Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Hivi nauliza igp ameshajua nan rais kama sio anapata wapi nguvu ya kumtisha mgombea kutoka chama kikubwa cha upinzani
😂😂😂😂😂 BAVICHA MNAJUA KUJIFARIJII KHAAAA😂😂😂😂 yaniii ninecheka sana, Mnavyojitoa Ufahamuu kuwa HAKUNA RAIS ZAID YA MAGU EAST AFRICA. sasa Huyu kirusi Lissu anamweza wapi Magu.....,.TANO TENA
 
Safi sana, fungia kufanya kampeni kabisa, kinukisheni sasa tuone.
Hahahaha
Nilini lissu ataenda Neccm? Naona tarehe kamavile imepita!
Tutarajie TL akirudi Moshi police post labda ndy aende tena neccm
 
Kura za polisi zote Lisu hapati

Anakwenda kusipata kwa wingi. Tundu Lissu keshawasomesha kuwa for the last 5 solid years HAWAKUWAHI KUONGEZWA MSHAHARA hata senitano. Polisi wana ukata wa kufa mtu✌️
 
😂😂😂😂😂 BAVICHA MNAJUA KUJIFARIJII KHAAAA😂😂😂😂 yaniii ninecheka sana, Mnavyojitoa Ufahamuu kuwa HAKUNA RAIS ZAID YA MAGU EAST AFRICA. sasa Huyu kirusi Lissu anamweza wapi Magu.....,.TANO TENA
Wacheka mkuu ila Mambo sio rahis Sana so weka akiba ya kicheko
 
Hivi nauliza igp ameshajua nan rais kama sio anapata wapi nguvu ya kumtisha mgombea kutoka chama kikubwa cha upinzani

Sirro hajui matokeo, lakini ameshurutishwa kuhakikisha Magufuli na chama chake cha ccm wanatangazwa washindi ili aendelee na ulaji. Kwakuwa anajua watanzania ni makondoo, basi atahakikisha anasimamia maagizo hayo, na yoyote atakayekataa hujuma ameshapewa amri ya kumfanyia ya Aqwilina, kwa kisingizio cha kulinda amani ya nchi.
 
Tupia ndani yeyote anayetaka kutusumbua wakati tukijenga Taifa letu sio kila mtu anajihusisha na mambo yao , waheshimu haki za wengine pia kwa kuacha kuondosha amani.

Safi sana kamanda Siro . Chapa kazi.
 
Jiwe kila siku anawafokea na kuwakaripia polisi mbona amwambii akaripoti polisi. Aache kutisha wananchi, asiamshe hasira za watz.


Magufuli ni Big Bosi wa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama, ni bosi wao, ...
 

Amesema hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa.

Nimeona viongozi wa Chadema wanakaripia askari, Tundu Lissu anakaripia watu wangu, namuonya sana, jana nimeongea na Mbowe, akae azungumze na watu wake watii sheria bila shuruti.

"Tundu Lissu hayupo juu ya sheria, tukiamua kutimiza majukumu yetu asilalamike,"IGP Simon Sirro

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro, amri hiyo inatokana na IGP kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na matendo mbalimbali ambayo wanayofanya.

Akifafanua suala hili IGP Sirro amesema "Nimeona matukio kadhaa yakifanyika na Viongozi wa Chadema, wamekuwa wakikaripia na kuwagombeza Askari Polisi. Nimeona mara kadhaa Tundu Lissu anagombana na Viongozi wa Polisi".

"Jana nimeongea na Kiongozi wake Bwana Mbowe akae na viongozi wake wazungumze suala la kutii sheria bila shuruti. Anayoyafanya Watanzania wenye hekima na Wazalendo wanaona. Lissu hayuko juu ya sheria polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake. Vyama vipo karibu kumi na mbili, Jeshi la Polisi limepewa wajibu wa kulinda watu na mali zao ndani ya nchi hii, yeye hana uwezo wowote wa kupambana na Jeshi la Polisi."

"Asije akafika mahali akawa na kiburi akadhani ana uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi. Niwasihi sana na niwaombe sana ndugu zetu wa Chama cha Chadema hii tabia iishe. Tundu Lissu aende akaripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro ili aende akaeleze aliyoyafanya jana. Lakini niwaombe wanasiasa na Viongozi wote katika ngazi zote. Suala la Udiwani, Ubunge, Urais bila amani na utulivu huwezi kufanya siasa na huna uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi wewe kama wewe. Kwahiyo tuheshimu sheria zilizopo ili tuchague viongozi tunaowataka lakini inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo viongozi wachache wanayoitaka ili uchaguzi usifanyike. Nawaambia uchaguzi utafanyika lakini itafika mahala tutawashughulikia sana."
View attachment 1587125

We Siro weweeee...thubutu...
 
Nafikiri Lissu ashasema hayuko yeye kama yeye. Yuko yeye na Wanachama wake, Bob Amsterdam, UN, AU vitengo vya haki za binadamu, vyombo vya habari vya kimataifa, Umoja wa Ulaya n.k

Angekuwa yeye kama yeye wala Sirro asingefanya press angekuwa kashamalizana nae huko huko. Nasubiria maneno ya utangulizi ya Lissu. Nafikiri ataripoti kituo cha polisi cha mahali alipo kwasasa hawezi kurudi Moshi.

Badala ya kuongea na Mbowe tu nafikiri kiitishwe kikao cha viongozi wa siasa, dini, polisi, tume na Serikali watu wakubaliane kuhusu HAKI itakavyotendeka na ionekane imetendeka kabla ya siku ya kura otherwise kuna hatari mbele maana uchaguzi huu wapinzani ni Sauli na Daud. Saul kajaribu kumaliza gemu nje ya uwanja toka 2017 imeshindikana.

Tunamsubiria Mungu mwenye HAKI na mwamuzi wa HAKI ambaye kisasi ni juu yake tuone analipaje kisasi uchaguzi huu.
Haki haihitaji majadiliano kwamba itendeke vipi na nani na kwa nani.

Sheria na kanuni za uchaguzi ziko wazi zifuatwe na wadau kwa usawa hakutakuwa na malalamiko yoyote.

Jeshi la polisi liache kutumika kisiasa.
 
Weshapanga, Magufuli atashinda kwa 86% and their say is a final say.
sio rahisi Kama tuzaniavyo ,Mambo ni magum mno,maridhiano ya vyama ni muhim kwa Sasa kuliko wakati wowote, nec ,vyombo vyote vya ulinzi na usalama ,kwamba mshindi atangazwe ,na alieshindwa asibugudhiwe achukuliwe Kama tunu ya taifa,ubabe kwa Sasa hauna nafasi ,taifa kwanza mengine badae,mkuu
 
sio rahisi Kama tuzaniavyo ,Mambo ni magum mno,maridhiano ya vyama ni muhim kwa Sasa kuliko wakati wowote, nec ,vyombo vyote vya ulinzi na usalama ,kwamba mshindi atangazwe ,na alieshindwa asibugudhiwe achukuliwe Kama tunu ya taifa,ubabe kwa Sasa hauna nafasi ,taifa kwanza mengine badae,mkuu
Acheni kutafuta maridhiano wakati Sisi tunawasubiri 28october tumlambishe mchanga kibaraka wa mabeberu
 
Back
Top Bottom