IGP Mangu: Lugumi ilitekeleza mkataba wake na Jeshi la Polisi

IGP Mangu: Lugumi ilitekeleza mkataba wake na Jeshi la Polisi

Mbona kuna taarifa ya yule msemaji wa lugumi kuwa hivyo vifaa vimechelewa kufika kufwatia kampuni iliyopewa tenda kutokukamilisha kuzitengeneza!!? Sasa tuamini taarifa hipi kati ya msemaji na IGP?
 
Kama ni IT professional Na hujuwi kiasi hicho basi IT professional imeingiliwa Na Makajanja bila Internet unaweza je connect kwenye database ambayo iko centre?
 
Mbona kuna taarifa ya yule msemaji wa lugumi kuwa hivyo vifaa vimechelewa kufika kufwatia kampuni iliyopewa tenda kutokukamilisha kuzitengeneza!!? Sasa tuamini taarifa hipi kati ya msemaji na IGP?
Hapa kuna ukakasi mkuu
 
Wandugu hii 46,000,000,000 (46bi) ukigawa kwa vituo 108 karibu 426,000,000 (426m)... watu wa IT hii imekaaje maana hapo umeisha jenga kaghorofa kamoja kwa hizo 426m.... nna wasiwasi na hii gharama pia.....
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi – Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu amekanusha madai ya wabunge na hata taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kampuni ya Lugumi kushindwa kufunga mashine kwenye vituo vya Polisi 108 kama mkataba wake ulivyomtaka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, IGP Mangu alisema anashangazwa na habari hizo na kueleza kuwa kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mashine hizo kama ilivyokubaliana na serikali.

“Siyo kweli, watu wana ugomvi wao, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa intaneti,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.

Alipoulizwa mwenye jukumu la kufunga mtandao wa intaneti ni nani, IGP alijibu, “...ni TTCL (Kamuni ya Simu) ingawa sehemu nyingi ofisi zetu zimekatiwa huduma hiyo kwa kuwa jeshi halijalipa.”
Tatizo sio kutekeleza mkataba tu BALI pia hiyo gharama inayotajwa ya bilioni 37 kwa mashine za vituo 108 haikubaliki.
Machine moja uki-google haizidi milioni 15. Sasa iweje gharama iende huko kote?

angalia bei za machine hapa: Live Scan Fingerprinting Equipment for Biometric Identification System

Hivyo at maximum haikutakiwa kuzidi: 20 Bilioni
 
Hapa ndipo IGP amejipalia mkaa na asipokuwa makini hii story itamletea maneno mengi mpaka atajuta kusema hadharani, hivi Thamani ya hivyo vifaa ni bilion 34 ? Uchunguzi uliofanyika kwa kiina Thamani ya Hizo mashine haifiki hata bilion 1 , pesa nyingi ilizidishwa ikaliwa na wajanja wakagawana na sasa ndiyo inatumika kuwanunua wote wanaotumwa kulichunguza hilo sakata, Rushwa imetembea sana na baadhi ya mashine zimefungwa chapchap kwenye Vituo ili kumlinda Said mwema na hii Aibu , lakini Ukweli harisi pesa aliyopewa Lugumi haiendani na Thamani ya hizo mashine bali pesa nyingi imeliwa na wajanja wachache kisha kuleta vifaa ili kuwahadaa Watanzania.
kwa hiyo sasa hivi mmeshabadilisha hoja kutoka ile ya mashine hazijafungwa mpaka hii ya thamani za mashine
 
Sasa wanawekaje vifaa vinavyohitaji internet kwenye vituo ambavyo havina internet?hapa ni jipu, aliyebuni mradi huo kabla ya kuhakikisha internet inapatikana ndio jipu lenyewe.
....

.....Mkuu inashangaza kweli tunasafiri ndeeeeeeeeeeefu sana
 
Muda wote alikuwa kimya, walikuwa wanaweka nyaraka vema
Kama ilikuwa ni hivyo, kwanini mkataba umekuwa nongwa kuwekwa hadharani?

Kwanini afisa wake ameitwa na PAC na kushindwa kujibu hadi kuundwa kamati ndogo?

IGP asituambie eti kazi imemalizika, anatakiwa atuambie tenda ilitangazwa lini, malipo yalifanyikaje na mkataba mzima unasemaje

Tuliwaambia Watanzania kuna jambo!
...

....well noted Mkuu
 
Mazingira ya kupatikana IGP mpya yamekamilika,sasa ni muda wowote,kwa hiyo kamati ya bunge itakuwaje?au ndio ule mchezo pale tume ya haki za binadamu inapokagua msongamano wa wafungwa,wakijua tarehe ya ziara wanawahamisha wafungwa wanabaki wachache? Je hizi machine hazitakuwa zikihamishwa kwenda mahali Tume ya bunge inapokagua
 
Mimi ni IT proffesional na sizdhani kama hizo biometric system ili zifanye kazi zinahitaji internet connection wala sio kweli Mangu anaongea mambo asiyo yajua. Only LOcal area network inahitajika kwenye hiyo system. Anajaribu kutetea uovu huyu Mangu
...

.....nijambo la kushangaza Mkuu labda bongoland inawezekana
 
Bunge limekwisha unda kamati ya kuchunguza, nadhani tuiachie ifanye kazi yake kwanza. Baada ya hapo tutaweza kujadili yatakayojitokeza
 
Ile delay ilikuwa ni kujipanga ili wafunge hizo mashine faster faster ila hapa kuna issue za ziada kama vila pesa zilizotumika ukilinganisha na gharama halilsi zinazotakiwa.

Cha kujiuliza ni kwanini wamechelewe kujibu tuhuma hizi?Jibu langu ni kuwa, walikuwa wana-buy time makusudi ili kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na kufunga hizo mashine.Si ndio hawa walikuwa wanatupiana mpira?Leo hii majibu haya ya ghafla yametoka wapi?!

Wacha tusubiri.
 
Hujaeapwela, post: 15994967, member: 278270"]Sasa wanawekaje vifaa vinavyohitaji internet kwenye vituo ambavyo havina internet?hapa ni jipu, aliyebuni mradi huo kabla ya kuhakikisha internet inapatikana ndio jipu lenyewe.[/QUOTE]
Hoja yako ni ya msingi sana kiongozi. Kwanza tujiulize ni vituo vingapi vya polisi vina angalau desktop 4 ambazo wanatumia hata moderm tuu kupata Internet? Ikiwa kuandika tuu maelezo ni kwa mkono, tena kwa karatasi za kubangaiza, sembuse hii issue sensitive ya machine za fingerprints? Aliyekuja na hili wazo kwa level ya vituo vya wilaya ni jipu. Bora wangeanza kwa RPC, then selected district polisi stations. Halafu hii ya kusingizia Internet ya TTCL haitasaidia coz walipaswa walijue kabla. Huwezi kupoteza billions halafu uje na excuse ya aina hiyo.
 
Ile delay ilikuwa ni kujipanga ili wafunge hizo mashine faster faster ila hapa kuna issue za ziada kama vila pesa zilizotumika ukilinganisha na gharama halilsi zinazotakiwa.

Cha kujiuliza ni kwanini wamechelewe kujibu tuhuma hizi?Jibu langu ni kuwa, walikuwa wana-buy time makusudi ili kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na kufunga hizo mashine.Si ndio hawa walikuwa wanatupiana mpira?Leo hii majibu haya ya ghafla yametoka wapi?!

Wacha tusubiri.
Ninaichukia sana ccm
 
Hujaeapwela, post: 15994967, member: 278270"]Sasa wanawekaje vifaa vinavyohitaji internet kwenye vituo ambavyo havina internet?hapa ni jipu, aliyebuni mradi huo kabla ya kuhakikisha internet inapatikana ndio jipu lenyewe.
Hoja yako ni ya msingi sana kiongozi. Kwanza tujiulize ni vituo vingapi vya polisi vina angalau desktop 4 ambazo wanatumia hata moderm tuu kupata Internet? Ikiwa kuandika tuu maelezo ni kwa mkono, tena kwa karatasi za kubangaiza, sembuse hii issue sensitive ya machine za fingerprints? Aliyekuja na hili wazo kwa level ya vituo vya wilaya ni jipu. Bora wangeanza kwa RPC, then selected district polisi stations. Halafu hii ya kusingizia Internet ya TTCL haitasaidia coz walipaswa walijue kabla. Huwezi kupoteza billions halafu uje na excuse ya aina hiyo.[/QUOTE]
Lisilo wezekana kwa watu waadilifu,kwa wana ccm linawezekana
 
Sasa kama Rais anamuweza Kabwe tu tutafanyaje? Kauli moja ya makonda ilitosha kumtumbua Kabwe jukwaani lakini jipu la lugumi mpaka makoo yanatukauka tukisema maigizo tutaambiwa cyber crime Act lakini haya ya lugumi ndiyo yanayotufanya tuamini kuwa ni maigizo! Mpaka bunge limesema lakini wapi ina maana anasubiri mpaka makonda alisemee na hili?
 
Back
Top Bottom