IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

Ukiwa na hasira sana usitoe maamuzi, kwa sababu ukitoa maamuzi, lazima utatoa boko
 
IGP Sirro amesema kuwa jeshi la polisi linaendeshwa kwa maandishi na kuna taratibu hivyo wanasubiri barua kutoka kwa waziri ili waangalie wanatekeleza vipi agizo lake.

Pia ameongeza kuwa hayo maelekezo ameyaona kwenye mitandao ya kijamii hivyo anasubiri barua rasmi ili waangalie jinsi ya kuyatekeleza hayo maelekezo ya Waziri wa afya kwani serikali inakwenda kwa maandishi.

Sirro pia amesema wataangalia kama kweli kuna jinai au lah ambayo ina haja ya kufungua mashitaka...

Na ameendelea kusema pia kama hatokuta jinai watashauri jinsi ya kumaliza hilo swala katika njia nzuri.

Source: Clouds FM

Pia soma:
- #COVID19 - Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19
hivi kuna haja ya kuwa na IGP wa hivi
 
Kuna baadhi ya Watanzania ni wapumbavu sana, yaani amri ya kumkamata Gwajiboy itoke kwa rais?

Acheni kumpa uspecial huyo tapeli ndio maana anaropoka anavyotaka.

Kipindi alivyokuwa anakamatwa na Makonda rais alihusika?
Unawafahamu wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama na majukumu yao?
 
..mimi kwa maoni yangu Polisi wamezembea kumkamata Askofu.

..unajiuliza kama maofisa upelelezi wa wilaya, na mkoa, wanafanya kazi zao sawasawa.

..kamati za ulinzi za wilaya na mkoa zinafanya kazi ikiwa mtu anaachwa anapotosha kwa muda mrefu kiasi hiki?

..Polisi walitakiwa wamkamate Askofu Gwajima muda mrefu uliopita, na maelezo na malalamiko ya Waziri ni kielelezo kwamba kuna uzembe ktk vyombo vyetu vya usalama.
Unauhakika gani kwamba kati ya Gwajima au serikali inapotokaposha? Hivi madhara ya muda mrefu tumeyaona? Vipi siku moja miaka kadhaa mbele yakatokea madhara makubwa kwa watanzania serikali ipo tayari kuwajibika?
 
Unauhakika gani kwamba kati ya Gwajima au serikali inapotokaposha? Hivi madhara ya muda mrefu tumeyaona? Vipi siku moja miaka kadhaa mbele yakatokea madhara makubwa kwa watanzania serikali ipo tayari kuwajibika?

..Askofu anasema mambo ya UONGO.

..kwa mfano, anadai ukichanjwa unakuwa na magnetic force ktk mwili wako.

..kwamba ukiweka sumaku pale ulipochanjwa sumaku itashikwa / itaganda.

..sasa huo ni UONGO wa waziwazi. Askofu alitakiwa aweke hoja za msingi ili zijadiliwe na sio kuleta uzushi.
 
Simple tu kesho atapokea barua
Hakuna wenye ubavu wa kuandika hiyo barua!! Vinginevyo wote waliowahi kupinga chanjo (akiwamo mwenyewe na naibu wake) itabidi Siro awakamate! Sirro hawezi kuhangaika na maagizo toka kwa mtu ambaye siku zake za kuwa waziri zinahesabika!
 
Hakuna wenye ubavu wa kuandika hiyo barua!! Vinginevyo wote waliowahi kupinga chanjo (akiwamo mwenyewe na naibu wake) itabidi Siro awakamate! Sirro hawezi kuhangaika na maagizo toka kwa mtu ambaye siku zake za kuwa waziri zinahesabika!
unauhakika?
 
Gwajima hakamatiki, wakizubaa Jumapili ataendeleza zoezi la kupambana na chanjo ya corona, safari hii atamshughulikia Dorothy 🤣
Wewe ni mtanzania kilaza wa mwisho kwa akili yako unafikili gwajima personally anaweza kushindana na serikali.
 
Ndiyo kuna haja tena haja kubwa tu!! Hivyo ndivyo sheria inavyotaka!! Ni kweli kunà wakati hawasubiri kupewa barua lakini hayo huwa ni makosa!
Nakubaliana nawe kabisa, maana yangu. Huyu siku zote alikuwa anakosea kamatakamata zake Leo hii anaona kesi ya sabaya baada ya kuvuliwa madaraka ndio anaona Kuna haja ya kuwa timamu
 
Back
Top Bottom