"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Ficha ujinga wako, management ya bandari imeteuliwa na nani? kama kuna upigaji alaumiwe nani? kama wapigani weusi wenzenu mnawajua mnakaa kimya hao weupe mtawaweza? report ya CAG ni wizi mtupu ila mpaka November kujadiliwa bungeni ndio ujue hatupo serious kabisa kama nchi no wonder miaka zaidi ya 60 ya uhuru bado nchi ni masikini..
 
Karibia kunakucha endelea kukomaa, endelea kupanda.mbegu very soon utakula kivulini, mwaka hautaisha hujalamba teuzi, take it from me.
Hakulamba kipindi Cha Kaka yake ngosha, Badi asitegemee kipindi hiki Cha Wala halua
 
Pascal katika Ushauri wako hiyo No. Kuwa mikataba yote ihusiyo maliasili ilidhiwe Bungen, sheria ya mwaka 2017 inasema hivyo ila kwa bahati mbaya ndo wamepeleka amendment Bungen kuondoa hicho kifungu.
 

Jitahidi ndugu Mayor Quimby unapoandika usiisahau "h", kwani wakati mwingine unapoisahau "h" , sentensi yako inaweza leta maana tofauti.
"ata" ni "hata".
"aina" ni "haina".
"uyaelewi" ni "huyaelewi"

Ni kweli kwenye ile team ya Mbarawa,hakuna "kichwa" cha kuingia mkataba kama ulivyoandika.
 
binafsi nimegundua viongozi wetu ni Vilaza waliotukuka sana , ndio maana nchi ina mkwamo wa maendeleo sababu kubwa tumeongozwa na watu wenye uwezo mdogo kiakili miaka mingi tu toka uhuru,
Tatizo la msingi sana sana hili,na ndio chanzo cha kutokupiga hatua kimaendeleo.

Watanzania wakishakuwa viongozi,wanajiona wao ndio wana akili sana sana zaidi ya wote wasio viongozi.

Kama nchi lazima turudi kwenye "drawing board" kutengeneza mfumo bora wa kutengeneza viongozi.

Huwezi kuendelea kama huna "succession plan", iwe kifamilia, kibishara, kinchi.
 
Shida kubwa ya azimio la Arusha .I dola kumiliki menejimenti ya njia kuu za Uchumi! Mengine yalikuwa safi.
Mkuu, ongezea na hili, kwamba nyakati zile ilikua ni lazma kuanza STRICTLY. Mambo ya kina Kambona baadae kwa ujyaji wangu natafsiri kama ilikua ni dalili za mwanzo kabisa za subversion. Issue ikiwa kwamba, TUSITOBOE kamwe. Yote yanejianika leo hii. Rejea pia andiko la Prof. Chachage (RIP) .. mambo ya makuadi. Muhimu ni pia kwamba tukiendelea kulala CHALI tusitegemee kutoka shimoni. Tufika pahala tutawaliwe na mashoga kama IRELAND, LUXEMBOURG....
 
Hizi mbwembwe za wanaharakati zinawapotezea wafanyabiahara wa kweli, fursa ya mabadiliko ya kimaendeleo yanayotaka kufanywa na DPW hapo bandarini.

Wizi ni sehemu ya DNA ya mtanzania hakuna report ya CAG isiyojaa madudu ya wizi kila sekta, lakini hauondoi umuhimu wa kuwekeza na kuleta teknolojia za kisasa hapo bandarini.

Ni vita ngumu kwani kukosekana kwa mifumo imara ya kisasa mahali pale ni fursa ya kudumu ya wapigaji kuweza kutengeneza pesa.

Sishangai kuona wanaopinga uwekezaji wakija na mada nzito za mpaka kutishia kuivunja Tanzania, maslahi yao maovu yanapoguswa wanapiga kelele kwa lugha zote wanazozijua lakini mwisho wao upo karibu sana.
 
Stop beating around the bush Pascal! Tatizo ni muhimili uliojichimbia chini
 
Pascal wewe hueleweki.
Mkuu Retired , kwanza naheshimu mawazo yako. Muda wa unielewa utakapo wadia, utanielewa.
Mimi huwa sikuamini! Ukiitwa kuteuliwa huwezi kuwa na msimamo......
Naheshimu mawazo yako
umesaka kuteuliwa muda mrefu.
Sijawahi kusaka kuteuliwa hata mara moja!. Msaka teuzi hawezi kuwa critical!.
Kama ukatili wa magufuli wooote uliuunga mkono, hupashwi kuaminiwa.
Sijawahi kuunga mkono ukatili wa aina yoyote!.
  1. Kwanza ile 2014 ni mimi ndio niliwaeleza humu kuwa Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli humo kuna kitu nililisema!.​
  2. Baada ya uchaguzi Mkuu kabla matokeo hayajatangazwa rasmi, nilisema Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!
  3. Ni mimi ndiye the one and only who dared ask such questions Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli
Kuna popote nimeunga mkono?
SAWA NA DR SLAA, SIWEZI KUMWAMINI KATU! HANA ANALOLISIMAMIA NI TUMBO. ANAPIGA KELEL SASA AKIPEWA UBALOZI ANGEUKA , MSIMWAMINI
Naheshimu mawazo yako
P.
 
Umekengeuka! Ungelijua kabila langu ungekwenda kutubu kanisani! Au mnatubu kwa shetani wewe na Jiwe
Kuna makabila mapya kama lile la mafisadi, wapambe, vilaza nk. Maendeleo ya kiteknolojia na uchumi yanaondoa mipaka ya asili ya makabila
 
Kwa heshima kabisa, kuna.kitu tunakichanganya kwenye hii IGA ya DPW. Vitu hivyo ni muundo/viwango na maudhui. Nitaelezea.

Kwa ufupi sana;
Baada ya kuisoma na kuisoma tena hii IGA ya DPW binafsi nimegundua haina hiyo illegality inayoongewa na wengi w sisi wanasheria (mawakili) kwakuwa inafikia vigezo vyote vya mkataba kimuundo/kiviwango.

Sasa tatizo lilipo ni wapi?
Wengi wa wanasheria (mawakili) wanachanganya sana suala la yale waliyokubaliana pande mbili na misingi ya kisheria. Ukweli ni kuwa kwenye makubaliano yaani kile tulichokubaliana Jamhuri ya Muungano ya Tanzania tulikosa watu wakuweza kubargain hii kitu kwa jicho la maslahi ya taifa yajayo.

Sijaeleweka;
Nitatoa mfano, ni sawa na kuwa gari linauzwa alafu mnunuzi amekuja na pesa milioni 10 lakini thamani halisi ni milioni 5 na akanunua kwa milioni 12. Halafu baadaye wakatokea ndugu na marafiki wakamwambia ule mkataba wa kuuziana gari una illegality kisa kauziwa gari la milioni 5 kwa milioni 12.

Ndicho kilichopo kwenye IGA ya DPW tulikosa watu wakupambania maslahi ya Taifa ndani ya makubaliano hayo. Na hili siwezi kutupa lawama kwa wanasheria wa serikali waliohusika bali lawama naweza kuzitupa kwa Bunge la Jamhuri pia.

Mimi ni hayo tu kwa sasa.
 
Pasal wewe ni figure "kubwa". Umeandika muda mrefu na kujijengea jina kubwa.

Nikueleza ukweli...umekuja kukengeuka wakati wa Magufuli na ulipoitwa na bunge. Ulitishwa na ukatishika na kugeuka nyuma ukawa Jiwe. Afadhali ungelinyamaza kuliko kukengeuka na kubadili msimamo!
Mama Tanzania Mbatia, baada ya kunyanganywa chama na Mutungi, amekaa kimya lakini hakukengeuka!

Finally, we angalia wanavyokuandika hapa JF, kila mmoja anasema you were smart huko nyuma, not today
Nakukumbuka sana toka nyuma ulipokuwa MC pale Peakcock Hotel harusi ya akina Malinzi! I was there!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…