Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 7,875
- 12,665
Ni muhimu kuwafunza waliokatika miliki yako maadili mema kuanzia watoto wako, wadogo zako, ndugu wa karibu pamoja na majirani mnaoishi kwa kushirikiana shughuli za kila siku, kila mtu akifanya hivyo katika eneo analoishi jamii nzima itakuwa na maadili mema na yanayofaa katika jamii na taifa kwa ujumla
Kila mtu ana akili ya kutambua kizuri na kibaya, kinachofaa na kisichofaa hata bila ya kutumia sheria za kidini wala sheria za nchi sasa kuna watakaosema kuwa jamii ya watanzania hatuna maadili maalum au utamaduni maalum wa kufuata jibu rahisi ni kuwa wewe kama mtu mwenye akili una uwezo binafsi wa kuchambua jema na baya bila kupangiwa na dini wala watunga sheria za nchi tofauti na mnyama hivyo jipangie utaratibu wa maisha ulio bora
Kwa ufupi sana maadili mema yanapimwa kupitia uvaaji, uongeaji, ushiriki wa shughuli za kijamii kama vile uongozi bora, uaminifu, heshima, uadilifu na uwajibikaji.
Pia kufanya vitendo vilivyo vyema na kuepuka vitendo viovu kama vile ubakaji, ulawiti, ukahaba na umalaya, matusi na maneno machafu, uvutaji bangi na midaharati, ushoga na usagaji, nyimbo na michezo isiyofaa yenye kutweza utu au kudhalilisha na mambo mengine mengi yasiyofaa
Kila mtu akifanya hivyo kwenye familia yake na watu wanaomzunguuka tutaweza kujenga taifa bora lenye kizazi bora na cha kuigwa hivyo kuleta ustawi wa kijamii na kitaifa kwa ujumla
Nawasilisha