My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,306
IGP Sirro jana umetoa kauli nzito na ngumu mno kutolewa na kiongozi wa aina yako na mtu mwenye umri mkubwa kama wewe na mtu anayeheshimika kwa cheo chake kama wewe.
Angalia sana ulimi wako jinsi unenavyo, muombe sana Mungu akupe hekima ili kabla ya kutamka neno lolote hekima ikutangulie.
Jana ulitamka maneno haya nami nakunukuu.
"Watanzania kuweni makini msije mkazaa mtoto wa hovyo hovyo kama Hamza aliyetuletea majanga Watanzania, wazazi wa Hamza mnajisikiaje kuzaa mtoto kama huyo? Na nyie ndugu zake mnajisikiaje kuwa na ndugu kama Hamza?". Mwisho wa kunukuu.
IGP Sirro, hakuna mzazi anayepanga azae mtoto wa aina gani, Binadamu tunazaa mwili hatuzai Roho.
Kuna kijana anasumbua sana mitaani, anajitapa kwamba hakuna wa kumfanya lolote kwa sababu Baba yake ana cheo kikubwa mno serikarini, kijana huyo huvuta unga na kwenda hadi kwenye Hotel ya Baba yake iliyoko Chanika ambako hufanya vituko vya ajabu, ukiwemo kupiga watu.
Je, unajua huyo mtoto ni wa nani? Tafadhali sana, wazazi wa Hamza hawakujua kama wanazaa mtoto wa aina gani, hata wazazi wako wewe Sirro hawakujua kama ipo siku utakuja kuwa IGP.
JITOKEZE UIOMBE MSAMAHA FAMILIA YA HAMZA ILI ULINDE HESHIMA YAKO.