"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Mimi mwenzenu, japo ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, ila pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea pia kwa kujitolea, nimehudumu kwenye sekta ya habari kwa takriban zaidi ya miaka 30, hivyo jicho langu limeona mengi, linaona mengi, na litaendelea kuona mengi, hivyo kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi zinazo kwenda kwa jina la Kwa Maslahi ya Taifa zenye maswali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, kisha majibu utayatoa wewe mwenyewe msomaji!.

Angalizo.
Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo muhimu!, hili ni bandiko la swali na sio bandiko la statement!. "Hii IGA ya DPW imetusaidia sana Watanzania kujitambua!, kumbe tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa kutosha!, lakini at the same time, pia tuna wanasheria vilaza wa ajabu sana!". Swali ni Je Bunge letu nalo, licha kushehenezwa na wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu nalo pia ni Bunge la ajabu?, linawezaje kupitisha na kuridhia vitu vya ajabu ajabu sana kama hii IGA ya DPW?. Na Serikali yetu pia, licha ya kuwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, jee nayo pia ni Serikali ya Ajabu?, hii IGA ya ajabu hivi ya DPW ilipita pita vipi kote huko ikiwa na vipengele so defective kisheria hata kwa Mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa kwanza, vipengele vya hii IGA viliwezaje kupitishwa bila kuwa noted or detected na hii IGA ika sail through serikalini undetected na sasa ime sail through Bungeni the same?!. What type of HGA tunayo anticipates kutokana na IGA ya kihivi?.

Umuhimu wa Angalizo
Umuhimu wa angalizo hili ni mimi mwenzenu huko nyuma niliwahi kuandika makala fulani kuulizia jambo fulani, HAPA na HAPA Mhe. Mbunge kilaza mmoja, HAPA akaisoma makala yangu bila kuiona ile alama ya kuuliza na kunituhumu kuwa nimetoa statement fulani, akanishitaki kwa Spika, nikaitwa Dodoma kuhojiwa mbele ya kamati fulani!, HAPA nikaitika wito, nilipowaonyesha ile alama ya kuuliza, kesi ile iliishia pale!, hivyo sitaki tena kuandika kitu kisha nikaitwa kujieleza popote ndio maana natoa angalizo hili mapema kabisa, hapa sijatoa statement yoyote ni nimeuliza tuu maswali!.

Mjadala wa IGA ya DPW na Bandari zetu bado umeshika kasi, huku ukijadiliwa kwenye fronts mbili kuu, front ya kwanza ni mijadala ya kisiasa, kwa wanasiasa mbalimbali kujitokeza kutoa hoja zao za kisiasa kwa kuita waandishi wa habari.

Front ya pili ni mijadala ya kisheria kwa wanasheria mbalimbali kujitokeza kutoa maoni yao ya hoja za kisheria, wakiongozwa na maoni ya Chama cha Mawakili Tannganyika, TLS, wakiwemo wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kama Prof. Issa Shivji, Dr. Rugemeleza Nshala, Jaji Joseph Sinde Warioba, Tundu Lissu na wanasheria mbalimbali.

Wale wenye fedha zao, wataita waandishi ukumbi wa hoteli fulani na kuwakirimu waandishi wa habari, na wale wenzangu na mimi, akina Apeche Alolo, ama watawaita waandishi majumbani mwao, au kutoa maoni yao kupitia Club House.

Tangu sakata hili la IGA ya DPW liibuke, mimi msimamo wangu ni ule ule haujawahi kuyumba, kama tumeshindwa kuiendesha Bandari yetu kwa ufanisi, hivyo hakuna ubaya wowote kusaidiwa! HAPA

Nikasisitiza kitu kilichohitajika ni uelimishaji umma na ushirikishwaji wa Watanzania, mambo ambayo hayakufanyika watu wakaona tuu MoU zinasainiwa Dubai wakati wa Expo Dubai ile February 2022, IGA ikasainiwa kimya kimya October 2022, kisha kuletwa Bungeni kuridhiwa June 2023!. Hizi kelele za Watanzania kulalamikia IGA, mimi zikanishangaza HAPA

Juzi Ijumaa, Jukwaa la Wahariri wakawaalika wahusika wakuu wa IGA ile wakiongozwa na Waziri husika, akiandamana na wanasheria kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali, ndipo nami kwavile pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nikashuhudia ukilaza wa ajabu kabisa kwenye tasnia yetu ya sheria!. Hii IGA imechambuliwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kama TLS, Prof. Shivji, Prof. Anna Tibaijuka, Dr. Rugemeleza Nshala, na wengine wengi, ikakutwa ina matatizo lukuki, huku TLS wakiainisha kifungu kwa kifungu na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua, kwenye timu ya TLS, ilijumuisha Mwanasheria nguli number moja Tanzania wa Investment law, Dr. Hawa Senare, ambaye ni pia ni mhadhiri wa sheria, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu serikali wanatuletea wanasheria wa kawaida tuu kuja kujibu hoja nzito za kisheria!.

Majibu mepesi ya wanasheria hawa wa Government Team, yamepelekea akina sisi watu wa kuhoji, ku search majina yao kwenye mtandao wa TLS, wengine majina yao hayapo!. Hili la serikali kutuletea wanasheria wanaotoa majibu mepesi kwenye hoja za kisheria kumepelekea wanasheria hawa kuonekana kama vilaza fulani, na kitendo cha majina yao kutoonekana kwenye list ya wanasheria wanaotambulika rasmi, inawezekana hawa ni miongoni mwa wale wanasheria makaratasi, waliofeli LST, wala sio mawakili, inawezekaje mtu asiyetambuliwa na TLS kutuongozea timu za majadiliano ya government negotiation team ya hii IGA?!, unategemea nini?!. ( Hapa naomba mliosoma na wanasheria hawa kwenye LL.B, mjitokeze kututhibitishia hawa ni wahitimu kweli wa sheria, maana usije kuta tuna watu fake wamejipenyeza!).

Sasa Wanasheria hawa anaonekana kama vilaza fulani, wanapoibuka na kusema hii IGA ni safi, nzuri na haina matatizo yoyote!, hii ni kumaanisha, TLS na wanasheria manguli wote wanaosema hii IGA ni matatizo, ndio vilaza?!...kweli?!.

Mimi nami kama mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nikatoa maoni yangu HAPA

Kule nyuma niliwahi kuuliza Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?, sasa ndio naanza kupata majibu, inawezekana kabisa Tanzania tuko hapa tulipo kwasababu ya wanasheria wa type hii, serikali yetu inaonekana ni serikali ya ajabu kwasababu ya wanasheria wa type hii!, na Bunge letu inaonekana ni Bunge la ajabu kwasababu ya wabunge wa type hii!.

Wakati wa kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar ile mwaka 1984, kulikomuondoa Abdul Jumbe aliyekuwa rais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Ali Hassan Mwinyi, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo!, aliwahi kusema, "Wanasheria ni watu wabaya sana" sikumbuki alimaliziaje, ila kwenye hilo sakata, aliyeshughulikiwa, sio rais wa Zanzibar pekee, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wa wakati huo, Wolfgang Dourado, pia alishughulikiwa kikamilifu!.

Wakati wa Bunge la Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, ambaye sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, kwa jina maarufu la OMO, naye alileta za kuleta kule Dodoma, wakati wa upigaji kura kupitisha katiba pendekezwa. Sisi washauri wa bure tukashauri Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Kwenye hili sakata la IGA ya DPW, mimi naungana na Baba wa taifa kwa kusema "Wanasheria vilaza ni watu wabaya na hatari sana kwa taifa letu!".

Ni wanasheria hawa ndio wametufikisha hapa kwenye hili la hii IGA ya DPW!, wanasheria ndio the source ya mikataba yote mibovu and in fact ni wanasheria ndio the source of katiba hii mbovu iliyopo ambayo licha ya kuwa ni katiba mbovu, pia imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili HAPA

Kwa hoja hizo, hakuna ubishi kuwa tuna wanasheria vilaza wa ajabu!, swali sasa jee serikali yetu pia ni serikali ya ajabu?, na Bunge letu Tukufu pia ni Bunge la ajabu kupitisha mambo ya ajabu ajabu?.
Hitimisho
Nimalizie kwa wanasheria wetu na wanasheria wenzangu. Prof. Shivji anasema hii IGA ina matatizo, TLS wanaainisha kabisa vifungu, halafu wewe mwanasheria kinda, unaibuka na kusema hii IGA ni safi na haina matatizo!, with all illegality nilio ainisha hapa, bado unathubutu kuibuka na kusema hii IGA ni safi na haina matatizo?.

Leo nimeandika makala kwenye gazeti la Nipashe, kwa kutoa rai kwa serikali, kuzijibu kisheria hoja za kisheria na tuufunge huu mjadala

Uzalendo wa kweli ni nia ya dhati kuisaidia nchi yako, kumsaidia rais wako, kuisaidia serikali yako, unapona jambo halijakaa vizuri, unakosoa na kushauri the right thing to do. Mimi nimekosoa na pia nimeshauri kuwa hata kama hii IGA ni tunabakwa, Mwanamke mgumba akibakwa, akapata ujauzito, atampenda mbakaji! Wajua Kuna Ndoa Halali, Batili na Batilifu?. Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji?. Wajua Ubakaji unaweza kuwa Halali?. IGA Batili Yaweza kuzaa HGA Halali?.
A Way Forward.
  1. First and foremost serikali ijibu kisheria hoja zote za kisheria zilizoibuliwa kupinga hii IGA, na sio kujibu hoja za kisheria kwa majibu ya kisiasa.
  2. Kwa vile hii sii mara ya kwanza, tumetunga sheria ipo halafu serikali yetu inatuletea mikataba kinyume cha sheria!, kama tumeona sheria hazifai, tuzibadili kwanza sheria ndipo tuingie mikataba!.
  3. Kwa vile hii IGA imeisha sainiwa na kuridhiwa na Bunge letu, hii maana yake ni HGA inafuata. Nashauri hiyo HGA iwe as transparent as hii IGA ili tuone maoni ya wananchi yamejumuishwa.
  4. Imeelezwa itaundwa kampuni ya ubia na itasajiliwa Tanzania, kisha 35% shares zitakuwa floated for public. Hizo shares zikiuzwa kupitia soko la hisa, DSE, then watu wenye the purchasing power ni wale wale matajiri, nashauri hizo shares zihodhiwe na mifuko ya hifadhi za jamii ya NSSF na PSSSF, ili waitumie faida kuanzisha hifadhi ya jamii kwa wote.
  5. Tubadili sheria zetu, mikataba yote ya rasilimali za taifa iidhinishwe na Bunge na sio kuridhiwa tuu.
  6. Bunge letu libadilike, liache kuwa ni Bunge rubber stamp la kupitisha tuu kitutusa kila kinacholetwa na serikali yetu mbele yake!. Sometimes serikali yetu inafanya madudu ! sasa Bunge linapoletewa madudu kama hili dubwana, au dubwasha na kulipitisha kitutusa, Bunge letu litakuwa na tofauti gani na Sultan Mangungo wa Msovero?.
  7. Bunge letu liache kuwa ni Bunge kibogoyo lisilo na meno!. Maadam sheria imelipa Bunge the power to review, then Bunge litimize wajibu wake kikamilifu!.
  8. Wanasheria, tuheshimiane, na kuheshimu professionalism na wanataaluma manguli wabobezi na wabobevu na kuheshimu maoni ya vyama vya kitaaluma, kama TLS, hii itazuia kuitana vilaza na mbululaz!.
  9. Kwangu mimi hii IGA ya DPW na Bandari yetu ni issue ndogo!, kuna ma issues makubwa, muhimu zaidi kama ubatili ndani ya katiba yetu unaonyima haki Watanzania, watu wako kimya!, halafu issue ndogo hii ya Bandari kelele mpaka karibu mbinguni!.
  10. Nimalizie kwa lile swali la msingi la bandiko hili kuwa hii IGA ya DPW imetusaidia sana Watanzania kujitambua!, kumbe tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa kutosha!, lakini at the same time, pia tuna wanasheria vilaza wa ajabu sana!. Swali ni Je Bunge letu nalo pia ni Bunge la ajabu? na Serikali yetu pia ni Serikali ya Ajabu?, hii IGA ya DPW ilipita pita vipi kote huko ikiwa na vipengele so defective bila kuwa noted?!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
 
Pascal wewe hueleweki. Mimi huwa sikuamini! Ukiitwa kuteuliwa huwezi kuwa na msimamo......umesaka kuteuliwa muda mrefu. Kama ukatili wa magufuli wooote uliuunga mkono, hupashwi kuaminiwa. SAWA NA DR SLAA, SIWEZI KUMWAMINI KATU! HANA ANALOLISIMAMIA NI TUMBO. ANAPIGA KELEL SASA AKIPEWA UBALOZI ANGEUKA , MSIMWAMINI
 
Wewe unawaamini wachagga wenzako tu 😃
 
Halafu badala ya kujibu hoja kwa hoja wa vipengele wao wanajibu kisiasa tu...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Pascal Mayalla wanasheria kwasababu umeona hawana cha kukufanya ndio umewaita vilaza, lakini bunge lililowahi kukuita na kukuhoji unaliogopa huku ukijua fika nalo limejaa vilaza wa kutisha, kuanzia na Spika, akifuatiwa na kina Musukuma, serikali inayoongozwa na kilaza namba moja nayo umeogopa kuitaja kwasababu bado unategemea kupata chochote toka kwake..
 
Paskali, jana usiku ulipata Whiskey...umemsikia Tulia? anakataza watu ambao hawajawahi kuagiza fulana wasiongee kuhusu bandari
 
Umemuuelezea vema kabisa, see also post #3 . asante sana

Hakumtaja samia ambaye anabariki upuuzi, wala hajaisema CCM inayoongoza huu upuuzi wala, bunge ambalo ni kikundi cha mchiriku....... anawashambulia mawakili, tena bila kuwataja nani walishiriki...
 
Itoshe kusema tuna taifa la ajabu sana
 
Sasa umekuwa P ninayemjua umeongea kwa Hoja nzuri sana Mungu akubariki
 
 
Leo nimeanza kumwona yule Mayala wa enzi za JK.

Sent from my Infinix X689F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…