Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa zenye maswali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, kisha majibu utayatoa wewe mwenyewe!.
Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo!, hili ni bandiko la swali na sio bandiko la statement!. "Hii IGA ya DPW imetusaidia sana Watanzania kujitambua!, kumbe tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa kutosha!, lakini at the same time, pia tuna wanasheria vilaza wa ajabu sana!". Swali ni Je Bunge letu nalo, lucha kushehenezwa na wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu pia ni Bunge la ajabu? na Serikali yetu pia, licha ya kuwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, nayo ni Serikali ya Ajabu?, hii IGA ya ajabu hivi ya DPW ilipita pita vipi kote huko ikiwa na vipengele so defective bila kuwa noted or detected na ika sail through?!.
Umuhimu wa angalizo hili ni mimi mwenzenu huko nyuma niliwahi kuandika makala fulani kuulizia jambo fulani, Mhe. Mbunge kilaza mmoja, akaisoma makala yangu bila kuiona ile alama ya kuuliza na kunituhumu kuwa nimetoa statement fulani, akanishitaki kwa Spika, nikaitwa Dodoma kuhojiwa mbele ya kamati fulani!, nikaitika wito, nilipowaonyesha ile alama ya kuuliza, kesi ile iliishia pale!, hivyo sitaki tena kuandika kitu kisha nikaitwa kujieleza popote ndio maana natoa angalizo hili mapema kabisa, hapa sijatoa statement yoyote ni nimeuliza tuu maswali!.
Mjadala wa IGA ya DPW na Bandari zetu bado umeshika kasi, huku ukijadiliwa kwenye fronts mbili kuu, front ya kwanza ni mijadala ya kisiasa, kwa wanasiasa mbalimbali kujitokeza kutoa hoja zao za kisiasa kwa kuita waandishi wa habari.
Front ya pili ni mijadala ya kisheria kwa wanasheria mbalimbali kujitokeza kutoa maoni yao ya kisheria, wakiongozwa na maoni ya Chama cha Wakili Tannganyika, TLS, wakiwemo wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kama Prof. Issa Shivji, Dr. Rugemeleza Nshala, Jaji Sinde Warioba, Tundu Lissu na wanasheria mbalimbali
Wale wenye fedha zao, wataita waandishi ukumbi wa hoteli fulani na kuwakirimu waandishi wa habari, na wale wenzangu na mimi, akina Apeche Alolo, ama watawaita waandishi majumbani mwao, au kutoa maoni yao kupitia Club House.
Tangu sakata hili la IGA ya DPW liibuke, mimi msimamo wangu ni ule ule haujawahi kuyumba kwa tumeshindwa kuiendesha Bandari yetu kwa ufanisi, hivyo hakuna ubaya wowote kusaidiwa!.
Nikasisitiza kitu kilichohitajika ni uelimishaji umma na ushirikishwaji wa Watanzania, mambo ambayo hayakufanyika watu wakaona tuu MoU zinasainiwa Dubai wakati wa Expo Dubai ile February 2022, IGA ikasainiwa kimya kimya October 2022, kisha kuletwa Bungeni kuridhiwa June 2023!.
Juzi Ijumaa, Jukwaa la Wahariri wakawaalika wahusika wakuu wa IGA ile wakiongozwa na Waziri husika, akiandamana na wanasheria kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali, ndipo nami kwavile pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nikashuhudia ukilaza wa ajabu kabisa kwenye tasnia yetu ya sheria!. Hii IGA imechambuliwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kama TLS, na Prof. Shivji, Dr. Rugemeleza Nshala, ikakutwa ina matatizo lukuki, halafu wanatuletea wanasheria vilaza tuu waliofeli LST, hivyo wala sio mawakili, kutuongozea majadiliano ya hii IGA, wanaibuka na kusema hii IGA ni nzuri na haina matatizo yoyote!, kweli?!.
Kule nyuma niliwahi kuuliza
sasa ndio naanza kupata majibu, inawezekana kabisa Tanzania tuko hapa tulipo kwasababu ya wanasheria wa type hii, serikali yetu inaonekana ni serikali ya ajabu kwasababu ya wanasheria wa type hii!, na Bunge letu inaonekana ni Bunge la ajabu kwasababu ya wabunge wa type hii!.
Wakati wa kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar ile mwaka 1984, kulikomuondoa Abdul Jumbe aliyekuwa rais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Idris Abdul Wakili, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema, "Wanasheria ni watu wabaya sana" sikumbuki alimaliziaje, ila kwenye hili sakata la IGA ya DPW, mimi naungana na Baba wa taifa kwa kusema "Wanasheria Vilaza ni Watu Wabaya Sana", ndio wametufikisha hapa kwenye hili la hii IGA ya DPW!.
- Naomba nianze na Serikali yetu inajua kabisa kuwa Bandari ina falls kwenye sheria hii iliwazaje kuruhusu hii IGA yenye vipengele vinavyokwenda kinyume cha sheria zetu?.
- Sheria ikiishapitishwa ni ipo, kupitisha jambo lolote linanalokwenda kinyume cha sheria iliyopo, jambo hilo ni illegality, hivyo hii IGA hapo ilipo it's illegal!.
- Jambo ambalo lingepaswa kufanyika ni kwa serikali yetu kubadili kwanza sheria zetu kisha ndio kuipitisha hii IGA!.
- Kwenye hii IGA, serikali yetu imeingia makubaliano na Dubai, ambayo sio sovereign, kukitokea mgogoro wa kushitaki kimataifa, Tanzania tunaweza kushitakiwa kwa international instruments, kwasababu Tanzania ni member wa Geneva Convention, lakini kama DPW ndio watatukosea, Tanzania tutawashitaki wapi wakati Dubai sio member wa Geneva Convention, member kule ni UAE!. Kwenye ile IGA, hakuna popote UAE, imetoa Power of Attorney kwa Dubai!, hivyo Tanzania kama nchi, tumeingia mkataba na an entity which has no capacity to contract a treaty!. DPW wangesainiana tuu na TPA na kumalizana juu kwa juu!.
- Ile 2017 wakati tunapitisha sheria hii, mimi niliuliza humu humu kuwa Tanzania tutaweza?.
- Sasa nije kwa Bunge letu Tukufu, kwanye mikataba ya kimataifa, international treaties, the role of Bunge ni kuridhia tuu, yaani ratification, kui ratify ili kui domesticate kuwa sehemu ya sheria zetu.
- Hiki ndicho Bunge letu Tukufu limekifanya kwenye hii IGA!. Sasa uliita Bunge letu hili ni Bunge la vilaza, utakuwa unalionea?.
- Lilichofanya Bunge letu ni ku rubber stamp tuu hii IGA!, ukiliita Bunge letu Tukufu ni Bunge rubber stamp utakuwa unalionea?!.
- Kwa mujibu wa sheria hii, the role of Bunge sio ratification na ku rubber stamp, the role of Bunge ni ku revives na kutoa mapendekezo!.
- Kabla waheshimiwa wabunge wetu kujadili mkataba huu, sisi washauri wa bure tuliwashauri kabla!. Kwa vile walifanya kinyume, tuna haki ya kuwabalasa!.
- Hii sio mara ya kwanza kwa Bunge letu kupitisha vitu vya ajabu ajabu kitutusa!. Kwenye ule mgogoro wa CAG, Prof.Assad, Bunge letu lilipitisha Azimio batili, nikawaambia Azimio lile ni batili, Bunge wakakomaa wakapitisha kwa mbwembwe!.
- Baada ya kupitisha nikawaeleza kuwa ni lazima waipokee ripoti ya CAG wasipoipokea Bunge linavunjwa!.
- Ndipo lile Azimio lao batili wakaliondoa kimya kimya na wakaipokea Ripoti ya CAG kimya kimya!. Sasa Bunge la aina hii ukiliita Bunge full of vilazaz kwa lugha ya rafiki yangu Le Mutuz (RIP) Bunge la mbululaz!, tutakuwa tunawaonea waheshimiwa wabunge wetu?.
- Nimalizie kwa wanasheria wetu na wanasheria wenzangu. Prof. Shivji anasema hii IGA ina matatizo, TLS wanaainisha kabisa vifungu, halafu wewe mwanasheria kinda, unaibuka na kusema hii IGA ni safi na haina matatizo, with all illegality nilio ainisha hapa, bado unathubutu kuibuka na kusema hii IGA ni safi na haina matatizo?.
- Leo nimeandika makala kwenye gazeti la Nipashe, kwa kutoa rai kwa serikali, kuzijibu kisheria hoja za kisheria na tuufunge huu mjadala
Hitimisho
Uzalendo wa kweli ni nia ya dhati kuisaidia nchi yako, kumsaidia rais wako, kuisaidia serikali yako, unapona jambo halijakaa vizuri, unakosoa na kushauri the right thing to do. Mimi nimekosoa na pia nimeshauri. Nimalizie kwa lile swali la msingi la bandiko hili kuwa hii IGA ya DPW imetusaidia sana Watanzania kujitambua!, kumbe tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa kutosha!, lakini at the same time, pia tuna wanasheria vilaza wa ajabu sana!. Swali ni Je Bunge letu nalo pia ni Bunge la ajabu? na Serikali yetu pia ni Serikali ya Ajabu?, hii IGA ya DPW ilipita pita vipi kote huko ikiwa na vipengele so defective bila kuwa noted?!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.