Mbona kama vile wako kwenye msiba? Halafu hata pale anapowataka wanyoshe mikono umeona ni asilimia ngapi ya waliohudhuria wakifanya hivyo. Kumbuka kura ni siri ya mtu. Wapo wengi tu hapo wamehudhuria mradi waonekane wakiogopa kisirani cha jiwe. Wewe endelea kujidanganya na utakapozinduka kumekucha na Ikulu ina mpangaji anayestahili, ambaye hakusukumiziwa.
Halafu naona kuna kitu bado hakiwashtui nalo ni kwa nini wengi humu tunatumia majina bandia. Nani asingependa kutumia jina lake rasmi kuikosoa serikali hii ya kikatili. Ni woga na hofu waliyonayo Watanzania kwani hakuna uhuru, hakuna haki, hakuna usawa...ni udikteta mtindo moja hadi hata Hitler mwenyewe angetuonea wivu. Hii miaka mitano haina mfano wake katika karne hii!