IGP kwenye suala la Lissu chutama, umatusononesha sana Watanzania kwa kumshambulia mhanga kwa maneno badala ya kutafuta wahalifu


..kwa mtizamo wangu Polisi haina haja na Lissu wala dereva.

..Lissu alikuwepo hapa Tz na alifika mpaka kwa Rpc Muroto wa Dodoma kudai apewe gari yake lakini polisi hawakumhoji.

..Kama polisi wanaamini dereva ana taarifa zinazowafaa wangeweza kuwatumia polisi wa Ubelgiji kumhoji. Huo ndio utaratibu unaotumika kwa mashahidi walioko nje ya nchi.

..Kama polisi wanaamini dereva ameshiriki tukio lile wanaweza kuwaomba Interpol na polisi wa Ubelgiji wamkamate na kumrejesha Tanzania. Huo ndio utaratibu unaotumika kukamata watuhumiwa waliovuka mipaka ya nchi yetu.

..Waliomshambulia Lissu wanaweza kukodishwa tena wakashambulia Mtanzania mwingine. Ni vizuri jeshi letu la polisi lifanye uchunguzi wa haraka kuwabaini waliohusika.
 
Nafikiri hatuelewani hapa, hayo yote uliyo sema ni sawa kwa upande wa Polisi. Je! Kwa upande wa dereva na Lissu huoni kuwa sasa waende polisi wenyewe bila shinikizo? Kusudi upelelezi uanze na pasiwe na kisingizio cha kutupiana mpira! Maana bila hivyo tunachotea maji kwenye tenga (orugega)!
 
Mambo hubadilika sana...nilidhani msiba wa Magufuli umewafundisha kujua Dunian tunapita lakini hamna.
 

..usichoelewa ni kwamba Lissu alishafika ofisini kwa Rpc Muroto wa Dodoma hakuhojiwa.

..Lissu pia alikamatwa baada ya uchaguzi na kushikiliwa na Polisi kabla Balozi wa Ujerumani hajamgomboa. Polisi hawakumhoji wakati wamemshikilia.

..Hiyo inadhihirisha kwamba Polisi hawana nia ya kumhoji Lissu.

..Kwa upande wa dereva imepita miaka 3 tangu tukio litokee. Kwanini Polisi hawashirikiani na wenzao wa Ubelgiji kumhoji? Au hawatumi maombi kwa Interpol ili arejeshwe nyumbani?

..Hivi kwa akili ya kawaida unadhani Polisi wanaweza kusubiri miaka 3 na zaidi ikiwa wanaamini dereva ana taarifa muhimu, au amehusika na tukio?
 
Anawasemea wale wote walioguswa na kuumizwa na kadhia hiyo ya kinyama.
Atafute lugha sahihi mf anaweza kusema ''sisi wana chadema"siyo kujumuisha umma wa waTanzania wote
 
Atafute lugha sahihi mf anaweza kusema ''sisi wana chadema"siyo kujumuisha umma wa waTanzania wote


Wewe unadhani hata wale waliompiga risasi wamo katika kundi la "sisi" ?!!----- common sense haikubali kabisa!! , ni wale touched tu ndio wanaozungumziwa hapa.
 
Wewe unadhani hata wale waliompiga risasi wamo katika kundi la "sisi" ?!!----- common sense haikubali kabisa!! , ni wale touched tu ndio wanaozungumziwa hapa.
Mkuu nimekutolea mf kabisa bado uwelewi?
 
Mkuu nimekutolea mf kabisa bado uwelewi?


Maana yangu ni hii haikuwa lazima awe specific kwani neno SISI linawakilisha uwingi na walioguswa kwenye kadhai ile ya kinyama ya Lissu ni wengi na sio lazima kwamba Chadema wote waliguswa kwani kuguswa ni jambo la moyoni mwa mtu hivyo neno SISI linawahusu wale ambao ni touched tu ama awe CCM, Chadema, Cuf, Act au mtu yeyote touched atakuwa kaingia kwenye SISI, na wapo CCM walikuwa touched na walienda kumtembelea hospitali Nairobi, mf, Mzee Ruksa hivyo naye yumo kwenye Sisi japo ni CCM.
 
Usiongele hisia jikite kwenye point mtoa mada alipo sema "sisi waTanzania"unaniondoaje mimi ambaye sikuguswa kabisa na tukio lile
 
kichwa kipo mchangani, nanii nje.
 
Usiongele hisia jikite kwenye point mtoa mada alipo sema "sisi waTanzania"unaniondoaje mimi ambaye sikuguswa kabisa na tukio lile
Siwazungumzii nyie mliofurahishwa na Kitendo cha Lissu kutaka kuuawa, nazungumzia wale walioguswa moyoni na jaribio lile
 
Usiongele hisia jikite kwenye point mtoa mada alipo sema "sisi waTanzania"unaniondoaje mimi ambaye sikuguswa kabisa na tukio lile


Mkuu, Angalisema; "sisi watanzania wote"--- hapo ingalikuwa ni issue, lakini kasema; "sisi Watanzania" bado maana yake ni wale watz waliokuwa touched tu,it is just a matter of common sense tu.
 
Missile of the Nation missiles are dangerous things sijui kama nia yako ni njema. Tuhuma ya kwanza ni ya kitoto, huwezi kuchunguza kama mhusika hatoi ushirikiano. Kwa mafunzo ya Kipolisi, ukikuta victim hatoi ushirikiano anakuwa treated kama ni hostile witness, atakuharibia kila kitu. Kwa nini tundulissu asiende polisi mwenyewe, kwa nini afuatwe? Aliitwa kwa IGP akakataa hadharani kwa dharau na kebehi, nadhani kuwafurahisha EU na mabwana zake mabeberu kama Sirro alivyosema. Kesi hii ni ya mchana kweupe, majambazi walionekana kwa tundulissu na dereva wake. It is pointless kumbembeleza tundulissu ajitokeze; kama hataki basi basi.

Watanzania tuko milioni 60 hatuwezi wote kuwa na body guard. CHADEMA wako milioni 10 (according to John Mrema) huwezi kuwapa wote police escort. Kuna NCCR, na Waarabu wa CUF, na UAMSHO, na Yanga, na wewe, wote mtapewa Police Escort? Why is tundulissu so special? Who is he?

La mwisho: kwa nini tundulissu kaumia upande wa kulia (kwa dereva) huku dereva hakuumia? Siku ile tundulissu alienda lunch peke yake kwa nini hata wa CHADEMA ngine hawakuenda?

Hii ya kuombewa kwa mungu barabani na viwanja vya kakobe ni private business kati yako na mungu wako, hakuna aliyewakataza. Ukitaka kuwa na T-shirt hapo hapo msikitini pia ni sawa, wewe na Paroko wako na Ustaadh na hata wakitaka ibadan kweye ubalozi wa ujerumani
 
IGP Sirro ulikuwa kioo cha jamii, lkn kadiri muda unavyokwenda mvuto wako unaporomoka kwa kasi ya kutisha!
Najua unakaribia kustaafu mkuu, legacy utakayoacha sidhani kama ni ile uliyoongia nayo. Jitafakari tena Mkuu wangu.
 
Huchunguzi jinai kwa ajili ya manufaa ya mtendewa jinai, unachunguza kwa ajili ya manufaa ya Jamhuri. Ndiyo maana lile ni kosa la jinai na si la madai!
Halafu wa kuhojiwa siyo mhanga peke yake bali mashahidi wengi, lini umewahi kusikia jeshi la polisi limemhoji yeyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…