote kukiwa na tatizo lolote la umeme mwalimu wa umeme na wanafunzi ndo huwa wanarekebisha hata kama walitakiwa kwenda tanesco na actually mara nying wanafunzi wanakuwa pekeyao.
 
Kwa ninavyofahamu kila shule
huwa ina sefa kwa ajili ya vyeti vya wanafunzi. Itashangaza sana
ukiniambia vyeti pia vimeungua. Ina maana huwa vinawekwa kwenye
kabati?

Uchelewi kusikia CDM, ndo mamepanga njama za uchomaji moto...
 
daaa .. so sad. Usikute madogo ndo wameteketekeza kwasababu ya ishu zao na walimu/uongozi wa shule!
 
Dah...imenikumbusha baadhi ya maneno katika wimbo wa shule!

Ifunda the glorious,
Technical School,
Live Long Forever,

With Our Motto..."Skills and Efficiency"..and Our School
Shall Shine Forever More,

Oooh, God Bless Our School
 
Nawakumbuka waalimu wangu kajembura, raphael(part time), luwahgo, kiwale, makyandu, luanda, kaguo,mruma, salwat, mnaroma, chota, narimi na wengineo poleni sana.
 
Ule ugomvi wa jamaa waliodai wanataka kuruhusiwa wavae barakashia uliisha kweli? Hawa jamaa inabidi wapewe dunia yao kama Pakistan
 
fire proof safe for every school? Kaka unaongelea U.S. au wap!
Wewe unaishi wapi? Labda kama unaongelea shule hizi za Kata. Lakini kama ni shule za sekondari za zamani zote zina ama safe halisi na ambayo wenye uwezo wa kuifungua ni mkuu wa shule na mtaaluma tu. Hiyo safe hawezi kufungua mtaaluma peke yake au mkuu wa shule peke yake. Ni lazima wawepo wote. Na ukienda kuchukua cheti ukakuta mmojawapo hayupo, hupati. Kwa vyuo nashule zilizo nyingi ambazo hazina safe halisi wameijenga kwa tofali na kutengeneza mlango wa chuma. Kama wewe hujaona hili basi una bahati mbaya. Mimi ni mwalimu na shuleni kwetu tunayo hiyo.
 
Nawakumbuka waalimu wangu kajembura, raphael(part time), luwahgo, kiwale, makyandu, luanda, kaguo,mruma, salwat, mnaroma, chota, narimi na wengineo poleni sana.

daa part time alifariki,luwago ni headmaster mtwivila sekondari.wengi walihama.umenifanya nimmic part time kwenye engineering science
 
hahahaaa umenikumbusha mbali sana aisee.da ila nimesikitika kwa kweli.

R.I.P office
Inasikitisha sana. Kama imechomwa kwa makusudi, najaribu kufikiria lengo la mchomaji lilikuwa ni lipi? Kumbe na wewe umepita pale rafiki?
 
Kwa ninavyofahamu kila shule huwa ina sefa kwa ajili ya vyeti vya wanafunzi. Itashangaza sana ukiniambia vyeti pia vimeungua. Ina maana huwa vinawekwa kwenye kabati?

Huo ndio ukweli kwa shule zote kongwe za sekondari, sijui tu kuhusu hizi shule za kata.
 
masikini Ifunda.mimi nilidhani ni msitu wa ndovu umeungua,au kule lyandembera.kumbe ni katika ofisi inayotunza nyaraka muhimu za UNGA wa watu.duh!sasa si na ofisi za jirani nazo zimeungua?kama ya mkuu wa shule na ya barsa?jamani.so sad.ule mpango wa kila shule na vyuo kuwa na magari ya kuzimia moto ulifia wapi?agizo hilo lilitolewa na kiongozi mkubwa tu wa nchi wakati ule wa mioto ya shule ya shaulitanga.
 
Labda wanataka ajengo mampya kama ilivyotokea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma
 
Usiku wa kuamkia jumapili tar 7 april watu wasiojulikana wamechoma moto ofisi ya taaluma hapo shuleni na kuteketeza kabisa kila kitu. Hakuna kilicho okolewa. Hasara ni kubwa sana zaidi ya mamilioni. Vyeti ya wahitimu form four na form six, vitabu na nyaraka muhimu navyo vyote vimeteketea



Na iyo ndo ofisi iliyoteketea kwa moto
 

Attachments

  • 563737_10200988752387939_95112334_n.jpg
    563737_10200988752387939_95112334_n.jpg
    125.1 KB · Views: 70
  • 575696_10200988744307737_182361372_n.jpg
    575696_10200988744307737_182361372_n.jpg
    25.6 KB · Views: 70
Hizi ni akili finyu sana. Huwezi kuangamiza mali ya umma kwa lengo la kumkomoa mtu au watu huku ukijua nawe ni mmiliki wa mali hiyo.Hawajui kuwa baada ya miaka mitano au kumi watoto wao au ndugu zao watapelekwa kusoma pale kukiwa hakuna miundo mbinu. Hapa ni sawa na kukata tawi la mti huku ukiwa umelikalia!
 
Back
Top Bottom