IGP Kenya Maandamano yamemng'oa Ofisini. Wakwetu matukio ya utekaji yatamng'oa lini?

Tumesikia wote kuwa mkuu wa Polisi Kenya kaamua kuwajibika kutokana na matendo ya polisi wakati wa maandamano ya GEN.Z na kupisha wengine.

Je, wa kwetu yeye anasubiri nini kwa matukio haya yaliyo shamiri ya utekaji na utesaji huku basdhi ya vituo vya polisi vikitajwa kuhusika na matukio hayo?

Au anasubiri atangazwe "kutenguliwa" nafasi hiyo?

PIA SOMA
- IGP Koome ajiuzulu, Ruto aridhia kujiuzulu kwake

View attachment 3040772
Hapa kwetu nafasi ya IGP inakuwa salama zaidi kadiri wakosoaji wanavyotekwa kwa wingi.
 
Tumesikia wote kuwa mkuu wa Polisi Kenya kaamua kuwajibika kutokana na matendo ya polisi wakati wa maandamano ya GEN.Z na kupisha wengine.

Je, wa kwetu yeye anasubiri nini kwa matukio haya yaliyo shamiri ya utekaji na utesaji huku basdhi ya vituo vya polisi vikitajwa kuhusika na matukio hayo?

Au anasubiri atangazwe "kutenguliwa" nafasi hiyo?

PIA SOMA
- IGP Koome ajiuzulu, Ruto aridhia kujiuzulu kwake

View attachment 3040772
Kenya watafika mbali sana.

Wameanza vizuri
 
Hapa kwetu kwa malofa mbunge wa kuchaguliwa pamoja na kumiminiwa risasi zaidi ya thelathini, IGP hakuwajibika kwa namna yoyote ile...ni laana!

.
Ila Tz hapana kwakweli khaa!!! Watu hata aibu hawana na wanshinda Makanisani na misikitini.
 
Kabisa 100%, wametuzidi elimu!.
Si elimu tu...wametuzidi busara, wametuzidi hekima na wametuzidi weledi.
Uhuru hauimbwi, hupiganiwa
Haki haibembelezwi, hudaiwa.
Amani haiombwi, ni matunda ya uhuru na haki.
 
Ni upumbavu kuona watu wanatamani machafuko kama ya Kenya. Tatizo la watanzania wengi ni exposure. Wengi wenu hamjawahi kwenda hata hapo Kenya mkajionea maisha magumu wanayoishi. Kenya wanaishi kibepari kwa 100%. Na ubepari ni unyama. Namsihi IGP Wambura asiwachekee wajinga wajinga wote wanaotamani tupitie njia wanayopitia wakenya.
 
Kuna quote moja ya anaitumia mkuu Invisible
akisema "onyesha weledi wako, ficha upumbaf wako"
inakuhusu sana hii katika maisha yako. Ni ushauri tuu
 
Back
Top Bottom