Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi halimpendelei yoyote wako kutenda haki na kulinda amani
Amewaambia wanasiasa wasiwe na hofu, Jeshi la Polisi litampigia saluti yoyote atakayechaguliwa kuingoza dola
Aidha amewataka Jeshi la Polisi, Waandishi, ZEC na NEC watimize wajibu wao. Na wanasiasa pia watimize wajibu wao ili wasiingize taifa kwenye uhalifu
Pia amesema kuna baadhi ya watu wamesema watatangaza matokeo, amesisitiza jukumu la kutangaza matokeo ni kazi ya Tume ya Uchaguzi