Wewe ndio umeongea chanzo hasa cha Kamanda kuchanganyikiwaSiro ukimwangalia mwonekano wake kimwili utadhani ni mtu wa kuheshimika sana!
Hapana, kuna wakati hata matamshi yake yalionekana kuwa ya mtu mwenye busara.
Haieleweki ni kitu gani hasa kimembadilisha akili kiasi hiki alivyokuwa sasa?
Unajua, inasemekana damu za binaadam zikimwagwa kwa uonevu tu, hazimwachi mtu anayesababisha zimwagike, ni lazima atadhurika tu kwa njia moja au nyingine.
Siro ni mhanga wa umwagaji wa damu za waTanzania ambao hawakustahili kuuliwa au kuumizwa.
Maisha yake ya uhai wake uliosalia yatakuwa ya matatizo tupu.
Damu za watu ziko juu yake.