pakaywatek
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,660
- 6,282
Hapa kuna ukakasi mkuuMbona kuna taarifa ya yule msemaji wa lugumi kuwa hivyo vifaa vimechelewa kufika kufwatia kampuni iliyopewa tenda kutokukamilisha kuzitengeneza!!? Sasa tuamini taarifa hipi kati ya msemaji na IGP?
Tatizo sio kutekeleza mkataba tu BALI pia hiyo gharama inayotajwa ya bilioni 37 kwa mashine za vituo 108 haikubaliki.Mkuu wa Jeshi la Polisi – Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu amekanusha madai ya wabunge na hata taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kampuni ya Lugumi kushindwa kufunga mashine kwenye vituo vya Polisi 108 kama mkataba wake ulivyomtaka.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, IGP Mangu alisema anashangazwa na habari hizo na kueleza kuwa kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mashine hizo kama ilivyokubaliana na serikali.
“Siyo kweli, watu wana ugomvi wao, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa intaneti,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.
Alipoulizwa mwenye jukumu la kufunga mtandao wa intaneti ni nani, IGP alijibu, “...ni TTCL (Kamuni ya Simu) ingawa sehemu nyingi ofisi zetu zimekatiwa huduma hiyo kwa kuwa jeshi halijalipa.”
Let us betAnatumbuliwa muda si mrefu huyo. Very soon!
kwa hiyo sasa hivi mmeshabadilisha hoja kutoka ile ya mashine hazijafungwa mpaka hii ya thamani za mashineHapa ndipo IGP amejipalia mkaa na asipokuwa makini hii story itamletea maneno mengi mpaka atajuta kusema hadharani, hivi Thamani ya hivyo vifaa ni bilion 34 ? Uchunguzi uliofanyika kwa kiina Thamani ya Hizo mashine haifiki hata bilion 1 , pesa nyingi ilizidishwa ikaliwa na wajanja wakagawana na sasa ndiyo inatumika kuwanunua wote wanaotumwa kulichunguza hilo sakata, Rushwa imetembea sana na baadhi ya mashine zimefungwa chapchap kwenye Vituo ili kumlinda Said mwema na hii Aibu , lakini Ukweli harisi pesa aliyopewa Lugumi haiendani na Thamani ya hizo mashine bali pesa nyingi imeliwa na wajanja wachache kisha kuleta vifaa ili kuwahadaa Watanzania.
....Sasa wanawekaje vifaa vinavyohitaji internet kwenye vituo ambavyo havina internet?hapa ni jipu, aliyebuni mradi huo kabla ya kuhakikisha internet inapatikana ndio jipu lenyewe.
...Muda wote alikuwa kimya, walikuwa wanaweka nyaraka vema
Kama ilikuwa ni hivyo, kwanini mkataba umekuwa nongwa kuwekwa hadharani?
Kwanini afisa wake ameitwa na PAC na kushindwa kujibu hadi kuundwa kamati ndogo?
IGP asituambie eti kazi imemalizika, anatakiwa atuambie tenda ilitangazwa lini, malipo yalifanyikaje na mkataba mzima unasemaje
Tuliwaambia Watanzania kuna jambo!
...Mimi ni IT proffesional na sizdhani kama hizo biometric system ili zifanye kazi zinahitaji internet connection wala sio kweli Mangu anaongea mambo asiyo yajua. Only LOcal area network inahitajika kwenye hiyo system. Anajaribu kutetea uovu huyu Mangu
shakti kumar ama shakti kapoor?Teeeeeeeeh teeeeeeeeh, naona picha ya govinda ndio inaendelea adui akiwa shakti
Ninaichukia sana ccmIle delay ilikuwa ni kujipanga ili wafunge hizo mashine faster faster ila hapa kuna issue za ziada kama vila pesa zilizotumika ukilinganisha na gharama halilsi zinazotakiwa.
Cha kujiuliza ni kwanini wamechelewe kujibu tuhuma hizi?Jibu langu ni kuwa, walikuwa wana-buy time makusudi ili kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na kufunga hizo mashine.Si ndio hawa walikuwa wanatupiana mpira?Leo hii majibu haya ya ghafla yametoka wapi?!
Wacha tusubiri.
lugumi itazimwa kwa sababu mshikaji wa karibu wa rais linamgusa, ccm hakuna mpambanaji wa ufisadi, Ni ukoo ws pnyaAnatumbuliwa muda si mrefu huyo. Very soon!
Hoja yako ni ya msingi sana kiongozi. Kwanza tujiulize ni vituo vingapi vya polisi vina angalau desktop 4 ambazo wanatumia hata moderm tuu kupata Internet? Ikiwa kuandika tuu maelezo ni kwa mkono, tena kwa karatasi za kubangaiza, sembuse hii issue sensitive ya machine za fingerprints? Aliyekuja na hili wazo kwa level ya vituo vya wilaya ni jipu. Bora wangeanza kwa RPC, then selected district polisi stations. Halafu hii ya kusingizia Internet ya TTCL haitasaidia coz walipaswa walijue kabla. Huwezi kupoteza billions halafu uje na excuse ya aina hiyo.[/QUOTE]Hujaeapwela, post: 15994967, member: 278270"]Sasa wanawekaje vifaa vinavyohitaji internet kwenye vituo ambavyo havina internet?hapa ni jipu, aliyebuni mradi huo kabla ya kuhakikisha internet inapatikana ndio jipu lenyewe.