"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

we hiyo critical thinking hata unajua maana yake. Hivi mpumbavu km wewe unaweza kumtahini profesa? We ni km ngedere tu umejaa wivu kwasababu huna uwezo wa kufikia level hizo utabaki kuzisikia kwa watu
Aliyejiita Docta wa uchumi Tz unamjua?

Knowledge
Understanding
Wisdom

Kutokana na majibu yako hivyo vitu 3 hapo juu waoneka huna
 
Weka mkataba wa marekani hapa nikuwekee wa tanganyika
 
We jamaa huwa hueleweki msimamo wako ni upi , nakushauri uwe unachukua mda kidog wa kutafakar kabla ya kuandika chochote, we s majuzi juzi ulikuwa chawa wa huu mkataba Leo tena unapiga U_turn
Hii Nchi in watu wa ajabu saana anafikiri tumesahau...yaani Uchawa Kwa Sasa ni Adui wetu no moja!
 
Mkuu Hatujui Jeshi Lipo Upande Gani.
 
1. Kwenye Legal aspect ya mkataba , Sisi tunawasikiliza TLS, Professor Shivji, Dr Nshala, Lissu, Mwabukusi, Madeleka

2. Kwenye economic aspect ya mkataba tunamsikiliza Professor Lipumba.

3. Kwenye social aspect ya mkataba tunamsikiliza Professor Tibaijuka

Kwa kuwa Manguli wote hao wamesema Mkataba huu una shida, basi una shida kweli na hatuutaki!
 
Ujumbe mkubwa ambao Samia anautuma Kwa vichwa ngumu ni
 
Paskali, jana usiku ulipata Whiskey...umemsikia Tulia? anakataza watu ambao hawajawahi kuagiza fulana wasiongee kuhusu bandari
Sasa naanza kuaminika pale juu akikaa Fulani na huku chini tutabadilika na kuwa kama Fulani. Lakini Pale Juu akilala Fulani na huku chini wengi tutatamani kulala kama Fulani!!!

Nipunguze sauti au niongeze?
 
Mindset kwa Sasa zipoje, na inatakiwa zibadilike ziwe za namna gani tofauti na Sasa hivi?

Tukiwa specific tutarahisisha maisha.
Za kijinga jinga zinawaza ujima na ujamaa badala ya kuwaza uchumi, Biashara na kukamatia fursa..

Mnawaza mambo ya kina Nyerere karne hii?
 
Za kijinga jinga zinawaza ujima na ujamaa badala ya kuwaza uchumi, Biashara na kukamatia fursa..

Mnawaza mambo ya kina Nyerere karne hii?
Mambo ya kina Nyerere yalikuwa ya Kijinga? Nipe kosa Hata moja la kijinga kijinga lililomo kwenye Azimio la Arusha(1967)! Mimi nikupe Lukuki yaliyomo kwenye Azimio la Zanzibar(1991/1992)

Sawa ujamaa unashida kwa mawazo yako, Na kujitegemea nako kuna shida? Yaani Dunia ya Leo unawaza kusaidiwa badala ya Kujitegemea na kuendesha mambo yako?

Hekima, Busara, na Uelewa wa Mambo ni nguzo muhimu katika kukabiliana na Changamoto. Yazingatie haya!
 
Naweza kukupa makosa hata elfu 1 ila nakupa mawili tuu kwanza ambalo ni starategic
1.Kutumia rasilimali Fedha na watu kwenda kupiganisha Nchi za watu Bure Bure Kwa kisingizio Cha undungu badala ya kutumia hizo pesa kuelimisha na kujenga Nchi Yako matokeo yake Tanzania imepitwa hata na hizo Nchi kama Zambia,Angola,Zimbabwe,Namibia South Africa nk..

Marekani na beberu hawafanyaji ujinga kama huo,unawasaidia Kwa makubaliano sio bure, Nyerere Hadi anaondoka hakuna shule hata Moja Wala hospital alijenza zaidi ya kutumia za Wakoloni ameacha watu na mavilaka , upuuzi.

Pili Mfumo wa uchumi wa ujamaa ni ujinga na uzembe mkubwa umejenga Taifa tegemezi na la walalamishi waliojaa woga,hofu ya mabadiliko na uliua vipawa huku ukiendesha mambo Kwa propaganda na vitisho..

Shida hizo ndio msingi Mkuu wa Umaskini na akili za kijinga za Watanzania Hadi keshokutwa..
 
Paskali... nadhani hints ni zile zile!
1. Poverty
2. Hunger
3. Poor education
4. Poor governance
5. Globalization
6. Greed
7. Elite capture
8. Resource curse
9. N.k
 
Kitaifa tutaendelea kuyumba kwa kudharau yafatayo:
1. Professionalism - kuheshimu na kuthamini utaalamu tulionao baada ya miaka 60+ ya uhuru. Wapo wengi na wakutosha na hivyo kujitegemea kitaaluma ambao wengine wametapakaa Dunia nzima. Baadhi yao walichoshwa na 'ubabaishaji' WA akili za ki-lumpeni kuhodhi mamlaka na uongozi. Mtaji WA kitaaluma, kiutawala (managerial skills) vyaweza kutumika kujikwamua .... vilaza na wababaishaji wabaki kwenye siasa za kibabaishaji
2. Sera ya ELIMU iondokane na kuendeleza ukilaza
3. Katiba Bora, ule UTI WA mgongo WA SHERIA zote .... ambayo haitatoa nafasi kwa kilaza yeyote na bangi zake hata kupenyeza kwenye UONGOZI na kuthubutu kuonesha ulevi wake.
4. Kuondokana na kukumbatia .... UARABU .... kwenye neno usta-arabu ... ATI sisi hatutoboi kwao. Wao ndo wenyewe. 'Slave mentality' hii huenda imetamalaki!
 
Kwa mfumo wetu wa uendeshaji nchi, chombo pekee chenye mamlaka ya kuukataa ni Bunge la JMT. Bunge ndio wawakilishi wa wananchi, hivyo kama Bunge limepitisha, hii IGA ni imepita!, sasa tunajiandaa kwa HGAs,
At this point or stage, hatuna tena uwezo wa kusema hatuutaki, kilichopo ni uwezo wa kuiboresha HGA!.

Hii IGA mbovu nimeitolea mfano wa Mwanamke mgumba aliyetamamani sana mtoto akakosa, akapigwa talaka kwa tatizo la ugumba, akawa ni mtu wa kutanga tanga. Siku moja katika kutanga tanga kwake, akatokea jamaa mmoja, akamsomba mzobe mzobe na kumpeleka kwake, akambaka usiku kucha!.

Asubuhi yule Mwanamke akashindwa kuondoka hapo kwa mbakaji, akajikuta japo amebakwa lakini angalau mbakaji ana mahali pa kulala!. Kuliko kutanganga tanga ni bora abaki kwa mbakaji!. Ikatokea ameshika ujauzito!. Do you know what happened?, Mwanamke yule alimpenda huyo mbakaji na kumpa mapenzi yote!.

Hii ndio the scenario ya hii IGA, Wajua Kuna Ndoa Halali, Batili na Batilifu?. Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji?. Wajua Ubakaji unaweza kuwa Halali?. IGA Batili Yaweza kuzaa HGA Halali?.
P
 
Acha kutukana wenzako ni vilaza ?....unataka wapoteze kazi sio ?

Kwa hoja hizo, hakuna ubishi kuwa tuna wanasheria vilaza wa ajabu, swali sasa jee serikali yetu pia ni serikali ya ajabu?, na Bunge letu Tukufu pia ni Bunge la ajabu
Ccm ndio chimbuko la huo Ukilaza, wao ndio tatizo hasa.
 
Weka mkataba wa marekani hapa nikuwekee wa tanganyika
Suala sio mkataba suala ni wapigaji wa hapo bandarini kusikitika wanapoona ulaji wao unawachomoka.

Kutoa kontena moja bandari ya Mombasa ni dola 1300 wakati kutoa kontena moja hapo TPA ni zaidi ya dola 3000.

Hiyo tofauti ya dola 1700 ndio chanzo cha maneno yote haya ya humu jamvini.

Ndio chanzo cha fitina na majungu mengi wanayofanyiwa wanasheria wa serikali mpaka muda huu.
 
Kwani mimi leo ni kivunja sheria nafanywaje? Waliokiuka sheria kwenye kusaini huu mkataba wapo na wanaendelea kutupiga kiswahili!
 
Aisee hadi mwili umesisimka, kwanza hongera kwa kutumia usomi wako kutuhabarisha pili kama mkataba ukiwekwa na ujinga mwingi kwenye IGA ! Basi kuna rushwa na upigaji upo na tunarudi kwenye mikataba kichefuchefu kama nishati na madini yaliyopita.
 
Shida kubwa ya azimio la Arusha .I dola kumiliki menejimenti ya njia kuu za Uchumi! Mengine yalikuwa safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…