IGP Kenya Maandamano yamemng'oa Ofisini. Wakwetu matukio ya utekaji yatamng'oa lini?

Kwa Wadanganyika na Uchawa wao haitakaa itokee kamwe
 
Afghanistan wana njaa kali ns umaskini, sijui kuhusu exposure ya elimu, akiachia ngazi atakufa njaa..bora fedhea lkn tumbo lishibe..aibu sana..yale mavi-8 unafikiri mchezo mzee??
 
Tena wa Kenya ni mwajiriwa ameamua kabisa aache mshahara mnono na machichiri kibao..nchi kwanza.Wa hapa bongo ni kupe mpaka labda mteule wake aamue.Ukipiga kelele sana na wewe unatekwa.
 
Tanzania sio Kenya. Hapa mtu ukiambiwa usifanye na ukafanya, UTAPIGWA TU. Nami nasema, WAPIGWE TU.
 
Huyu wa kwetu ataondokaje wakati yeye ndiye anawatuma watekaji?
 
Amefanya uamuzi sahihi kwa sababu ameua bila sababu badala yankuwalinda wanaondamana na mali za raia.

Usifananishe na Tanzania ya mama Samia ambayo ukiandamana unapewa ulinzi wa polisi usidhurike na usidhuru, kiulaini kabisa .

Kitu ambacho miaka minne tu nyuma, hata kuthubutu ilikuwa haiwezekani. Umesahau?
 
Toka aingie Samia kuna maandamano gani yaliyofanywa na wananchi na Samia akawapa ulinzi? Au unakusudia yale maandamano ya Chadema?
 
Mnaamini kabisa hili jeshi letu la polisi akijiuzulu mtu pale ndio mambo yatakaa sawa?
 
Huyo amejiuzulu baada ya maandamano.kwa hapa Tz ni ngumu Kwa sababu watz ni waoga wa kudai haki zao.Haki huwa inapiganiwa Kwa nguvu na siyo kutegemea huruma za watawala.Hata kipindi tunadai uhuru kipindi Cha ukoloni tulipambana na wakoloni Kwa nguvu Hadi kupelekea vifo na hatimaye uhuru tukapata Bila maandamano tz msahau kupata haki.kila siku mtaendele kukamuliwa tozo na mama abdul ili Abdul azitumie kukuza makampuni yake ambayo ameyaanzisha kipindi Cha mama yake kuwa rais
 
Kuna faida gani kumlinda mtu kwenye maandamano ya wazi lakini unawasaka mmoja mmoja anayepinga mtandaoni na kumteka kumpeleka kumtesa Osterbay polisi kisha kwenda kumuulia porini Katavi au kumtupa baharini?
 
Umemuona sativa muhuni mmoja aliyejiteka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…